JINSI MPANGO WA BIASHARA UNAVYOWEZA KUONGEZA MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI MPANGO WA BIASHARA UNAVYOWEZA KUONGEZA MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO


Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusiana na ikiwa mpango wa biashara unaweza kusaidia katika mafanikio ya biashara au la, watu wengi kwa muda mrefu wamekuwa na dhana kwamba mchanganuo au mpango wa biashara ni kwa ajili ya kuombea pesa (mkopo) tu na baada ya hapo basi ni kuuweka kabatini uendelee kuliwa na wadudu.

Zipo sababu nyingi zinazoweza kuwafanya wajasiriamali wengi kutokuandika mpango wa biashara lakini iliyokuwa kubwa zaidi ni hii ya kufikiri kwamba, kuandika mpango wa biashara ni jukumu zito linalohitaji muda mwingi na utaalamu katika tasnia ya biashara na fedha. Lakini kumbe ni kinyume chake kabisa.

SOMA: SABA(5) KWANII UANDIKE MPANGO WA BIASHARA YAKO

Kwanza mpango wa biashara siyo kwa ajili ya kuombea fedha tu peke yake, isitoshe siyo kweli kwamba kuandika mpango wa biashara mtu anatakiwa kuwa amesomea masomo ya biashara ndipo aweze kuandika.

Kama unao uwezo wa kufikiria wazo la biashara, ukatafuta mtaji wa kuanzisha biashara yenyewe pamoja na kuiendesha, basi wewe tayari unao uwezo wa kuandika au kuandaa mpango wa biashara yako kuliko hata mtu mwenye digirii ya biashara. Kila siku, kila mahali duniani na karibu kila binadamu katika wakati fulani wa maisha yake ni lazima aandae mpango/mchanganuo wa biashara, penda asipende. Haiwezekani kabisa mtu ufanye biashara yeyote ile hata kama ni ya kuuza karanga mitaani pasipo kwanza kufanya mchanganuo wa biashara hiyo akilini kwake.

SOMA: Kwanini mpango wa biashara wa kuandikiwa siyo mzuri kwako?

Kitendo tu cha kujua utapata faida kiasi gani kwenye kilo moja ya karanga utakazokaanga, tayari hiyo ni hatua mojawapo ya mchanganuo wa biashara hiyo ya kuuza karanga. Sasa iweje useme huwezi kutengeneza mpango wa biashara? Siku hizi mambo yamerahisishwa mno siyo kama zamani, Mpango wa biashara wa kukuwezesha kuendesha biashara yako kwa ufanisi mkubwa siyo lazima tena uandike kurasa 20 au 50 kama unapeleka benki kuomba pesa. Lakini pia unaweza kuandika haikatazwi na ni faida zaidi ikiwa unaweza kufanya hivyo.

Pointi yangu hapa ni kwamba, ikiwa unaona uvivu kuandika mchanganuo wa biashara wenye kila kitu kama michanganuo iliyokuwepo katika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, basi zipo njia fupi zinazoweza kukufanya ufurahie kufanya mchanganuo wa biashara yako pasipo kutumia muda mwingi wala utaalamu mkubwa sana.

Njia mojawapo mimi binafsi ninayoikubali sana, ni ya kujifunza namna ya kufanya michanganuo ya biashara kupitia usomaji wa michanganuo kama ile tunayotoa OFFA katika group la Michanganuo. Ukishajua mbinu zinazotumika wakati wa kuandaa mpango wa biashara, hiyo ni nusu ya kuandika mpango wenyewe wa biashara kwani sasa unaweza tu kufanya biashara yako kwa kutegemea mpango unaouweka kichwani(akilini) mithili ya matajiri wa zamani ambao hawakuwa wamesoma hata darasa moja lakini ulikuwa huwezi kuwaeleza kitu chochote kwenye usimamizi na uendeshaji wa biashara zao.

Watu hawa ‘walimaster’ mbinu za kuendesha biashara zao kutokana na uzoefu tu walioupata na uwezo wao wa kufanya ufuatiliaji wa kila kitu wanachojipangia au kumpangia mtu kufanya katika kutimiza malengo yao ya biashara.

SOMA: Je, huna muda wa kutosha wa kuandika mpango wa biashara yako?

