MAFANIKIO NA UTAJIRI: WATU WENGI UMETOKANA NA FALSAFA HIZI 7 ZA FEDHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAFANIKIO NA UTAJIRI: WATU WENGI UMETOKANA NA FALSAFA HIZI 7 ZA FEDHA

 

Matajiri Aliko Dangote na Elon Musk
Kabla ya kuanza somo letu la leo rasmi, kwanza nikushukuru kwa kusoma blogu hii, mahali sahihi  ambapo siku zote umekuwa na utaendelea kupata makala adimu zinazohusu  fedha kwa mapana yake.

Elimu ya fedha na umuhimu wake limekuwa ni jambo lisiloweza kukwepeka kwa mtu yeyote yule anayetafuta mafanikio ya kimaisha kwenye Dunia hii ya karne ya 21. Pamoja na makala tunazoandika hapa kwenye blogu hii, pia ukipenda kupata elimu ya fedha ile ‘cream’ kwa kina zaidi, basi karibu ujiunge na familia yetu Group na Channel ya Michanganuo-online.(MASTERMIND GROUP 2021)  Kila siku jioni tunakuwa na masomo ya kipekee(exclusive) yasiyoweza kupatikana mahali kwingine kokote!

Kujiunga tuwasiliane kwa watsap namba, 0765553030 au 0712202244, tuna maktaba ya masomo zaidi ya 100 ya siku za nyuma na kila siku tunajifunza somo jipya la kipekee.

Yamkini wewe ndio kwanza unaanza safari yako ya kifedha, au labda tayari ulishaianza kitambo lakini bado hujafanikiwa kuufikia ule uhuru wa kifedha unaotamaniwa na karibu kila binadamu aliyezaliwa na mwanamke.  Lengo kubwa la kila mtu akiwa hai ni siku moja hatimaye kuja kumiliki rasilimali(assets) za kutosha zenye uwezo wa kuzalisha au kutengeneza kipato ambacho kitakuwa chanzo cha pesa za kulipia gharama zote za maisha.

SOMA: Utajuaje kama umeufikia uhuru kamili wa kifedha?

Je na wewe pia unayo ndoto hii? Basi hapa chini  leo nimekuandalia falsafa 7 ambazo zimejaribiwa na kufanyiwa kazi kwa miaka mingi na watu mbalimbali waliofanikiwa kifedha miaka na miaka huko nyuma lakini mpaka hivi leo na hata siku zijazo. Ni imani yangu zitakusaidia katika safari yako ya kifedha kama na mimi pia zinavyoendelea kunisaidia.

1. Weka Malengo

Umekuwa kila mara ukisikia maneno haya, “weka malengo….weka malengo…..weka malengo….” na naamini mpaka sasa hivi pengine umeshachoka nayo na hutaki tena kuyasikia lakini nakupa moyo usichoke, endelea tu kuyasikia ila kitu cha muhimu zaidi lifanyie kazi na ipo siku utakuja kuyakumbuka haya maneno yangu.

Kabla hujajiwekea malengo yeyote unapaswa kwanza kuwa na maono ya kile unachokitaka, (Katika kitabu changu kimoja kiitwacho, MIFEREJI 7 YA PESA, nimeainisha Malengo, Dhamira, Maono, Dira na Ndoto kwa kina sana) kwanini unakitaka kitu hicho na ni lini unakitaka. Ni vigumu kufikia mafanikio yeyote ikiwa kama hutobainisha mafanikio hayo kwa uwazi.

SOMA: Kanuni kuu ya mafaniki Duniani iliyo kubwa kuliko zote

Kwa mujibu wa kitabu hicho amini katika kuweka malengo yako ukizingatia kanuni iitwayo kwa kimombo S.M.A.R.T au kwa kiswahili tunaweza kuiita isivyorasmi “Ma.Pi.Fi.Fa.Mu” kwa kirefu malengo yanapaswa yawe; Maalumu, yawe yana Pimika, yawe yana Fikika, yanayoFaa na yenye Muda maalumu wa utekelezaji;

S: Specific,

M: Measurable

A: Attainable/Relevant

T: Time based

Kwa mfano ikiwa una lengo la kupunguza deni unalodaiwa, badala tu ya kusema utapunguza deni, sema ni kiasi gani hasa unachotaka kupunguza, lini na pia ni kiasi gai unataka upunguze kwa siku, kwa mwezi na hata kwa mwaka ili kuweza kumaliza deni lote unalodaiwa katika muda ule uliojiwekea katika lengo lako.

