MIKAKATI (2) YA PESA, WA SUNGURA NA WA KOBE: JE, WEWE UNATUMIA UPI KATI YA HIYO? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MIKAKATI (2) YA PESA, WA SUNGURA NA WA KOBE: JE, WEWE UNATUMIA UPI KATI YA HIYO?


MBIO ZA SUNGURA NA KOBE
Ingawa nimeanza na mkakati wa pesa wa Sungura na Kobe, si nia yangu kusimulia hadithi za Cheichei hapa bali lengo langu hasa ni ili ndugu msomaji uweze kupata picha halisi ya kile ninachotaka kukielezea. Tukirudi kwenye mada, leo nataka nifanye rejea kidogo kwenye kitabu kimoja maarufu sana duniani cha fedha kilichoandikwa na Bwana Robert Kiyosaki cha Rich Dad Poor Dad

Kwa waliowahi kukisoma, Assets(Rasilimali) ni moja kati ya vitu au mawazo makubwa yaliyotawala katika kitabu hiki. Kwa maana rahisi kabisa unaweza ukasema, Asseti ni kitu kilichokuwa na uwezo wa kukuingizia pesa mfukono mwako bila kujali kama umefanya kazi ama la. Mifano mbalimbali ya asseti ni kama hii ifuatayo;

·       Account yako ya kudumu ya benki
·       Hisa zinazokua
·       Biashara
·       Ardhi nk.

Unaweza kuona hapo nimetaja biashara kwasababu biashara inakuingizia pesa, lakini hutegemea pia na biashara kwani biashara zipo za mifumo tofauti, na biashara unayoweza kuiita asseti ni ile ambayo haitegemei sana muda wako au nguvu zako moja kwa moja ili ikuingizie fedha. Chukua mfano labda una nyumba ya wageni, hii ni assseti nzuri kushinda duka unalokaa peke yako pale kwani hutakaa pale muda wote kusimamia biashara ndipo ikuingizie pesa ingawa pia hata duka linaweza kuwa asseti nzuri kulingana na namna utakavyoamua kuweka mfumo wako wa usimamizi. Ajira  siyo asseti kabisa bali ni njia ya kuingiza tu pesa kwa sababu usipokuwepo pale na pesa pia hamna kabisa.

SOMA: Maajabu ya kununua na kuweka asseti kidogokidogo kama njia ya kutajirika kwa pesa kidogo.

Watu wengi huchukulia asseti kama vile ni lazima iwe vitu vikuubwa sana kama majumba labda, mahekari ya ardhi nk. lakini hapa tuchukulie tu mfano wa mtu anayeamua kununua friji kama asseti yake. Friji ni asseti kwasababu inaweza ikakuingizia fedha kupitia kuuza icecream, maji baridi, soda nk. Mtu anayemiliki mashine ya kukamulia juisi ya miwa au pikipiki ya bodaboda huwezi ukamlinganisha na mtu asiyekuwa kabisa na vitu hivyo.

Vifaa hivyo hata ikiwa hatavitumia yeye mwenyewe lakini bado anao uwezo wa kuingiza pesa kwa kupitia njia ya kumkodishia mtu mwingine kwa masharti watakayokubaliana wawili. Kwahiyo hapo ni asseti zinamuingizia pesa bila ya yeye mwenyewe kufanya kazi au akifanya kazi zingine, hapa pesa inamfanyia kazi na si yeye anaifanyia pesa kazi.

SOMA: Sababu 5, kwanini masikini wengi hawafanikiwi kirahisi (Nakosea wapi part ii)

Na hapo tumezungumzia tu asseti katika ngazi(level) ya chini kabisa, lakini hivi ndivyo hata matajiri wakubwa wanavyotengeneza pesa kwa kutumia asseti mbalimbali. Kinachowafanya matajiri kuzipenda sana asseti ni kwamba asseti zina tabia ya kujiongeza zenyewe kupitia ununuzi wa asseti nyingine kwa kutumia pesa zitokanazo na aaseti zilezile.

