KWANINI NI HATARI KUKOPA AU KUWAKOPESHA NDUGU NA JAMAA ZAKO WA KARIBU?

usimkopeshe ndugu, jamaa au rafiki kiholela utajuta
Upo usemi kwamba kumkopesha ndugu au rafiki matokeo yake ni kupoteza vyote viwili, pesa zako pamoja na undugu au urafiki wenyewe. Kauli hii binafsi nimewahi kuishuhudia kivitendo katika pande zote mbili, kumkopesha rafiki na pia kukopeshwa na ndugu/jamaa.

Kukopeshana baina ya ndugu, jamaa au rafiki ni moja ya njia ya kupata mkopo wa haraka lakini mara nyingi hakuambatani na masharti yeyote yale yanayolenga kuja kumbana mkopaji ili aweze kuona umuhimu wa kulipa wala huwa watu hawawekeani muda maalumu wa marejesho zaidi ya kila mmoja kujua tu ipo siku watarudishiana pasipo kutilia maanani usemi ule usemao, kukopa harusi, kulipa matanga.

SOMA: Kutumia kiwanja, nyumba au ardhi kama rehani kuomba mkopo ni sahihi? Naomba ushauri.

Katika upande nilioona ni mgumu zaidi ni ule wa kumkopesha ndugu au rafiki. Ijpokuwa inaweza kudhaniwa kuwa mkopaji ndiye anayeteseka zaidi pale anaposhindwa au kuchelewesha kulipa ukweli ni kwamba wewe mkopeshaji unaweza kuwa ndiye mhanga zaidi wa adha hii.

Unaweza hata usiwe na mawazo ya kumdai lakini kila utakapomuona mdaiwa wako unahisi kama vile hajisikii vizuri, unatamani hata kumwambia nimesamehe deni lenyewe lakini unashindwa. Hali hii mwishowe humfanya mkopeshaji kumkwepa mkopaji na mkopaji naye anapoona hivyo hupatwa na wasiwasi na kujisikia mnyonge muda wote.

SOMA: Kuendeha biashara bila mtaji au mtaji kidogo ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini.

Utawasikia wengine wakitoa kauli mfano, Ni heri hata kukopa Mpesa, Tigo pesa, airtel money au hata mtandao wowote ule wa simu zikiwemo kampuni za kukopesha mkopo online kama vile Tala na Branch kuliko kumfuata ndugu, jamaa au rafiki wa karibu kumuomba akukopeshe mkopo rahisi. Wapo pia wanaoona ni heri kukopa pesa benki kutawapa Amani ya moyo.

Hatari nyingine ya kumkopesha ndugu au rafiki ni kwamba huwezi kumchaji riba, mara nyingi ni mkopo bila riba. Kwanza tu kumtajia sual la riba tayari ataona kama vile unataka kumfanya yeye kitegauchumi chako jambo litakaloleta manunguniko makubwa ndani ya familia, ukoo au baina ya pande mbili zinazofahamiana vyema.

SOMA: Sababu kubwa 9 duniani kwanini watu hukopa pesa, 4 kati yake ni za kuogopa kama ukoma.

Familia hushindwa kukaa pamoja hata katika vikao kutokana na mdaiwa kuwa na hofu ya kukaa karibu na mdai hasa ikiwa mdai ni mtu asiyeweza kujizuia kuwatangazia wanafamilia au wanandugu wengine. Mdaiwa hatimaye anaweza akatengwa hata na wanafamilia wengine wakidai ni kwanini hataki kulipa deni.

Lakini pia hatari nyingine ni kwamba mkopaji hugeuka kama mtumwa kwa mkopeshaji kwani hujikuta akilazimika kukubaliana na kila kitu atakachosema mkopeshaji hata kama hoja zenyewe siyo sahihi na hazina mashiko, huwezi kumpinga kwa lolote.

