RIPOTI YA USOMAJI KITABU CHA THINK & GROW RICH KURASA ZA MWANZO NA DIBAJI YA MWANDISHI-SIKU YA KWANZA, 29/07/2025 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

RIPOTI YA USOMAJI KITABU CHA THINK & GROW RICH KURASA ZA MWANZO NA DIBAJI YA MWANDISHI-SIKU YA KWANZA, 29/07/2025


Writen by Napoleon Hill, Translated by Peter Tarimo

JALADA LA MBELE – COVER PAGE

Narejea nakala ya Kiswahili kidogo na nitarudi kwa nakala ya kiingereza nikifika kwenye Dibaji ya mwandishi.

Jalada limenakshiwa pembezoni kwa picha za noti pesa ya Kitanzania aina mbalimbali toka Uhuru mpaka sasa. Katikati lina rangi ya njano na maandishi makubwa meusi mchanganyiko na ya rangi nyeupe na nyekundu kidogo

Kisha unafuata ukurasa uliobeba jina la kitabu kwa lugha zote 2 na majina ya mwandishi na Mfasiri wa kitabu. Ukurasa unaofuata ni wa Hakimiliki, ISBN namba pamoja na anuani ya mfasiri. Unafuata ukurasa wa Wakfu kisha Yaliyomo na Shukrani unaoanza kwa namba za kirumi ‘i’

SHUKRANI

Kwenye shukrani mfasiri ametoa shukrani zake za dhati kwanza kwa Mwenyezi Mungu muweza wa yote, kisha kwa Familia na Waandishi wengine waliomhamasisha kwenye kazi za uandishi

DIBAJI YA MWANDISHI

Katika Dibaji ya mwandishi mwenyewe Bwana Napoleon Hill anaanza kwa kuelezea Siri ya kupata pesa iliyozungumziwa ndani ya hiki kitabu. Anasema siri hiyo ndiyo iliyowawezesha watu 500 matajiri zaidi aliowahoji kufikia pale walipokuwa

Anasimulia kwamba siri hiyo alijulishwa kwa mara ya kwanza kabisa na mtu aliyekuwa tajiri zaidi Marekani wakati huo na aliyejulikana kwa jina la  Andrew Carnegie wakati alipokwenda kufanya naye mahojiano (Kumbuka Hill alikuwa mwandishi habari)

Bwana Carnegie alimtaka Napoleon Hill aende kuifanyia majaribio kanuni (siri) hiyo kwa watu wengine Wanaume kwa Wanawake katika kila nyanja ili kuonyesha utimilifu wake

Katika Dibaji hii mwandishi anajaribu kuelezea kwa kifupi jinsi kanuni ama siri iliyoko ndani ya kitabu ilivyobadilisha maisha ya watu mbalimbali kama sura nyingine za kitabu hiki zitakavyokwenda kubainisha kuanzia Sura ya kwanza mpaka ile ya 15 ambamo pia ndipo zinakopatikana kanuni 13 za Mafanikio

Ametaja kwa mfano Sura ya 3 inayohusu IMANI, jinsi Shirika moja la chuma cha pua huko Marekani lilivyoitumia siri hii chini ya kijana mmoja aitwaye Charles M. Schwab. Siri hii pia ilitumiwa na watu wengine wengi kwa mafanikio makubwa mfano kina Randolf na wengineo

Anasema Siri imetajwa mara nyingi sana lakini siyo moja kwa moja. Ni kwa aliyekuwa tayari tu kuipokea na kuitafuta ndio anayeweza kuipata. Ikiwa mtu upo tayari kuitumia, anasema utaigundua tu angalao mara moja katika kila sura ya kitabu hiki.

Kitu cha kustaajabisha kuhusu siri hii ni kwamba wale wamaoichuka na kuitumia hujikuta wenyewe wakipata mafanikio makubwa huku wakitumia nguvu kidogo sana na kamwe huwa hawarudi tena kwenye maanguko.

