“Unajua
matatizo ya wale wanaokabiliwa na uhitaji wa kuanza tena upya [To become great again].
Kuna mamilioni ya watu Duniani leo hii ambao wangependa kujua jinsi wanavyoweza
kubadilisha mawazo yao kuwa pesa, watu ambao ni lazima waanze tokea mwanzo,
pasipokuwa na pesa, na kurudisha hasara walizopata. Ikiwa mtu yeyote anaweza
kuwasaidia, wewe [Napoleon
Hill] unaweza.”
..................................
Edwin C. Barnes alifanikiwa kwasababu alichagua lengo dhahiri, na akaelekezea kwalo
nguvu zake zote, matumaini yake yote pamoja na jitihada zake zote katika
kulitimiza lengo hilo.
Alishinda
lengo lake kwasababu alitaka kuwa mbia kibiashara na Bwana Edison zaidi
kushinda alivyotaka kitu kingine chochote kile
Hakujiachia
kabisa uwezekanao wa kurudi nyuma. Ilikuwa ni lazima aidha ashinde au afe!
..................................
Mnaiona meli ikiteketea kwenye moshi, hiyo ina
maana kwamba hatuwezi tukaondoka ufukwe huu tukiwa hai ikiwa kama hatutashinda
vita! Sasa hatuna chaguo-ni lazima tushinde, vinginevyo tuangamie!
Kila mtu anayeshinda kwenye jambo lolote lile gumu,
ni lazima kwanza akubali kuchoma meli yake na kukata vyanzo vyote vinavyoweza
kumfanya arudi nyuma.
..................................
Ni wale tu wenye utambuzi wa pesa wanaoweza kutajirika.
Utambuzi wa pesa maana yake ni kwamba akili imejawa
mno na hamu ya pesa kiasi kwamba mtu anaweza kujihisi mwenyewe kuwa tayari
anazimiliki.
..................................
Ikiwa kama hautaweza kuuona utajiri mkubwa katika
fikra zako, basi kamwe hautaweza kuuona katika balansi yako ya benki
..................................
Dunia hii inayobadilika, ambamo tunaishi ndani
yake, inahitaji mawazo mapya, njia mpya za kutenda mambo, viongozi wapya,
ugunduzi mpya, njia mpya za kufundisha, njia mpya za kutafuta masoko, vitabu
vipya, fasihi mpya, vifaa vipya vya redio, vifaa vipya kwa ajili ya video.
Nyuma ya mahitaji hayo kwa vitu vipya na vizuri
zaidi kuna sifa moja ambayo mtu ni lazima kwanza awe nayo kusudi aweze
kushinda, nayo ni, ukamilifu wa lengo,
elimu ya ni nini mtu anachokitaka, pamoja na shauku kuu ya kukimiliki.
..................................
Ikiwa kitu unachotaka kufanya ni sahihi, na
unakiamini, endelea kufanya! Iweke ndoto yako mbele, na kamwe usijali kile watu
“wanachokisema”
..................................
KILA ANGUKO
HUJA LIKIWA LIMEBEBA MBEGU YA MAFANIKIO YENYE UKUBWA SAWA NA ANGUKO LENYEWE
..................................
Thomas Edison aliota ndoto ya taa ambayo ingeweza
kuwaka kwa kutumia umeme. Licha ya kufeli mara elfu kumi, aliisimamia ndoto
yake hiyo mpaka ilipogeuka kuwa kitu halisi. Waotaji ndoto kivitendo huwa hawakati
tamaa!
Dunia ya leo imejaa fursa tele ambazo
waotajindoto wa zamani kamwe hawakuzijua. Shauku
kubwa ya kuwa na kutenda ni alama
ya kuanzia ambayo muotajindoto ni lazima aanzie.
..................................
Kipindi muhimu katika maisha ya wale wanaofanikiwa
kwa kawaida huja katika kipindi cha matatizo
..................................
Soma kilichopita kwenye Usomaji huu hapa
Soma kifuatacho kwenye Usomaji huu hapa
.....................................