Njia nyingine maarufu sana siku hizi ni kutengeneza kitu kinachoitwa Mpango wa biashara Ukurasa mmoja (Ope Page Business Plan). Hii ni aina ya mpango wa biashara ambao haihitaji muda mwingi kuandaa lakini vipengele vyote muhimu vya biashara hujumuishwa ndani. Mfano na Template ya namna ya kuandika mpango huo upo kwenye kitabu (E-book) ambayo ni miongoni mwa vitabu vilivyoko kwenye Offa yetu ya semina ya mwaka huu 2022

Sasa basi ni kwa jinsi gani unavyoweza ukatumia mchanganuo au mpango wako wa biashara kuiendesha biashara yako ikakuletea mafanikio?

Hakuna mtu asiyefahamu kuwa kwenye biashara yale tunayoyapanga hayawezi kuja kuwa sawasawa na matokeo yenyewe wakati wa kufanya biashara yenyewe halisi. Mambo mara nyingi huja kwenda tofauti. Lakini hauwezi ukasema kuwa mpango wa biashara hauna maana kwa sababu hata ikiwa hujafanya mpango rasmi wa biashara kama nilivyotangulia kusema hapo juu ni lazima tu ulipanga kichwani, hilo halina ubishi, ukisema hukupanga basi wewe siyo binadamu ni roboti.

Ingawa tunapanga lakini vilevile tunahitaji kujiandaa na mabadiliko yatakayojitokeza kwa kasi katika hali halisi mbele ya safari. Na hivyo ndivyo binadamu tunavyofanya kila mara tunapopanga kufanya jambo lolote lile katika maisha yetu ya kila siku. Sasa kwa faida zaidi ya kupanga ndipo utakuta watu wakipanga “simple” na katika kutafuta urahisi huo ndiyo maana mimi huwa nashauri kila  wakati mtu ujue …ABCD…. kuhusiana na mipango ya biashara na kisha kwenye kuandika uandike mpango 'simple' utakaokusaidia katika kusimamia biashara yako kwa uhakika na kisasa, pasipo hata kuandika mamia ya kurasa.

Kuna vitu kwa mfano kama;
·       Malengo ya biashara, maono
·       Mikakati
·       Vitendo halisi
·       Vipimo katika utekelezaji
·       Hesabu na namba za msingi kama vile mauzo, bajeti ya gharama mbalimbali na mahitaji.

Ukishaandika vitu hivyo kwa ufupi sasa unatakiwa wakati wa utekelezaji wa biashara ufanye mapitio mara kwa mara, unaweza ukaamua kujipangia ratiba ufanye mapitio ya mpango wako vs hali halisi katika kipindi fulani, kwa mfano unaweza kufanya kila siku, kwa wiki au kwa mwezi. Unaangalia tofauti iliyokuwepo kati ya mpango na matokeo halisi. Hapa huhitaji kuwa mtaalamu wa biashara bali unatumia akili ya kawaida tu ya kuifahamu vizuri biashara yako na kufuatilia kujua ni kitu gani kilichotokea ukilinganisha na kile ulichopanga.

SOMA: Utambulisho rasmi wa semina ya michanganuo ya biashara awamu ya kwanza 1

Katika ulinganisho huo ni lazima utagundua kwamba, mpango wa biashara mara nyingi hauwezi kwenda sawasawa kwa asilimia 100% kama ulivyopanga. Lakini kuna umuhimu mkubwa na faida kiutendaji kwani kunakuwezesha kufahamu ni kwa nini hali haikwenda sawa na ulivyopanga. Kumbuka hali halisi siyo mara zote huwa tofauti kwa maana ya mambo kwenda mrama hapana, kuna wakati mwingine hata pengine katika mpango ulikisia mauzo kuwa Sh. 1,000,000/= lakini katika hali halisi unashangaa mauzo yanakuja kuwa 1,300,000/=. Kwa hiyo zoezi hili litakusaidia kuamua ufanye mabadiliko gani, na utegemee matokeo gani kwa wakati ujao.