Au inawezekana labda wewe lengo lako ni kujiwekea akiba ya fedha za kutosha kununulia kiwanja kwa ajili ya kujenga nyumba ya kuishi au hata ya kupangisha wapangaji wakuletee kodi kila mwisho wa mwezi. Hakuna ubaya wa kuwa na lengo kama hilo lakini je, lengo lako hilo ni S.M.A.R.T? Unahitaji pesa kiasi gani hasa? Ni lini na siku gani utazihitaji? Ni mabadiliko yapi uliyo tayari kuyafanya kusudi uweze kulitimiza lengo lako hili?

2. Fanya Ufuatiliaji.

Ikiwa unataka mafanikio kwenye jambo lolote lile maishani, fanya ufuatailiaji! Ni hivi, huwezi kujua ni wapi unakokwenda ikiwa hujui pale ulipo sasa. Mara utakapokuwa umejiwekea lengo lako, fuatilia maendeleo yake na uyapime kulingana na malengo MA.PI.FI.FA.MU (S.M.A.R.T) Kwenye jambo hili unatakiwa kutafuta njia utakayoweza kuitumia kujua hasa umepunguza deni kiasi gani, ni kiasi gani kilichosalia, umepunguza matumizi yako kiasi gani? Ni kiasi gani kimeongezeka katika thamani ya mali zako unazozimiliki na ni kiasi gani pia mapato yatokanayo na vitegauchumi vyako yameongezeka.

Jeff Bezos na Elon Musk

Mfano mzuri ni pale mtu anapotunza kila rekodi ya miamala anayoifanya katika kitabu ama daftari lake la mahesabu. Ikiwa hutafuatilia mahesabu yako ya fedha unaweza siku moja ukaja kupata mshangao mkubwa pale utakapokuja kuamua kufuatilia. Ikiwa unataka kuweka akiba, huna budi kwanza kufahamu matumizi yako ya kila siku. Na ikiwa pia utataka kukuza mali zako ni lazima kila mwezi ufahamu ni kiasi gani zimeongezeka.

3. Fanya uwekaji Akiba kuwa Kipaumbele chako cha Kwanza

Kuweka akiba ndiyo njia ya kweli na ya uhakika ya kutengeneza utajiri iliyofanyiwa majaribio na kutumiwa na watu wengi duniani. Utamsikia kila mtu akisema lake, wengine watakuambia  uweke akiba asilimia 10% ya mapato yako, wengine asilimia 20% nk. Lakini kiukweli ikiwa utataka kujenga utajiri haraka unaweza kuweka akiba hata asilimia zaidi ya 50% ikiwa mazingira yataruhusu.

4. Lipa Madeni Unayodaiwa

Umeshaweka akiba yako, sasa utaifanyia kitu gani? Ikiwa unayo madeni ni jambo zuri ukayapunguza au kuyalipa yote kwanza. Haijawahi kutokea hata siku moja mtu akatajirika angali ana madeni mabaya. Ukiwa na deni hutofautiani na mtu aliyetia nanga ufukweni mwa bahari na wakati huohuo akitarajia kushinda mbio za majahazi. Deni ni kizingiti kwenye safari yako ya kifedha. Anza kulipa madeni yale yaliyokuwa na riba kubwa kwanza na ikiwezekaha hata yalipe yote ili uanze freshi/upya.

5. Wekeza pesa zako.

Na sasa umeshamaliza kulipa madeni yako yote, unaweza ukasheherekea kidogo, lakini kumbuka huu ndio muda muafaka wa wewe kufanya biashara na ongezeko la fedha zile ulizokuwa ukitumia kulipa madeni. Ikiwa kama kweli upo makini(serious) kujijengea utajiri unatakiwa kununua vitegauchumi vile vilivyo na tabia ya kuongezeka thamani kadiri muda unavyopita mfano ardhi, hisa za makampuni nk. na wala siyo vitegauchumi vile vinavyopungua thamani kama vile gari, TV na Simu. Kitegauchumi kinachoongezeka thamani chaweza pia kikawa ni biashara yeyote ile ilimradi tu iwe ni biashara inayoingiza faida na siyo hasara.

