Unaweza kutajirika bila kuwa na chochote sawa na Dunia ilivyotokana na atom ndogo sana(From Zero to Hero) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

Unaweza kutajirika bila kuwa na chochote sawa na Dunia ilivyotokana na atom ndogo sana(From Zero to Hero)

MWANZO WA KUUMBWA KWA ULIMWENGU(THE BIG BANG)
Wanafizikia wanatueleza kwamba pamoja na Ulimwengu(The Universe)  kuwa ni dude kuubwa sana la kutisha lisilokuwa na mwisho katika upeo wa macho ya binadamu, hata utumie chombo chenye spidi kali namna gani huwezi kufika mwisho wake. Lakini ulimwengu  huohuo ambao dunia yetu ni sehemu yake ndogo tu, uliumbika kutokana na kachembechembe kadogo sana! ndogo kushinda hata mbegu ya haradali ambayo ndani yake ilikuwa imesheheni nguvu kubwa na uzito wa ajabu.

Yapata miaka takribani bilioni 14 sasa tokea tukio hili la  kuzaliwa kwa ulimwengu. The Big bang, mlipuko mkubwa ukiambatana na joto kali uliotokea wakati huo uliifanya “mbegu” hiyo ndogo sana kuliko atomu mara mamilioni kuanza kujitanua yenyewe kwa kasi na kuendelea kutanuka mpaka hivi leo tunaposhuhudia Ulimwengu mkubwa kabisa usiomithilika. Hebu fikiria ni kwa jinsi gani kitu kidogo namna hiyo ndani yake kinaweza kuwa na uwezo wa ajabu kama huo!

SOMA: Maisha sayari mpya yaja jiandae.

Hali hii ya kutokea kwa Ulimwengu inafanana sana na jinsi ambavyo mtu anaweza kutajirika bila kuanza na chochote akajakumiliki utajiri mkubwa wa kushangaza kama kina Bill Gates, Warren Buffet, Mo, Bakhresa na wengineo. Siyo hadithi ni ukweli kuna watu walioweza kuanzia sifuri kabisa mpaka wakafikia kuitwa mabilionea wakutupa chini ya jua! Watu wengi huuliza, nawezaje kuwa tajiri bila kuwa kwanza na chochote? Lakini siri za matajiri wengi duniani ndio hii tutakayoiona leo.

Tangazo muhimu!
Ndugu msomaji wangu makala hii ni moja ya makala zangu za pesa za kusisimua zaidi ndani ya Grouo la Michanganuo-online katika mwaka huu wa 2018, ni miongoni mwa makala 30 za kuufungia mwaka huu. Nyingine nilizoandika toka mwezi Januari pia ni kali na nimezicompile katika vitabu 3 ambavyo pamoja na semina na masomo mengine yote ya mwaka huu nakupa bure kama offa ya kuumaliza mwaka. Maelezo zaidi utayapata mwishoni chini ya makala hii.

Unaposikia mtu kutajirika pasipo kuanza na chochote kama mtaji wa pesa na rasilimali zingine inashangaza kidogo na inaweza isiingie akilini hata kidogo kutokana na sababu kubwa kwamba kupata tu pesa sembuse utajiri wenyewe imekuwa ni shughuli pevu hata kwa yule tayari aliye na mtaji.

SOMA: Stadi moja ya maisha itakayokuwezesha kuingiza pesa bila ya kuwekeza chochote.

Ungelitegemea kwamba  ikiwa mtu anaweza kutajirika bila kuanzana na kitu chochote, kwa yule anayeanza na mtaji kidogo basi ingelikuwa rahisi kwake mara mbili au tatu zaidi kutajirika. Lakini tunashuhudia idadi kubwa ya watu pamoja na kumiliki mitaji ya maana bado wanahangaika, ‘wanastruggle’ kupata utajiri wa maana. Ni siri gani basi hiyo nyuma ya pazia inayosababisha watu wachache kutajirika pasipo kuanza na chochote mkononi kama mtaji wa pesa au rasilimali nyingine zinazoshikika?

Ingawa njia hiyo ya kutajirika kwa kuanza na sifuri ipo wazi kabisa, inafanana sana na mchezo wa riadha ambao mshiriki unaona kabisa ushindi uleee! lakini shughuli inakuwa ni kwenye kuupata utajiri wenyewe. Anayeshinda utakuta ni lazima awe amebobea katika mazoea fulani na kwa mkimbia marathoni  siri ni mazoezi.

SOMA: Nitawekezaje kwenye ardhi na majengo wakati sina hata mia mfukoni?

Kwa upande wa utajiri siri siyo mazoezi  kuna tofauti kidoogo, na tofauti hiyo sasa ndiyo tunayotaka leo kwenda kuijua katika somo hili la 8 la kipekee kabisa kati ya masomo 30 ya Desemba inayoishiaishia. Kumbuka tuna masomo 22 mbele yetu  hivyo nakusihi sana usikose hata moja.

Binadamu wote tunazaliwa kutoka kwenye matumbo ya mama zetu tungali hatuna chochote, ukiachilia mbali wale wanaokuja kuridhi mali za wazazi wao asilimia kubwa ya watu inayobakia ni lazima wapigane wao wenyewe kufa na kupona ikiwa watataka kutajirika. Cha ajabu kinachokuja kujitokeza ni kwamba kati ya hao hao wengi ambao hawana bahati ya kuridhi mali au kushinda bahati na sibu wapo tena wachache kati yao wanaokuja kuibuka kuwa matajiri na wengi wakiendelea kusota katika lindi la umasikini. Idadi hiyo ndogo ya watu wanatajirikatajirikaje?