Zoezi hili la kufanya marekebisho ya mpango pamoja na kulinganisha mpango na matokeo halisi ni jambo muhimu sana na katika hali ya kawaida kabisa ni zoezi linalofanyika katika maeneo mengi ya kazi na biashara. Kwa mfano unapoingia katika nyumba nyingi za habari (News rooms) iwe ni katika magazeti, redio au Televisheni, utakuta kila siku wana mikutano, wengine huiita “postmortem” Mhariri mkuu hukaa na wafanyakazi wote na kuanza kufuatilia kile walichofanya jana yake ikiwa walifikia malengo waliyojiwekea jana kwa kiwango gani. Kisha siku hiyo mhariri huandaa mpango mwingine wa siku, nani aende wapi, akafanye nini, na kwa gharama gani nk.

Ingawa utakuta kuna vitu havikuenda sawa kama mpango ulivyosema, lakini hapa kumbuka mhariri hamtafuti mchawi wala kumlaumu mtu, bali yeye anachotafuta ni kwa nini mambo hayakwenda sawa au kwanini yalikwenda vizuri zaidi kushinda ilivyokisiwa, kusudi mbinu hizo ziweze kutumiwa zaidi wakati ujao.

Kwa hiyo matokeo ya mchakato wa kupanga au mpango mzuri wa biashara siyo maandishi bali ni utekelezaji wake(execution), jinsi unavyopanga vipaumbele vya biashara yako na kufuatilia utekelezaji wake kujua ni kipi kimeenda sawa au ni kipi kimeenda mrama kwa ajili ya kufanya marekebisho kwa ajili ya wakati ujao.

Kusimamia biashara ni sawa na mtu unavyoendesha gari, unatakiwa uelewe ni uelekeo upi unaokwenda na uwe na maono ya kule uendako, picha ya hatma ya safari yako. Ukichanganya vitu hivyo na marekebisho ya hapa na pale njiani kama vile kuruka matuta, kukwepa vitu barabarani nk. hata kama ikiwa ni barabara kubwa kama Morogoro road, hakukosekani matuta na vizuizi vya hapa na pale. Lakini muda wote unatakiwa kushikilia usukani wako pasipo kutetereka kwa kuwa tayari unao mpango na maono kichwani ni wapi unakokwenda.

………………………………………………………………….

Ndugu msomaji, ikiwa wewe unahitaji kujifunza kwa kina jinsi ya kuandika mpango wa biashara yeyote ile pamoja na kupata  ‘materials’ zote zinazohusiana na michanganuo ya biashara kama vile vitabu kwa kiswahili na kiingereza, Templates za kiswahili na kiingereza na Sample za Michanganuo kamili ya biashara mbalimbali, basi hapa ndiyo mahali pake.

Tunayo Semina inayoendelea sasa kwenye Group la Michanganuo-online kila siku usiku yenye masomo 11 na leo ni siku ya pili. Ada ni Tsh. 10,000/= na ukiwahi kujiunga kabla ya tarehe 10/4/2022 unapewa papo hapo Offa ya Vitabu, michanganuo na templates jumla ni vitu 20 kama ilivyoonyeshwa hapo chini;

Namba zetu ni: 0765553030  au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo. Baada ya kulipia tuma ujumbe usemao, "NATAKA SEMINA NA OFFA YA VITU 20"


OFFA YA VITU 20 ITAKAYOISHA RASMI TAREHE 10/04/2022

 

                      1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

                      2.      KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili

 

                      3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

                      4.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

                      5.      KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza

 

                      6.      Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili

 

                      7.      Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili

 

                      8.      Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili

 

                      9.      Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili

 

                    10.    Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza

 

                    11.    Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili

 

                    12.    Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili

 

                    13.    Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

                    14.    Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili

 

                    15.    Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza

 

                    16.    Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

                    17.    Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

                    18.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili

 

                    19.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza

 

                    20.    Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili

 

                    21.    Kunganishwa group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima

 

                

2 Responses to "JINSI MPANGO WA BIASHARA UNAVYOWEZA KUONGEZA MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO"

  1. Habari! Nahitaji kuandika andiko la ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa na ujenzi wa madarasa matatu ya wanafunzi wenye mahitaji Maalum. Naweza kusaidiwa juu ya hilo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inawezekaka kabisa, tuwasiliane namba zangu ni 0765553030

      Delete