HUDUMA ZETU MBALIMBALI ZA MALIPO, (MAFUNZO, VITABU & MICHANGANUO)
1. Kujiunga na programu yetu ya MAKE YOURSELF GREAT AGAIN ndani ya group la VIP
Hii ni programu ya mafunzo na mentorship mwaka mzima yenye course mbalimbali ikiwemo, Kujifunza kuandika business plan kwa undani, usomaji wa think & grow rich kwa kina, kujifunza ubunifu kwenye biashara, masoko na mauzo nje na ndani ya mtandao, siri za biashara ya rejareja pamoja na uwekezaji.
Kujiunga ada ni sh. 20,000/= kwa ajili ya vitabu na michanganuo ya rejea lakini kwa sasa ukiwahi muda haujaisha unalipia shilingi 10,000/= tu
Au unanunua tu kitabu cha Think & Grow Rich (Fikiri & Utajirike) softcopy au Hardcopy na kuunganishwa moja kwa moja
Ikiwa utalipia vitabu na michanganuo unapewa papo hapo Vitabu 5 kikiwemo cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali , halafu OFFA ya Michanganuo kamili ya Biashara 7 kama uonavyo hapo chini. Jumla ni vitu 12 unatumiwa.
Michanganuo 7 ya offa iliyoorodheshwa unaweza kubadilisha kabla hujatumiwa kwa kuchagua mwenyewe ile uitakayo miongoni mwa Michanganuo 18 utakayoorodheshewa pale chini kabisa mwishoni ilimradi tu imefika 7. Wasiliana nasi kwa namba 0765553030 / 0761002126
2. Kuandikiwa Mchanganuo wa Biashara yako
Tunaandika Mpango kamili wa biashara yeyote ile kwa Kampuni na wafanyabiashara binafsi kwa gharama rafiki, njoo tuzungumze kupitia namba za simu au wasap 0765553030 / 0761002125 Michanganuo yetu tunaandaa kulingana na maono ya mteja kama yalivyo pamoja na mazingira ya soko linalomzunguka
3. Kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
Kitabu hiki kilichowasaidia wajasiriamali wengi wadogo na wale wa kati kinatatua changamoto mbalimballi za biashara za rejareja kubwa ikiwa ni usimamizi wa mapato yasipotee au kudokolewa kiholela na wasaidizi wako, ni uzoefu wa miaka 12 wa mwandishi mwenyewe kwenye hii biashara.
Kukipata unaweza kulipia Tsh. 10,000/ kupitia namba 0761002125 jina peter Augustino Tarimo, kisha nitakutumia kitabu chako kwenye simu au kompyuta mara moja. Au pia unaweza ukatembelea duka letu la mtandaoni kukinunua hapo kwa kiungo hiki>>MAFANIKIO YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA
4. Kitabu cha THINK & GROW RICH –SWAHILI EDITION (FIKIRI & UTAJIRIKE)
Kitabu hiki kilichosomwa duniani na zaidi ya watu milioni 100 tunayo nakala ya Kiswahili kwa bei zifuatazo;
Nakala ngumu hardcopy ukiwa Dar es salaam ni Tsh. 25,000/= – Tunakuletea mpaka pale ulipo, ukishapokea kitabu ndipo unalipa pesa
Ukiwa mikoa mingine Tanzania tunatuma kitabu kwa njia ya Mabasi kwa gharama jumla Tsh. 35,000/= kitabu na usafiri
Nakala laini Softcopy; Ukiwa popote pale Duniani unaweza kukipata kwenye mtandao wa GETVALUE kupitia kiungo hicho kibofye kuingia ununue sasa hivi na kukidownload.
5. Vitabu zaidi &Michanganuo mbalimbali ya biashara
Kwa vitabu zaidi na Michanganuo mbalimbali ya biashara iliyo tayari tembelea duka letu hili la mtandaoni uweze kuona na kujinunulia kwa urahisi kabisa>>SELF HELP TANZANIA ONLINE BOOSHOP
0 Response to "HAMASA YA LEO ALFAJIRI / EARLY MORNING MOTIVATION - 01/08/2025"
Post a Comment