SEMINA SIKU YA 3: MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUSAGA NAFAKA (DONA) HATUA KWA HATUA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA SIKU YA 3: MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUSAGA NAFAKA (DONA) HATUA KWA HATUA

Kabla hatujaendelea na sehemu yetu hii ya 4, ningependa kusisitizia kidogo mambo haya mawili yafuatayo; 

1. Kumbuka kwamba sehemu hii ya soko ndiyo muhimu sana kwa mjasiriamali yeyote yule kwani biashara bila soko la uhakika haiwezi kuwa endelevu. Lakini soko halizuki tu hivi hivi kama uyoga porini hapana. Ni lazima ulitengeneze, ni biashara chache sana siku hizi hupata bahati ya kujiuza zenyewe, usemi ule wa kale, “Kizuri chajiuza, na kibaya chajitembeza” umegeuka “vice versa”.

2. Pia nikukumbushe tena kwamba, jipatie mchanganuo kamili wa USADO Milling kwani licha ya kuutumia ukifuatilia semina hii lakini utajifunza mambo mengi kuhusiana na ubunifu katika kiwanda chochote kile kidogo. Unaweza  ukatumia baadhi ya mikakati iliyotumika katika mchanganuo huu kwenye biashara yako unayotarajia au uliyokwisha ianzisha tayari hata kama siyo ya usagishaji nafaka. Bei yake ni sh. Elfu 10 tu, nakutumia kwenye simu yako pamoja na offa ya vitabu na michanganuo mingine mizuri.

Hebu sasa tuendelee na semina yetu………4.0 TATHMINI YA SOKO
Maelezo mengi kwenye Sura hii yanatokana na majibu ya utafiti ule wa soko. Vipengele vinavyotakiwa kuelezewa ni hivi vifuatavyo ingawa katika Mpango wa USADO inawezekana kuna vilivyoachwa au kuna vilivyoongezeka pia;

4.1 Mgawanyo wa soko
4.2 Soko lengwa
4.2.1 Mahitaji ya soko
4.2.2 Mwelekeo wa soko
4.2.3 Ukuaji wa soko
4.3 Tathmini ya sekta
4.3.1 Washiriki katika sekta
4.3.2 Usambazaji
4.3.3 Ushindani
4.3.4 Washindani wako wakubwa

Kama kawaida baada ya kuacha nafasi ndogo ya Muhtasari nitaenda kuanza moja kwa moja na kipengele kidogo cha “4.1”

4.1 Mgawanyo wa soko
Kwenye mgawanyo wa soko nimeelezea kwanza soko USADO inalolilenge kwa ujumla kwamba ni eneo zima la jiji la Dar es salaa na Mkoa wa Pwani. Lakini nazidi kuchuja soko hilo kwa kutaja vipande au makundi 3 ya wateja inaowalenga ambao ni Maduka ya rejareja, Maduka ya jumla na Wanunuzi mmoja mmoja wa dona. Kisha kila kundi au kipande nimekielezea sifa zake zikoje.

4.2 Mkakati wa Soko lengwa
Hiki ni kipengele kingine kidogo kwenye Soko na kama tulivyoona kile kilichotangulia, hiki tunazidi kuchuja ili kupata kipande cha soko kinacholengwa zaidi ambacho ni kundi au kipande cha “Maduka ya rejareja”. Naweza pia kuelezea ni kwanini kampuni imeamua kuchagua kipande hiki cha soko, uhusiano wake na vitu kama bei, ubora nk.

4.2.1 Mahitaji ya Soko
Hiki ni kipengele kidogo kwenye soko lakini chini ya kipengele kidogo cha soko lengwa hapo juu na kinaelezea namna soko lengwa linavyohitaji bidhaa ya unga wa dona. Nilionyesha kulingana na utafiti uliofanyika wingi wa watu au kaya zinazohitaji unga wa dona kila siku katika mikoa ya Pwani na Dar es salaam hivyo kufanya maduka ya rejareja kuwa na mahitaji makubwa ya kuuza unga wa dona.

Nikaelezea pia ni kwanini wateja hupendelea sana kula dona lakini ajabu ni kwamba huwa hawanunui dona na badala yake hununua zaidi sembe. Katika utafiti unajua wateja walipoulizwa walijibu kitu gani? Basi ndicho nilichokiandika hapo kisome.

4.2.2 Mwelekeo wa soko
Ni kipengele kingine kidogo chini ya soko lengwa na nimeelezea mielekeo kwa maswala mbalimbali yanayoweza kuliathiri kundi hili la soko linalolengwa. Masuala hayo 3 niliyataja kuwa ni, Hali ya kisiasa, Hali ya hewa na Hali ya Ulaji wa watu.

4.2.3 Ukuaji wa Soko.
Katika kipengele hiki nimejaribu kuonyesha jinsi soko linalolengwa na USADO uwezekano wake wa kukua ulivyo na nikataja takwimu mbalimbali kwa mujibu wa Mamlaka ya Takwimu ya Taifa (NBS), mamlaka nyingine za serikali kuu na serikali za mitaa. Takwimu hizi hupatikana kwenye utafiti wa dawati uliofanywa kabla ya zoezi hili kuanza.
4.3 Tathmini ya Sekta
Hiki ni kipengele kidogo kinachojitegemea katika Sura ya soko na nimeielezea sekta nzima ya Usagishaji nafaka nchini, washiriki wake na muelekeo wake kwa ujumla ulivyo.

4.3.1 Ushindani
Ni kipengele kidogo cha Soko lakini chini ya kile cha ‘Tathmini ya Sekta’ na katika hiki nilitaja ushindani kwenye sekta ya usagishaji nafaka, wadau hasa hushindania kitu gani. Pia nikataja washindani wakuu wa USADO Milling ni kina nani, wana sifa zipi na USADO Milling wanatofautiana vipi na hawa washindani wote watatu.

SEMINA SIKU-2                SEMINA SIKU-4


Mpaka kufikia hapo ndugu msomaji wangu sehemu hii ya 4, Tathmini ya soko ndio tunafika tamati lakini sehemu ya 5, Mikakati na Utekelezaji ni siku ya kesho Mungu akitujalia afya.

Usisahau kujikinga, Barakoa ni muhimu hata ukikosa ya kununua kuwa mbunifu mwenyewe, jitengenezee hata ya leso na raba bendi inasaidia ilimradi iwe na layer 2 kuliko kutembea bila kinga yeyote hasa maeneo hatarishi kama sokoni, stendi za mabasi na hospitalini. Mtu anaweza akapiga chafya ghafla au kukohoa matonetone yatatua juu ya leso au barakoa yako badala ya puani au mdomoni moja kwa moja.
…………………………………..

0 Response to "SEMINA SIKU YA 3: MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUSAGA NAFAKA (DONA) HATUA KWA HATUA"

Post a Comment