Jibu rahisi sana unaloweza kupewa na mshauri au mtaalamu wa biashara na ujasiriamali ni kuwa tofauti hiyo hutokana na jinsi watu tunavyozitumia rasilimali tulizokuwa nazo. Tajiri na masikini ni matokeo ya namna walivyotumia rasilimali/pesa walizokuwa wakizipata siku zilizopita.

SOMA: Kwanini kufanikiwa kifedha si dhambi na kila mtu anastahili afanikiwe?

Ingawa ukweli huu nao unaweza kuwa na mashiko kwa kiasi fulani lakini bado yanabaki mashaka kwamba kama suala ni matumizi ya rasilimali, vipi kuhusiana na wale ambao walipoanza hawakuwa na rasilimali yeyote zaidi ya kuwa wao wenyewe? Ni kwa jinsi gani waliweza kuzalisha pesa pasipokuwa na kitu? Ni maajabu sawa na yale ya Ulimwengu kuumbika kutokana na atomu ndogo kabisa hadi dude lisilokuwa na mwisho.


JINSI UNAVYOWEZA KUTENGENEZA UTAJIRI MKUBWA HATA KAMA HAUNA KABISA KIANZIO CHA HELA AU RASILIMALI ZOZOTE.

Kupata pesa achilia mbali kutajirika ni jambo gumu linalohitaji mtu kufanya kazi kwa juhudi zote na maarifa. Na ni ukweli usiopingika kuwa hamna njia ya mkato. Lakini pia haipingiki kuwa pamoja na ugumu uliopo kutajirika kwa kuanza na sifuri kupo na inawezekana tu endapo mtu atakuwa tayari kufuata mchakato maalumu wa kumfikisha kwenye utajiri. Ishu hapa leo siyo kutajirika tu bali ni kutajirika kunakoanzia na hali ya kutokuwa na kitu chochote kama fedha na rasilimali nyingine.

UNAVYOWEZA KUANZA

Linapokuja suala la pesa au rasilimali za kuwekeza ili mtu uweze kutengeneza pesa na utajiri mkubwa, karibu kila mtu utamsikia akilalamikia moja kati ya mambo yafuatayo;

·       Nimezaliwa katika familia masikini sana
·       Kabila letu hatuna mwamko wa pesa
·       Kipato kidogo ninachokipata hakitoshi kuanzisha mradi wala kuwekeza kwenye kitu chochote.
·       Familia haina amani, mke/mume/wanafamilia hawanisapoti
·       Eneo ninaloishi hamna fursa za kuingiza pesa
·       Sina muda wa kutosha wa kutafuta kipato zaidi.

Lakini ukweli ni kwamba, visingizio vyote hivyo na vingine ambavyo mtu yeyote anaweza akasingizia havina msingi wowote isipokuwa tu watu huvitumia kama uhalali  wa kutokutimiza malengo yao. Kwa kuwa hatma ya maisha ya mtu ipo mikononi mwake mwenyewe na uamuzi anao yeye, hakuna mtu yeyote wala serikali inayoweza kumpeleka jela kwa sababu ametoa visingizio vya uwongo juu ya kushindwa kwake kupata pesa.......................


.........................Baada ya vitu hivyo sasa ndio vitafuata vitu vingine ambavyo tumesema huja vyenyewe, kwa mfano suala la kubana matumizi na kujiwekea akiba litakuja lenyewe tu moja kwa moja automatic baada ya kumaliza vitu hivyo muhimu. Mtindo huu ndio karibu kila anayetajirika kwa kupitia juhudi zake mwenyewe huutumia, watu kama vile kina Bill Gates, Reginald Mengi, Said Salim bakhresa, Mark Zuckerberg, Steve Jobs na wengineo wengi walikaa..............................somo hili linaendelea.........................


…………………………………………………


Mpenzi msomaji wa blogu hii karibu sana ujiunge na mfululizo wa masomo haya ndani ya group la MICHANGANUO-ONLINE, si lazima uwe na Wasap, email inatosha kwani tunatuma kila kitu pia kupitia email kama hutumii wasap.  Mwisho wa masomo ya mwaka huu wa 2018 ni Desemba 30 ambapo tutaanza Programu nyingine mpya. Kwa mwaka mzima programu yetu tulikuwa tukijifunza masomo yenye maudhui ya fedha pamoja na Jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara bunifu hatua kwa hatua. Masomo hayo yote yamehifadhiwa katika mfumo wa vitabu(softcopy) na kila anayejiunga tunamtumia masomo yote tangu tuanze  mwezi Januari mpaka sasa.

Tuna masomo spesho 30 yanayoendelea ndani ya mwezi huu wa 12 nayo mwishoni yatatiwa katika kitabu chake maalunu. Ni masomo maalumu ya kufungia mwaka huu ambayo huwezi kuyapata mahali pengine popote pale. Kupata vitu vyote hivi vya mwaka mzima na hiyo “30 spesho” unapaswa kulipia sh. Elfu 10 tu, na hii ni offa ya muda mfupi sana. Baada ya tarehe 30 Desemba 2018, ada ya kujiunga na Group itapanda na kuwa sh. elfu 20 bila offa ya masomo yeyote yaliyopita.

Kwanini ukose kitu cha thamani kwa gharama hiyo ndogo namna hii? Naamini mimi sitakujakulaumiwa kwamba sikukujulisha mapema.

Ili kujiunga lipa kiingilio sh. Elfu 10 kisha tuma ujumbe kwa simu au wasap usemao, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”

Simu: 0712202244
Wasap: 0765553030

Jina: Peter Augustino Tarimo.   



0 Response to "Unaweza kutajirika bila kuwa na chochote sawa na Dunia ilivyotokana na atom ndogo sana(From Zero to Hero)"

Post a Comment