SEMINA NA MAFUNZO: JINSI YA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA KIVITENDO YAANZA TENA WIKI HII KWA KISHINDO! | Jifunzeujasiriamali

SEMINA NA MAFUNZO: JINSI YA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA KIVITENDO YAANZA TENA WIKI HII KWA KISHINDO!

 

Peter Augustino Tarimo (Mtaalamu wa Michanganuo ya biashara)

Ndani ya Programu yetu ya MAKE YOUR SELF GREAT AGAIN wiki iliyomalizika jana tulikuwa na zoezi zito la kuanzisha Usomaji wa kitabu Maarufu cha Think & Grow Rich.

Namshukuru Mungu zoezi limeenda vizuri na mpaka kufikia leo hii tumeshamaliza kusoma sura ya pili japo tunakwenda kwa mwendo wa kinyonga kidogo kwa lengo hasa la kutokuwaacha nyuma wenzetu wenye kasi ndogo ya usomaji.

Programu yetu tulisema itakuwa na vitu vingi ndani yake lakini kubwa zaidi ikiwa ni Mafunzo ya kina juu ya uandaaji wa Michanganuo ya biashara (Business planning).

Kwanini business planning? Ni kwa sababu mpango wa biashara ni kila kitu, ndani yake utakutana na vipengele vingine vyote vinavyounda biashara mfano masoko, mauzo, usimamizi, uongozi, fedha na kila kitu kingine kinachofanya biashara iitwe biashara.Tunaua ndege wote kwa jiwe moja!

Hivyo kuanzia Jumatatu ya tarehe 4/7/2025 tutaendelea na zoezi la mafunzo ya uandishi wa Michanganuo ya biashara hatua kwa hatua kwa vitendo na sasa badala ya kuwa na mchanganuo wa biashara moja tu wa kufundishia tutakuwa nayo mitatu (3). Hii inamaanisha kwamba tutakuwa na madarasa matatu tofauti yakiendelea kwa wakati mmoja

Unapojiunga sasa unakuwa na fursa ya kuchagua ni mchanganuo wa biashara ipi  utapenda  kujifunzia, tunayo michanganuo ya biashara za aina nyingi ikiwemo michanganuo ya kuku, mgahawa, saloon, utengenezaji wa sabuni, duka la rejareja, kilimo cha tikiti maji, uokaji wa keki na vitafunwa, biashara ya genge, ufyatuaji tofali za saruji na mingine mingi

Mafunzo haya ya semina yataendeshwa kwa mfumo wa maandishi/text watsap, voice notes, videos na PDF 

Mwisho wa kujiunga na madarasa kwa wiki hii ni Alhamisi, watakaojiunga Jumanne, Jumatano na Alhamisi watajifunza mafunzo yaliyotangulia kwa muda maalumu ili waweze kulingana na wenzao waliowahi. Kujiunga zaidi ya Alhamisi itabidi mtu asubiri madarasa ya wiki zinazofuata.

JINSI YA KUJIUNGA NA KIINGILIO

Ada ya mwaka ni Tsh. 20,000/= lakini ukiwahi kabla ya offa kuisha unalipia Tsh. 10,000/= tu



HUDUMA ZETU NYINGINE MBALIMBALI ZA MALIPO 

(VITABU & MICHANGANUO YA BIASHARA)

 

1. Kuandikiwa Mchanganuo wa Biashara yako

Tunaandika Mpango kamili wa biashara yeyote ile kwa Kampuni na wafanyabiashara binafsi kwa gharama rafiki, njoo tuzungumze kupitia namba za simu au wasap 0765553030 / 0761002125 Michanganuo yetu tunaandaa kulingana na maono ya mteja kama yalivyo pamoja na mazingira ya soko linalomzunguka

2. Kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA

Kitabu hiki kilichowasaidia wajasiriamali wengi wadogo na wale wa kati kinatatua changamoto mbalimballi za biashara za rejareja kubwa ikiwa ni usimamizi wa mapato yasipotee au kudokolewa kiholela na wasaidizi wako, ni uzoefu wa zaidi ya miaka 12 wa mwandishi mwenyewe kwenye hii biashara.

Kukipata unaweza  ukatembelea duka letu la mtandaoni kukinunua hapo kwa kiungo hiki>>MAFANIKIO YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA

 

3. Kitabu cha THINK & GROW RICH –SWAHILI EDITION (FIKIRI & UTAJIRIKE)

Kitabu hiki kilichosomwa duniani na zaidi ya watu milioni 100 tunayo nakala ya Kiswahili kwa bei zifuatazo;

Ukiwa popote pale Duniani unaweza kukipata kwenye mtandao wa GETVALUE kupitia kiungo hicho kibofye kuingia ununue sasa hivi na kukidownload.

4. Vitabu zaidi &Michanganuo mbalimbali ya biashara

Kwa vitabu zaidi na Michanganuo mbalimbali ya biashara iliyo tayari tembelea duka letu hili  la mtandaoni uweze kuona na kujinunulia kwa urahisi kabisa>>SELF HELP TANZANIA ONLINE BOOSHOP



0 Response to "SEMINA NA MAFUNZO: JINSI YA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA KIVITENDO YAANZA TENA WIKI HII KWA KISHINDO!"

Post a Comment