SOMA: Kabla ya kukopa mkopo wa biashara yako, pambana kiume kwanza usije kuumbuka bure!

Mkopaji pia anaweza akaja na kuomba kupewa tena mkopo mwingine. Badala sasa ya kuwa umemsaidia mara moja inakuwa ndiyo njia ya kumfanya asijishughulishe tena na kazi bali kila mara atarudi kwako kutaka msaada zaidi. Anageuka mwiba kwako.

Si hivyo tu kwani wanandugu au marafiki wengine wakishajua unakopesha nao humiminika kwako kuja kuomba mkopo rahisi/nafuu usiokuwa na riba wala masharti ya kuwabana wasiingie mitini kama ilivyo mikopo ya mabenki mfano CRDB, NMB, ACCESS, AKIBA, DCB, EQUITY na mengineyo mengi nchini Tanzania .

Wewe uliyekopesha hali yako kifedha inaweza ikageuka na kuwa mbaya ghafla ukahitaji kurudishiwa fedha zako na mkopaji/wakopaji lakini itakuwa vigumu sana kukulipa na hata wengine wanaweza watakubeza usiamini kabisa kama ni wao waliokuja mikono nyuma kutaka uwakopeshe bila riba. Mpaka unaweza ukajiuliza hivi kukopesha au kukopa ni dhambi? mbona nanyanyasika hivi na pesa zangu mwenyewe.

SOMA: Biashara ndogo rahisi kwa wajasiriamali zinazoendana na wakati tulio nao.

Suluhisho la yote hayo.
Mapenzi yako kwa ndugu, jamaa au marafiki hayapaswi kabisa kupimwa kwa ukarimu uliokuwa nao, lakini pia kwa kuwa ni vigumu sana kulitekeleza hili kivitendo...............

...........................................

Somo hili halijamalizika bado na linaendelea katika GROUP LA WATSAPP LA MICHANGANUO-ONLINE pamoja na Channel yake ya TELEGRAM

Mpenzi msomaji wa masomo haya, si lengo langu kuu kukatisha masomo haya kwa nia ya kuvutia watu walipie hapana, bali hii ni njia ninayoweza kwa urahisi kukujulisha wewe ulie na nia ya kujifunza zaidi ya makala za kawaida ninazoweka hapa. 

Sisemi makala za kawaida si nzuri hapana lakini hata ningeamua kuweka kila kitu tu hapa bloguni bado kuna watu wengine hawataona umuhimu wa kufuatilia kila siku ndio maana tukaona ni vizuri tuwe na baadhi ya masomo ambayo mtu atachangia gharama kidogo sana ya sh. elfu 10 kwa mwaka mzima kusudi aweze kuyachukulia masomo hayo kwa uzito unaostahili.

Hata hivyo tutaendelea kuweka makala nzima kama ilivyokuwa kawaida na hizi za kulipia ni sehemu tu ya makala zote kwa ujumla katika blogu hii. Unaweza ukasearch makala nyingi tu nzuri na za bure katika blogu hii bila kulipia chochote.

IKIWA UNGEPENDA KUJIUNGA NA GROUP LETU LA WASAP & CHANNEL YA TELEGRAM BASI, UNAKARIBISHWA UTOE KIINGILIO CHAKO SH. ELFU 10 KUPITIA NAMBA ZETU, 0765553030  AU 0712202244 JINA NI PETER AUGUSTINO TARIMO, KISHA TUMA UJUMBE USEMAO HIVI;

"NIUNGE NA GROUP LA MICHANGNAUO-ONLINE PAMOJA NA OFFA YA VITU 7,VITABU NA MICHANGANUO"


Kwa vitabu vyetu na Michanganuo ya biashara mbalimbali tembelea Duka letu mtandaoni la SMART BOOKS TZ

0 Response to "KWANINI NI HATARI KUKOPA AU KUWAKOPESHA NDUGU NA JAMAA ZAKO WA KARIBU?"

Post a Comment