SOMA: Wanaofanikiwa maishani wengi husema 'no'(hapana) kwa vitu hivi vitatu 3 

Jitahidi sana kuwekeza katika miradi isiyokuwa na hatari kubwa hasa ikiwa wewe ni mwajiriwa usiyekuwa na muda mwingi wa kufuatilia vitegauchumi vyako au uwekezaji.

6. Tengeneza Kipato Zaidi.

Tayari uneshajiwekea malengo,Umefuatilia malengo yako zikiwemo na hesabu za fedha zako vizuri, umeweka akiba asilimia kubwa ya kutosha katika mapato yako ya kila siku, umelipa madeni yako  na kufanya uwekezaji. Sasa ni nini kitafuata? Kinachofuata ni kuzidisha mara dufu mzunguko wako wa uwekezaji na kuweka akiba kwa kuongeza kipato chako.

Ikiwa wewe ni mwajiriwa mahali fulani fikiria ni nini utakachokifanya ili kuongeza thamani katika kampuni uliyopo, mfano kuongeza ujuzi/elimu nk. Kama ni mfanyabishara fikiria utafanya kitu gani kuongeza mauzo yako? Unaweza pia kufikiria kuhusu kufungua biashara ya pembeni zaidi ya ile uliyokuwa nayo au kazi unayofanya. 

SOMA; Ujanja Matajiri wanaoutumia kupata pesa kutoka vyanzo vingi vya mapato. 

Je, kuna kitu chochote kile una mapenzi nacho na ungependa kuwashirikisha wengine mfano biashara mbalimbali za kwenye mtandao? Kwa kadri utakavyojitahidi kwa kasi kuongeza kipato chako kwa  njia mbalimbali ndivyo pia utakavyoweza kuufikia uhuru wako wa kifedha haraka zaidi.

Hitimisho:

Kuna njia nyingi za kutengeneza Utajiri, lakini mbinu na falsafa nilizozielezea katika makala hii zimedhibitika kufanya kazi kwa watu wengi waliowahi kupata mafanikio makubwa. Jambo la msingi tu ni wewe kuchukua hatua ya kwanza.

………………..mwisho…………………

 

 

BIDHAA NA HUDUMA MBALIMBALI TUNAZOTOA

1.  Kitabu cha THINK & GROW RICH kwa lugha ya Kiswahili sasa unaweza kukipata popote pale ulipo. Kwa nakala tete(softcopy) bonyeza kiungo kifuatacho, THINK & GROW RICH-SWAHILI-EDITION, na kisha fuata maelekezo, ukimaliza kulipia kupitia mtandao wako wa simu utakidownload kwenye smartphone yako.

Kwa nakala Ngumu(Hardcopy) kitabu kinapatikana kwa wakala wetu mkuu, Bright Bookshop & Stationery iliyopo Mbezi-Kimara jirani na Sekondari ya St. Augustine au Kanisa la KKKT Mji mpya. Unaweza kupitia njia ya Temboni au Kibanda cha Mkaa,  Bei ya kitabu ni sh. 25,000/=

Kwa Dar es salaa tunatoa huduma ya Delivery popote mteja alipo kwa gharama ya sh. 2000/=

Mikoa mingine yote Bara na Zanzibar tunatuma kwa mabasi au boti na gharama zote pamoja na kitabu ni Tsh.35,000/=

2.  Vitabu vyetu vingine vyote pia vinapatikana: MICHANGANUO & UJASIRIAMALI, DUKA LA REJAREJA na MIFEREJI 7 YA PESA

3.  Kujiunga na MASTERMIND Grop letu la masomo ya fedha kila siku na michanganuo ya biashara zinazolipa Tanzania katika group la whatsap & Channel ya telegram, lipia kiingilio cha mwaka mzima sh. Elfu 10 tu kwa namba 0765553030 kisha tuma ujumbe, ‘NIUNGE NA MASTERMIND GROUP 2021/2022’  kisha nitakutumia bure vitabu na michanganuo pamoja na kukuadd katika hilo group na channel ya telegram muda huohuo.

4.  Na ile huduma ya kuandikiwa MCHANGANUO WA BIASHARA(Business Plan) kwa biashara yeyote ile kitaalamu nayo inapatikana kwa gharama ya asilimia 1% ya mtaji wa biashara husika, lakini mazungumzo pia yapo.

 

MAWASILIANO YETU NI: 0765553030 au 0712202244        

0 Response to "MAFANIKIO NA UTAJIRI: WATU WENGI UMETOKANA NA FALSAFA HIZI 7 ZA FEDHA "

Post a Comment