UMEKATA TAMAA YA MAISHA? HEBU SOMA MAAJABU YA MWANASAYANSI HUYU MKUBWA DUNIANI. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UMEKATA TAMAA YA MAISHA? HEBU SOMA MAAJABU YA MWANASAYANSI HUYU MKUBWA DUNIANI.


Mwanasayansi mkubwa duniani Stephen Hawking wa Uingereza aliyefariki jana, kifo chake kimetokea miaka 55 baada ya madaktari kumwambia kwamba alikuwa na miaka 2 na nusu tu ya kuishi kutokana na kugundulika kuwa na ugojwa wa mishipa ya fahamu kupungua uwezo wa kusapoti misuli. Ugonjwa huu unawapata watu kwa nadra sana na unajulikana kitaalamu kama, amyotrophic lateral sclerosis (ALS)


Akiwa na umri wa miaka 21 tu, huku ukiwa ni mwaka wake wa kwanza akisomea PHD katika chuo kikuu cha Cambridge ndipo alipolazwa hospitalini kwa uchunguzi wa ugojwa huo, kwa hakika zilikuwa ni habari za kushitua sana kwake na kwa familia yake. Hata hivyo kuna vitu kadhaa vilivyomfanya asikate tamaa moja kwa moja licha ya habari hiyo ya kuogofya.

Kitu cha kwanza kabisa kilichomfanya awe na matumaini ni pale pale akiwa amelazwa hospitalini, kulikuwa na kijana mwingine aliyekuwa amelazwa naye chumba kimoja kwa tatizo tofauti la ugojwa wa leukemia. Akilinganisha ukubwa wa tatizo la kijana yule mwezie alilokuwa akikabiliana nalo na la kwake, Stephen Hawking baadae aliliona tatizo lake kuwa na nafuu zaidi na linaloweza kuvumilika zaidi ya hilo la mwenzake la leukemia. Leukemia ni ugojwa wa kansa ya damu ambao mgojwa hawezi kudumu nao kwa muda mrefu.


Muda mfupi baada ya Stephen kuruhusiwa kutoka hospitali, aliwaza kichwani na kujifananisha na mtu aliyekuwa akisubiri hukumu ya kifo, lakini mawazo yake hayo yalimfanya kutambua kwamba bado kulikuwa nafasi japo kidogo katika maisha yake yaliyosalia ya kufanya mambo ya maana hata ikiwa I machache kiasi gani. Huku akitambua wazi kwamba amesaliwa tu na miaka michache ya kuishi pengine masikini hata kutokutosha mpaka asheherekee PHD yake, aliamua kusoma kufa na kupona angalao atomize ndoto yake aliyoota akiwa pale hospitalini ya kufanya vyema mambo machache yaliyobakia katika muda mfupi wa kuishi hapa duniani.

Ugonjwa ulimbadililisha kuwa mwanasayansi mkubwa kama yeye mwenyewe alivyowahi kusimulia hivi,
“Kabla sijagundulika na ugonjwa huu, sikuwa kabisa na malengo na masomo, nilikuwa nimechoshwa sana na maisha, sikuwa naona chcochcote kile cha maana cha kufanya, lakini pindi tu baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa na nisingeliweza kuishi hadi nimalize chuo nikaanza kuzingatia masomo”-Stephen Hawking  

Sababu hii ndiyo iliyokuja kumfanya Hawking kuwa mwanasayanzi mashuhuri kiasi hiki. Alijitupa katika tafiti na kazi mbalimbali mbali za kisayansi hususani kuhusiana na anga za mbali na kwa kadiri mafanikioa yake katika tasnia hiyo yalivyozidi kuwa makubwa ndivyo na afya yake ya kimwili nayo ilivyozidi kuzorota. Lakini jambo la ajabu katika ugonjwa huu ni kwamba akili hubakia kama ilivyo, huwa haiathiriwi kabisa na ugonjwa huu wa (ALS).

Ilifikia kipindi akawa kila kitu kimwili ni lazima asaidiwe huku akitumia kiti cha magurudumu mawili. Sauti nayo ikakatika kabisa lakini kwa msaada wa wataalamu wa kompyuta kutoka Marekani wakaweza kumtengenezea program(speech synthesizerinayoweza kutafsiri hisia za mtu na kutamka maneno anayotaka kusema ambayo ilikuja kumsaidia hata alipokuwa akitoa mihadhara mbalimbali katika vyuo vikuu duniani mpaka anakufa. 





Akitumia programu hiyo na msaidizi aliweza kuandika ripoti mbalimbali za kisayansi na zisizokuwa za kisayansi, vitabu na hata amewahi pia kujihusisha katika filamu na vipindi vya televisheni hadi mauti inamfika jana.

Mtu huyu ni ushahidi wa wazi kwetu sisi wajasiriamali kwamba akili ya binadamu inao uwezo wa ajabu wa kutenda mambo bila hata ya kutegemea mwili wake(Think & Grow Rich). Aliweza kufanya mambo makubwa yanayolingana na mambo waliyowahi kufanya kina Albert Einstain, Sir Izak Newton, Galileo Galilei na wengineo huku mwili na viungo vyake vikiwa havifanyi kazi yeyote isipokuwa akili yake pekee. Hayo ndiyo maajabu ya UBONGO wa binadamu.

Akifungua mashindano ya paralympic mwaka 2012 huko London baada ya kukaribishwa na watu kumshangilia mno kwa makofi alitamka maneno yafuatayo;

 “Sisi sote tuko tofauti, hakuna kitu kama binadamu wanaofanana au wa aina moja, lakini tunachangia wote kuwa na roho. Kitu muhimu ni kwamba tuna uwezo wa kubuni. Ubunifu huu unaweza kuchukua sura nyingi, kuanzia mafanikio yanayoshikika mpaka fizikia ya nadharia. Hata maisha yawe magumu kiasi gani, mara zote kuna kitu mtu unachoweza kufanikisha.” ”-Stephen Hawking  

0 Response to "UMEKATA TAMAA YA MAISHA? HEBU SOMA MAAJABU YA MWANASAYANSI HUYU MKUBWA DUNIANI."

Post a Comment