RIPOTI
YA USOMAJI KITABU THINK & GROW RICH-AWAMU/SESSION- 2 (SURA YA 1)
English
version:
Chapter
1: INTRODUCTION
THE
MAN WHO “THOUGHT” HIS WAY INTO PARTNERSHIP WITH THOMAS A. EDISON
Nakala ya kiswahili:
SURA YA1: Utangulizi
MTU ALIYEFIKIRI NJIA YAKE KUWA
MBIA NA THOMAS A. EDISON
Katika Sura hii ya kwanza Mwandishi anaanza kwa kueleza
jinsi ilivyokuwa kweli kwamba ‘FIKRA
au MAWAZO ni vitu halisi’ na ni vitu vyenye nguvu pale vinapochanganywa na nia
thahiri, msimamo na shauku kubwa katika kuvigeuza kuwa utajiri ama
vitu vingine vinavyoweza kushikika
Tutaona mfano
wa kwanza kabisa atakaoanza nao kuthibitisha kauli hiyo ni habari ama hadithi
ya mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Edwin C. Barners. Bwana huyu siku nyingi
sana alikuwa akigubikwa na shauku kubwa ya kutaka kuwa mbia na mgunduzi maarufu
wakati huo aliyejulikana kama Thomas Edison.
Akiwa na ndoto
yake hii kubwa kumbuka hakuwa na chochote kile mfukoni wala hakuna mtu
aliyekuwa anamjua achilia mbali connection
yeyote ile ambayo labda ingeliweza kumfanya akutane na mgunduzi huyo. Kitu
pekee alichokuwa nacho kichwani mwake ni hilo wazo na shauku kali ya kutaka
kuitimiza ndoto hiyo
Sasa
alifanyafanyaje mpaka ndoto yake ikaja kuwa kweli, tafadhali sana hebu tujumuike
pamoja kusoma kurasa hizi 10 leo.
Alipoona hana
jinsi mwishowe aliamua kusafiri kwa treni la mizigo mpaka mji aliokuwa
akiishi Thomas Edison kuliko kukosa kabisa kwenda. Aliwasili katika maabara ya
Bwana Edison na kutangaza kwamba alikuwa amefika pale kuingia ubia wa kibiashara
na Mgunduzi
Miaka kadhaa
baadae Bwana Thomas Edison mwenyewe katika mkutano mmoja na Edwin C.Barnes
akiwemo alikuja kukiri kwamba alimpatia fursa ile Barnes kutokana na dhamira
yake ya dhati ya kukipata kile alichokuwa akikitaka na alitamka maneno
yafuatayo;
“Nilikuwa nimejifunza kutokana na uzoefu wa
miaka mingi na watu kwamba, mtu anapotamani
sana kitu kiasi cha kuweka rehani mustakabali wake mzima wa baadaye
kwa ajili ya kukipata, bila shaka atakuwa na uhakika wa kufanikiwa kukipata”
Kitu
kilichokuja kubadilisha maisha ya Edwin C. Barnes moja kwa moja na ndoto yake
kutimia akatoboa baada ya kufanya kazi za chini kwa bosi wake huyu muda mrefu
ni chombo kipya cha sauti alichokuwa amekigundua Edison wakati huo ambacho hata
leo hii tunakiita Earphone ama Ediphone.
Tukio hili
lilikuja kama fursa iliyokuwa imejificha katika sura ya jambo lisilowezekana
kabisa kwani kila mtu wakiwemo watu wote wa mauzo kwenye kampuni ya Edison
walikuwa wakisema kwamba chombo kile cha ajabu kisingeliweza kuuzika kirahisi
sokoni
Lakini mwanaume
Edwin C. Barnes akajisemea moyoni, “hapahapa sitakubali, hapa ndipo fursa
yenyewe ilipo”. Yeye aliamini kabisa mashine ile ya ajabu ingeliwe kuuzika bila
wasiwasi wowote sokoni na kazi ikaanza rasmi......
FUTI
TATU TU KUTOKA DHAHABU ILIPO
Katika sura hii
pia kuna hadithi nyingine ya “FUTI
TATU TU KUTOKA DHAHABU ILIPO” ambapo mwandishi anaeleza kisa cha watu wengi
kuwa masikini kwa sababu tu ya kukata tamaa hata pale ambapo kumbe ilikuwa
imebakia kidogo tu watoboe.