Kwa kutumia fedha kidogo ulizokuwa nazo kununulia asseti fulani inamaanisha kwamba unaongeza uwezekano wako wa kuja kuingiza pesa nyingi zaidi hapo siku za baadae. mfano mmoja hebu jaribu kufikiria kama mwaka jana mwanzoni ungelinunua mashine zako 2 za kutengeneza pop corn na kuamua kuwapatia vijana waweke stendi mbalimbali kisha kila jioni wakuletee kiasi fulani cha pesa ambacho usingekitumia zaidi ya kununulia mashine nyingine, leo hii ungelikuwa unamiliki mashine ngapi?

SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.

Lakini pia unaweza ukajiuliza hivi; “Ikiwa hivi ndivyo ilivyo na ni wazi kabisa kila mtu analijua hili kwamba asseti ndiyo kila kitu, kwanini basi watu ‘wastraggle’ hivyo na umasikini na kushindwa kutumia mkakati huu kutajirika? Sababu kubwa ni kwamba asseti zinahitaji mtu uwe na subira, unaponunua kifaa leo au hisa au kufungua biashara fulani, unawekeza pesa na ile pesa haiwezekani uirudishe ndani ya muda mfupi tena, itarudi kidogokidogo ila itafika mahali inarudi pesa yote na sasa unaanza kuingiza faida tu, na hapo ndipo sasa raha yenyewe ya kumiliki asseti ilipo.

Kitu kingine ni kwamba katika asseti mfano kuna biashara zingine mtu utahitaji kuwekeza katika maarifa ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti kwa muda mrefu kabla hujaona faida na siyo jambo la chapchap tu. Sasa unaweza kuona yakwamba ni rahisi zaidi mtu kuamua kutafuta kazi(ajira) kuliko kuhangaika na kuwekeza katika asseti mbalimbali. Hapo sijasema ajira ni mbaya hapana, kwani kila kimoja ajira na biashara ni muhimu ili dunia iweze kusonga mbele, huu ni mjadala mwingine mrefu tutautafutia siku nyingine.

SOMA: Biashara ndogondogo zenye faida ya haraka Tanzania ni hizi hapa, zipo nne(4)

Hapa sasa ndipo inapoingia ile Mikakati miwili (2) niliyoanza nayo kule mwanzo, mkakati wa sungura na mkakati wa Kobe…….

............................................................

Mpendwa msomaji wangu, ungependa kujua ni kitu gani kilichojiri baina ya hawa mabwana wawili Sungura na Kobe? Tafadhali ni kisa cha kusisimua, Usikose kuungana na mimi katika MASTREMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE mkasa huu mzima utakutana nao kule na mambo mengine mengi mazuri, unakaribishwa saana!

Unapolipia kiingilio chako cha shilingi elfu 10, unakuwa mwanachama, lakini pia nakutumia offa ya masomo, michanganuo, seminars na vitabu mbalimbali muda huohuo. OFFA hii ya vitu vingi utachagua mwenyewe usome nini kwa jinsi ilivyokuwa na wingi wa vitu. OFFA ni ya muda mfupi na inakaribia kuisha.

Pia utapata fursa ya kushiriki katika seminar zetu za kila mwezi juu ya michanganuo ya biashara za viwanda vidogovidogo bunifu. Mwezi huu tarehe 15 tutakuwa na semina ya kiwanda cha USAGISHAJI NAFAKA baada ya mwezi uliopita kuwa na ya KIWANDA CHA TOFALI ZA SARUJI. Semina hizi zinaamsha ari ya mtu kuanzisha kiwanda anachokitaka.

Kwa yule asiyependa kujiunga na magroup au wasiotumia WHATSAPP, email inatosha kwani tunatuma masomo na vitu vyote kwa email pia.

Namba za malipo ni 0765553030 au 0712202244 baada ya kulipia tuma ujumbe wasap au SMS ya kawaida ukisema; 

"NIUNGANISHE NA GROUP PAMOJA NA OFFA INAYOKARIBIA MWISHO"



0 Response to "MIKAKATI (2) YA PESA, WA SUNGURA NA WA KOBE: JE, WEWE UNATUMIA UPI KATI YA HIYO?"

Post a Comment