MAMBO 7 KUHUSU KITABU CHA MIFEREJI 7 YA PESA ULIYOKUWA PENGINE HUJAYAJUA BADO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAMBO 7 KUHUSU KITABU CHA MIFEREJI 7 YA PESA ULIYOKUWA PENGINE HUJAYAJUA BADO


1.  Kitabu hiki kina kurasa 52, kinabebeka kiurahisi na kusomeka bila matatizo.

2.  Ndiyo kitabu cha kwanza kabisa nchini Tanzania cha elimu ya pesa na mafanikio kuandika juu ya MIFEREJI 7 YA PESA(KIPATO), Siri kubwa za matajiri ambazo zilikuwa hazizungumzwi mara kwa mara, na masuala yote yahusuyo maendeleo binafsi ya mtu kama vile njia bora kabisa za kujiwekea malengo maishani, matumizi mazuri ya muda, nidhamu ya hali ya juu ya pesank.

3.  Kitabu hiki kila aliyewahi kukisoma, atakwambia kimempa hamasa isiyomithilika katika masuala ya utafutaji pesa na maisha kwa ujumla,(Nilishangazwa na mteja mmoja aliyepiga simu akikita kitabu hicho kwa mara ya pili akidai kopi ya kwanza imechakaa kuna baadhi ya kurasa hazisomeki vizuri na angependa kuwa nacho kwa muda mrefu hata ikiwezekana mjukuu wake aje akikute)

4.  HESABU MUHIMU ZAIDI KATIKA BIASHARA ni somo jipya lililoongezwa kwenye kitabu hiki katika toleo lake jipya ambalo limefanyiwa marekebisho makubwa, somo hili siyo la kukosa kwani ndilo huwafanya watu wengi kutajirika au kuendelea kubakia katika hali za kawaida za kiuchumi(average persons).

5.  Wengi waliokinunua husema bei yake hailingani kabisa na yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu, kuna watu waliodiriki hata kusema ingefaa kiuzwe shilingi elfu 12. Lakini sera na dhamira ya mtunzi wa kitabu hiki tangu mwanzo ilikuwa ni kumfanya angalao kila Mtanzania anaye ‘struggle’ na maisha akisome.
MIFEREJI SABA  7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA
Mifereji 7 ya Pesa.
6.  Hakuna kitu kibaya kinachoweza kuigwa na watu, kitabu hiki kudhihirisha kwamba kimewahamasisha watu wengi(inspire many peple), ambalo ndilo lililokuwa lengo kuu la mwandishi, wamejitokeza waandishi wengi chipukizi walioiga maudhui na hata yaliyomo ndani ya kitabu hiki na kuandika katika blogs na wengine hata kutunga vitabu, kwa mfano wapo badala ya kuandika mifereji 7 ya pesa wameandika mifereji 8,9 na hata 10 ya pesa. Hili siyo jambo baya ilimradi tu wameweka ubunifu kidogo, na hicho ndiyo kitu mwandishi wa kitabu hiki hasa anachosisitiza.

7.  Kitabu hiki unaweza kukipata ukiwa popote pale ndani na nje ya Tanzania. Hapa Dar es salaam tuma meseji au piga simu utaletewa mpaka pale ulipo kwa shilingi elfu 5 tu. Mikoani tuma jumla shilingi elfu 10 kama upo mkoa wa mbali au shilingi elfu 9 kwa mikoa ya karibu, tuma pia na jina la basi linalofika hapo unapoishi tutakutumia kitabu. Kama utataka kitabu hicho kwa njia ya e-mail, tuma shilingi elfu 3 tu pamoja na anuani yako ya e-mail na tutakutumia softcopy au PDF ya kitabu hicho. Namba za simu ni, 0712 202244  AU  0765 553030 Jina litakalojitokeza ni; Peter Augustino Tarimo



0 Response to "MAMBO 7 KUHUSU KITABU CHA MIFEREJI 7 YA PESA ULIYOKUWA PENGINE HUJAYAJUA BADO"

Post a Comment