Habari hii inamhusu mjomba wake Bwana mmoja aliyeitwa R. U. Darby aliyekumbwa na “Homa ya dhahabu” kipindi cha mfumuko wa machimbo ya dhahabu huko
Marekani na akaenda Magharibi kuchimba ili aweze kutajirika.
Lakini
kilichotokea ni kwamba baada ya kuchangisha pesa kutoka kwa ndugu jamaa na
marafiki kwa ajili ya ufadhili wa mradi ule na wakaingia mgodini kuchimba
hatimaye yeye na mjombake walikata tamaa na kuuza ule mgodi kwa Muokota makopo
mmoja mjanja ambaye alikuja kutajirika muda mfupi tu baada ya wao kurudi
nyumbani.
Kumbe kipindi
wanakata tamaa ilikuwa imebakia kama futi tatu tu wakutane na mwamba wenye
dhahabu ya kutosha!
SOMO
LA SENTI 50 KATIKA KUWA NA MSIMAMO
Stori nyingine ni hii ambayo pia inamhusu huyuhuyu Bwana
Darby na mjomba wake pamoja na mtoto mdogo mweusi wa mpangaji wao. Baada ya
kurudi kutoka machimboni walikoanguka vibaya, Darby na mjombake maisha yaliendelea na mjomba
kwa bahati nzuri alikuwa akimiliki shamba kubwa ambalo ndani yake kulikuwa na
wapangaji wakati huo wengi wakiwa ni Waafrika weusi maskini
Siku moja Darby na mjombake wakiwa kwenye kinu cha
kusagia nafaka wanapiga kazi, ghafla akaja mtoto wa mpangaji mmoja na
kumjulisha mjomba kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa na shida na aliomba apatiwe
senti 50 tu. Lakini mjomba alikataa katakata na kumtaka yule mtoto aondoke mara
moja kurudi kwa mama yake.
Hata hivyo mtoto alionyesha ung’ang’anizi wa ajabu na
katu hakukubali kuondoka pale mpaka mjomba akatishia kumchapa bakora. Mwishowe
mjomba mwenyewe alichoka akaingiza mkono mfukoni na kuchomoa senti 50 akampatia
yule mtoto akaenda zake.
Sasa ni nguvu gani hii ya ajabu iliyoyeyusha moyo wa yule
mjomba hata akaahirisha kumchapa yule mtoto bakora na kumtimizia kile
alichokitaka? nguvu hiyo utaenda kuijua ukisoma hiki kitabu mpaka mwisho.
Bwana Darby miaka mingi baadae alikuja akawa
mfanyabiashara mkubwa sana wa kuuza bima na katika maisha yake ya biashara
mafunzo haya mawili aliyoyapata moja akiwa na mjomba wake kwenye machimbo ya
dhahabu na la pili akiwa na mjombake kwenye kinu cha kusaga nafaka ambapo mtoto
mweusi wa mpangaji alimtia mjomba adabu yalimsaidia sana, yalimwezesha hatimaye
apate naye mafanikio makubwa kwenye biashara hii ya kuuza bima licha ya mapigo
hayo 2, na hadidhi hii alimsimulia Napoleo Hill katika eneo lilelile kilipokuwa
kinu cha kusaga nafaka zamani.
Napoleon
anaendelea kutuambia kuwa, maisha ni ya ajabu, na mara nyingi hayafikiriki!
Vyote, kufanikiwa na kuanguka vina mizizi yake katika uzoefu wa vitu rahisi
kama hadithi hizo mbili za Darby na mjombake zilizosimuliwa hapo juu.
Utajiri huanza
na hali ya akili, pamoja na udhahiri wa lengo, huku kukiwa na kazi kidogo sana
au hata kutokuwa na kazi ngumu kabisa. Wewe na mtu mwingine yeyote, mnapaswa
muwe wenye kuvutiwa na kufahamu jinsi ya kuwa na hali ya akili inayovutia
utajiri.
Mara unapozielewa vizuri kanuni za falsafa
13 zilizoandikwa humu kwenye hiki kitabu na kuzitia kwenye matendo hali yako
kifedha itaanza kuimarika. Kila kitu utakachogusa kitaanza kugeuka chenyewe kuwa
rasilimali kwa faida yako na neno HAIWEZEKANI kwako litakuwa halipo kabisa
Mafanikio huja kwa wale wenye kufikiria
mafanikio.
