NGUVU YA USHIRIKA, UMOJA NI NGUVU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NGUVU YA USHIRIKA, UMOJA NI NGUVU

nguvu ya ushirika, umoja ni nguvu

Ni hali inayojitokea popote pale palipo na mapambano ya aina yeyote. Wapigania uhuru wote duniani walikutana na hali kama hiyo, na hata mimi na wewe leo tunaopambana na hali mbalimbali za kimaisha ni lazima tukubali ukweli huu kwamba mapambano yeyote huanza na mtu mmojammoja lakini hakuna ushindi mpaka pale watu hao mmojammoja watakapoamua kukaa na kuunda umoja (Master Mind Group).

SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.

Vita ya kutafuta uhuru hawakuanza Mwalimu Nyerere, Jomo Kenyetta, Obote, Mugabe, Lumumba na wengineo, hapana, kabla yao yalikuwepo mapambano kama hayo mengi mfano wa akina Kinjekitile na Majimaji, Maumau, nk. Lakini kwanini hawakuweza kuwashinda Wakoloni? Sababu kubwa ilikuwa ni kukosa Umoja! Hawakuwa na kundi la kushauriana(mastermind group) la uhakika.

Umeona katika Sura ya 8 ya ya kitabu cha Think & Grow Rich(Fikiri Utajirike) umuhimu wa kuwa na umoja(kundi) pamoja na kufanya maamuzi thabiti. Mapambano ya Uhuru wa Marekani yalianza muda mrefu watu wakipambana mmojammoja  lakini nguvu ya maana ilikuja kujitokeza baada ya “Mababa wa Taifa hilo kuja kugundua kuwa, kumbe bila ya umoja, ushirikiano, hakuna Ushindi wowote ule wa kweli.

SOMA: Muda biashara itakaorudisha faida.

John Hancock, Samuel Adams na Richard Henry Lee walianzisha wazo la mawasiliano ya pamoja kati ya makoloni yote 13 ambalo hatimaye lilikuja kuzaa uhuru tunaoushuhudia leo hii Marekani. Kabla ya hapo hakukuwa na watu walioweka mioyo yao, akili, roho na mwili pamoja katika uamuzi mmoja kusuluhisha matatizo yao.

Leo nimeandika haya kwa lengo la kuonyesha umuhimu wa kufanya kazi kama kundi. Wakati mwezi huu ukianza tulitangaza kuanzisha semina maalumu za michanganuo ya biashara zenye ubunifu wa kipekee kwa njia ya Whatsapp, pamoja na zoezi hili kuchelewa kidogo hata hivyo leo tarehe 19 tumeianza rasmi na tayari kundi la whatsapp limeshaundwa. Katika kundi hilo tutajadili mada mbalimbali zinazohusiana na;

·       Michanganuo ya biashara 12 zenye fursa za kipekee.
·       Jinsi ya kuongeza mzunguko wa fedha katika biashara zetu.
·       Jinsi ya kuandaa mipango ya biashara kwa kina.
·       Mada yeyote ile inayohusiana na Ujasiriamali, biashara na maendeleo binafsi itakayoibuliwa na mwanachama.
Unapojiunga na kundi hili unapata vitu vifuatavyo bila malipo ya ziada.;

·       Kitabu cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali katika lugha ya Kiswahili(softcopy)
·       Kitabu mashuhuri zaidi cha jinsi ya kuandika mpango wa biashara katika lugha ya kiingereza.
·       Templates(Vielezo) za mpango wa biashara za Kiswahili na za kiingereza zitakazokuwezesha kuandika mpango wa biashara yako kwa muda mfupi.
·       Kuunganishwa na Blogu maalumu ya michanganuo ya private bure.

SOMA: Jinsi ya kujiunga na Darasa la michanganuo online.

Kundi la Whatsapp ni njia rahisi na nzuri zaidi ya kuwasiliana kwa haraka na ambayo kila mwanachama anapata fursa ya kutoa mchango wake kwa wanakundi wenzake wote tofauti na njia

zingine kama email ambazo ni ‘admin’  peke yake mwenye fursa hiyo.

Ili kujiunga na kundi la MICHANGANUO ONLINE, tuma ujumbe kwenye Whatsapp kupitia namba 0765553030 unaosema; “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”. Nitakuunganisha kwanza na kundi la MAPOKEZI, kisha baada ya malipo ya kiingilio ambacho ni sh. Elfu 10, unaunganishwa moja kwa moja na kundi la Michanganuo online pamoja na kupata vitu vingine vyote vilivyoorodheshwa hapo juu.

SOMA: Utambulisho rasmi wa semina ya Michanganuo ya biashara.


Karibu njoo tushirikiane kwa karibu zaidi, haijalishi uelewa wako wa michanganuo ya biashara ni kiasi gani, tunawakaribisha kila mtu, uwe hujui kabisa maana ya mpango wa biashara na hata ikiwa ni mtaalamu uliyebobea ndio tunakuhitaji haswa, kwani lengo letu ni kila mmoja ajifunze kutoka kwa mwenzake na hii ndiyo sababu kubwa ya kuanzisha kundi la Wassap ili kila mmoja aweze kutoa mchango wake.

0 Response to "NGUVU YA USHIRIKA, UMOJA NI NGUVU"

Post a Comment