Anasema mtu huhitaji Elimu kubwa ndipo uweze kunufaika na siri hiyo kwani watu wengi walioitumia kwa mafanikio makubwa  walikuwa na elimu kidogo sana mfano kina Henry Ford na John Wanamaker

Hili mwishowe anawataja kwa majina baadhi tu ya watu Matajiri aliowahoji kwenye safari yake hiyo ya miaka zaidi ya 20 na kusema majina hayo machache yanawakilisha baadhi ya mamia ya watu wengine mashuhuri Marekani walioweza kufanikiwa kwa kutumia kanuni ya Carnegie

Mwisho anamalizia kwa kusema; “Ikiwa upo tayari kwa siri hii tayari unayo nusu ya siri yenyewe, Utaitambua nusu ya siri iliyobakia punde tu itakapofika akilini mwako” Akimaanisha wakati ukisoma kitabu hiki

 

DIBAJI YA MFASIRI

Katika nakala ya Kiswahili kuna hii Dibaji ya mfasiri ambapo alielezea umuhimu wa lugha ya Kiswahili kama lugha inayojitosheleza katika nyanja zote kuu za kimaisha akitolea mifano vitabu vilivyowahi kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kama vile vitabu vitakatifu vya Biblia na Qurani Tukufu.

Lakini pia vitabu vya Shakespear alivyotafsiri Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mapepari wa Venis na Julias Kaizari pamoja na hiki cha Think & Grow Rich. Alieleza pia sababu kubwa iliyomsukuma kufanya kazi hii ya kukitafsiri hiki kitabu

......MWISHO WA RIPOTI YANGU YA LEO...

Tukutane tena kwenye ripoti zijazo, nategemea  washiriki wengine pia kuandaa ripoti zao hasahasa ile ya Sura nzima, lakini hata mtu waweza kuandaa ya kurasa 10 tunazosoma kila siku. Andaa vyovyote vile jinsi ulivyoelewa na mafunzo uliyoyapata  

Peter A. Tarimo

0765553030 / 0761002125

 

Tukutane Kesho Alfajiri saa 11 kwenye Early Morning motivation, Dont Miss kwani ikiwa kama kweli wewe ni mwanamafanikio unayetafuta kuujenga ukuu wako sidhani kama saa 11 inakukuta umejifunika shuka.

 

Soma kilichopita kwenye usomaji huu hapa 

Soma kifuatachi kwenye usomaji huu hapa


HUDUMA ZETU NYINGINE MBALIMBALI, VITABU & MICHANGANUO YA BIASHARA

 

1. KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA

Tunaandika mipango ya biashara kwa ajili ya Wajasiriamali na Makampuni inayoendana na mazingira yao halisi kwa gharama rafiki sana, tuwasiliane kwa namba 0765553030 au 0712202244.  Unaweza pia kuona baadhi ya kazi za wateja wetu hapa kwa ufupi tulizowahi kufanya

2. KUANDIKA WASIFU WA BIASHARA (COMPANY PROFILE)

Tunaandika company profile zenye mvuto na za kipekee kulingana na maono ya mteja mwenyewe na gharama huanzia Tsh. 50,000/=

3. KITABU CHA FIKIRI & UTAJIRIKE (THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION)  

Dar es salaa tunampelekea mteja alipo kwa gharama ya Tsh. 25,000/= na mteja hufanya malipo akishapokea kitabu. Mikoa mingine kwa mabasi ni sh. 35,000/=. Nakala laini (softcopy) kinapatikana app ya GETVALUE popote pale ulipo, bonyeza link hiyo kununua.

4. KITABU CHA MAFANIKIO BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA & GENGE TOLEO LA 2025

Nakala ngumu  ni Tsh. 20,000/= Dar tunamfikishia mteja alipo, anapokea kitabu ndipo analipa na Mikoa mingine kwa mabasi ni Tsh. 30,000/= Nakala laini (softcopy) tunatuma kwenye simu au kompyuta ya mteja kwa bei ya Tsh. 10,000/= Pia unaweza kununua mtandaoni kwenye duka letu kwa bofya kiungo hiki>>>Siri ya mafanikio ya biashara ya duka la rejareja 2025 & genge ndani yake

5. VITABU ZAIDI & MICHANGANUO YA BIASHARA

Kupata vitabu vingine zaidi pamoja na Michanganuo ya biashara mbalimbali iliyokwisha andaliwa tayari tembelea Duka letu la mtandaoni kwa kiungo kifuatacho>>>; Augustinopeter bookshop

Watsap/Call/Sms: 0765553030 au 0761002125

Peter Augustino Tarimo


0 Response to "RIPOTI YA USOMAJI KITABU CHA THINK & GROW RICH KURASA ZA MWANZO NA DIBAJI YA MWANDISHI-SIKU YA KWANZA, 29/07/2025"

Post a Comment