Kuanguka huja kwa wale ambao pasipo
kujali hujiruhusu wenyewe kufikiri kuanguka. Lengo la kitabu hiki
ni kuwasaidia wale wote wanaotaka kujifunza stadi za kubadilisha mawazo yao
kutoka kufikiria maanguko kuwa katika kufikiria
mafanikio.
SIRI YA MAFANIKIO YA HENRY FORD
Mwandishi
anaelezea habari nyingine kumhusu Mgunduzi wa magari Bwana Henry Ford ambaye
nyakati fulani hivi akiwa amebuni injini ya gari lake aina ya V-8 Motors,
alichagua kuunda injini yenye silinda zote 8 ndani ya bloku moja lakini
mainjinia wake (wahandisi) walimkatalia katakata kuwa isingeliwezekana, hata
hivyo Ford hakuwakubalia pia kirahisi akawataka ni lazima waunde ile injini
piga ua! Na mwishowe kweli kama mazingaombwe iliwezekana, dhamira ya Ford ikawa
imeshinda!
Henry Ford
amefanikiwa kwa sababu anafahamu na kuzitumia kanuni za mafanikio. Moja kati ya
hizo ni SHAUKU: mtu kufahamu kitu unachotaka
WEWE
“NDIYE BOSI WA MAISHA YAKO, NAHODHA WA ROHO YAKO
Mwandishi amenukuu
mistari ya shairi la Mshairi mmoja wa Kiingereza aitwaye W.C. Henley isemayo “Mimi ni kiongozi wa majaaliwa yangu, mimi ni
nahodha wa roho yangu” Hapa alitaka kutuambia kwamba, sababu ya sisi kuwa
bosi wa maisha yetu, nahodha wa roho zetu ni uwezo wa kudhibiti mawazo(fikra)
zetu.
Napoleon anasema kwamba mshairi
alitaka kutueleza juu ya nguvu ya ajabu ya Kiulimwengu iliyojazwa angani na
ambayo hujigeuza yenyewe
kuwa katika mfumo wa mawazo tunayofikiri katika akili zetu, na hutuathiri kwa
njia za kawaida katika kubadilisha mawazo yetu kwenda katika mfumo wa vitu
vinavyoweza kushikika.
Nguvu hii haibagui kati ya mawazo
yanayobomoa na yale yanayojenga, itageuza kuwa vitu vinavyoshikika mawazo ya
umasikiki sawasawa tu na vile ambavyo ingegeuza mawazo ya utajiri kuwa vitu
vinavyoshikika. Ubongo (akili) zetu hupata nguvu mithili ya sumaku kwa mawazo
yanayotawala katika akili zetu kwa njia ambayo hakuna mtu anayefahamu. “Sumaku”
hizi huvuta kwetu nguvu, watu, mazingira katika maisha yanayoendana na aina ya
mawazo yanayotawala fikra zetu.
Kabla hatujaweza kujipatia utajiri
kwa kiasi kikubwa ni lazima kwanza tuziambukize akili zetu na shauku kubwa ya
utajiri mithili ya sumaku vile ifanyavyo, hii inamaanisha kwamba
tuzishughulishe akili zetu kuwaza (kufikiri) maswala yahusuyo fedha mpaka hamu
hiyo inatufikisha hatua ya mpango kamili wa kuzipata.
Kidogokidogo ukweli umejifunua
wenyewe kwamba, kanuni 13 zilizoelezwa ndani ya kitabu hiki zinabeba siri za
namna ya kuyathibiti maisha yetu kiuchumi.
Mpaka
hapo mpenzi msomaji wangu tumemaliza kurasa zetu 10 na tunakaribia kabisa
kufika tamati ya Sura nzima ya kwanza kwani sura hiyo haikuwa na mambo mengi
sana ilikuwa tu ni Utangulizi na mwandishi, bado hakuwa ameanza kueleza kanuni
zake 13 za mafanikio.
Kurasa
10 zitakazofuata au session ya 3, tutamalizia kidogo kurasa chache zilizobakia
za sura ya kwanza na kuanza kusoma Sura ya pili yenye Kanuni ya kwanza kabisa
ya mafanikio ambayo ni SHAUKU, kaa tayari.
Usikose
pia Early morning Motivation ya kesho Alfajiri saa 11 juu ya alama. Tutakuwa na
mistari ya hamasa kutoka katika kurasa 10 za session ya tatu (3)
Soma kilichopita kwenye Usomaji huu
Soma kifuatacho kwenye Usomaji huu
.....................................
HUDUMA ZETU MBALIMBALI ZA MALIPO, (MAFUNZO, VITABU & MICHANGANUO)
1. Kujiunga na programu yetu ya MAKE YOURSELF GREAT AGAIN ndani ya group la VIP
Hii ni programu ya mafunzo na mentorship mwaka mzima yenye course mbalimbali ikiwemo, Kujifunza kuandika business plan kwa undani, usomaji wa think & grow rich kwa kina, kujifunza ubunifu kwenye biashara, masoko na mauzo nje na ndani ya mtandao, siri za biashara ya rejareja pamoja na uwekezaji.
Kujiunga ada ni sh. 20,000/= kwa ajili ya vitabu na michanganuo ya rejea lakini kwa sasa ukiwahi muda haujaisha unalipia shilingi 10,000/= tu
Au unanunua tu kitabu cha Think & Grow Rich (Fikiri & Utajirike) softcopy au Hardcopy na kuunganishwa moja kwa moja
Ikiwa utalipia vitabu na michanganuo unapewa papo hapo Vitabu 5 kikiwemo cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali , halafu OFFA ya Michanganuo kamili ya Biashara 7 kama uonavyo hapo chini. Jumla ni vitu 12 unatumiwa.
Michanganuo 7 ya offa iliyoorodheshwa unaweza kubadilisha kabla hujatumiwa kwa kuchagua mwenyewe ile uitakayo miongoni mwa Michanganuo 18 utakayoorodheshewa pale chini kabisa mwishoni ilimradi tu imefika 7. Wasiliana nasi kwa namba 0765553030 / 0761002126
2. Kuandikiwa Mchanganuo wa Biashara yako
Tunaandika Mpango kamili wa biashara yeyote ile kwa Kampuni na wafanyabiashara binafsi kwa gharama rafiki, njoo tuzungumze kupitia namba za simu au wasap 0765553030 / 0761002125 Michanganuo yetu tunaandaa kulingana na maono ya mteja kama yalivyo pamoja na mazingira ya soko linalomzunguka
3. Kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
Kitabu hiki kilichowasaidia wajasiriamali wengi wadogo na wale wa kati kinatatua changamoto mbalimballi za biashara za rejareja kubwa ikiwa ni usimamizi wa mapato yasipotee au kudokolewa kiholela na wasaidizi wako, ni uzoefu wa miaka 12 wa mwandishi mwenyewe kwenye hii biashara.
Kukipata unaweza kulipia Tsh. 10,000/ kupitia namba 0761002125 jina peter Augustino Tarimo, kisha nitakutumia kitabu chako kwenye simu au kompyuta mara moja. Au pia unaweza ukatembelea duka letu la mtandaoni kukinunua hapo kwa kiungo hiki>>MAFANIKIO YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA
4. Kitabu cha THINK & GROW RICH –SWAHILI EDITION (FIKIRI & UTAJIRIKE)
Kitabu hiki kilichosomwa duniani na zaidi ya watu milioni 100 tunayo nakala ya Kiswahili kwa bei zifuatazo;
Nakala ngumu hardcopy ukiwa Dar es salaam ni Tsh. 25,000/= – Tunakuletea mpaka pale ulipo, ukishapokea kitabu ndipo unalipa pesa
Ukiwa mikoa mingine Tanzania tunatuma kitabu kwa njia ya Mabasi kwa gharama jumla Tsh. 35,000/= kitabu na usafiri
Nakala laini Softcopy; Ukiwa popote pale Duniani unaweza kukipata kwenye mtandao wa GETVALUE kupitia kiungo hicho kibofye kuingia ununue sasa hivi na kukidownload.
5. Vitabu zaidi &Michanganuo mbalimbali ya biashara
Kwa vitabu zaidi na Michanganuo mbalimbali ya biashara iliyo tayari tembelea duka letu hili la mtandaoni uweze kuona na kujinunulia kwa urahisi kabisa>>SELF HELP TANZANIA ONLINE BOOSHOP
0 Response to "RIPOTI YA USOMAJI THINK & GROW RICH AWAMU YA PILI (PAGE 9 – 18 / UKURASA.17 – 37) SURA YA 1"
Post a Comment