MPANGO WA FEDHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MPANGO WA FEDHA

SOMO LA KUMI

SOMO LA 10

                        
7.0 MAKISIO YA FEDHA
Mchanganuo wa biashara ni mchanganyiko wa maelezo na namba zinazowakilisha hesabu na taarifa mbalimbali. Tangu sehemu zilizopita huko nyuma tulikwishaanza kuona baadhi ya hesabu kwa mfano katika maelezo ya kampuni tuliona jedwali la vyanzo vya mahitaji kwa biashara mpya pamoja na jedwali la hesabu za kipindi cha nyuma kwa biashara ya zamani.

Tuliona pia hesabu ya makisio ya mauzo, gharama za mauzo, gharama za uendeshaji na jedwali la mishahara kwenye kipengele cha uongozi na wafanyakazi.

Katika kipengele hiki cha makisio ya fedha ndipo unapotakiwa kuunganisha hesabu hizo nyingine ndogondogo zote na kutengeneza makisio ya taarifa tatu muhimu ambazo ni, Faida na Hasara, Fedha taslimu na Mizania ya biashara.

Kimsingi hesabu za mpango wa biashara ni tofauti na hesabu halisi za kawaida za biashara kwani ni makisio, zinafanana tu kimuundo. Kwa hiyo mtu hauhitaji kuwa mhasibu au mtaalamu wa biashara aliyebobea ndipo uweze kukisia taarifa hizo ingawa pia mtu atahitajika kuwa na uelewa wa msingi wa hesabu za biashara. Ikiwa unaandika mpango wa biashara na sehemu hii inakutatiza unaweza ukamtafuta mtaalamu au mwenye uzoefu wa kutosha akakusaidia eneo hili.

Tofauti nyingine ni kwamba, hakuna mtu atakayeweza kukuwajibisha kisheria kwa kukisia mahesabu ya mpango wa biashara yanayotofautiana na hesabu halisi lakini katika uhasibu unaweza hata kufungwa jela kwa kuandika ripoti za hesabu zisizokuwa sahihi.

Makisio ya mpango wa biashara mara nyingi huwa tofauti na hesabu halisi wakati wa kutekeleza mpango na unatakiwa uwe unafanya mapitio kujua mpango wako wa biashara na hali halisi vimepishana kwa kiasi gani na hivyo ufanye kitu gani zaidi kurekebisha.

 

Vipengele vidogo katika sehemu hii ni hivi vifuatavyo,…………………..

 …………………….Inaendelea kwenye group la Michanganuo-online

 

Semina hii iliyofanyika katika group la Michanganuo-online unaweza ukaipata muda wowote ule katika mfumo wa e-book ukiwa mwanachama wa group hilo. Unaidownload katika channel yetu ya telegram au pia tunaweza kukutumia moja kwa moja inbox katika watsap ama email yako.

Kama unahitaji kupata semina hii pamoja na masomo mengine yote yaliyowahi kufundishwa katika group letu zaidi ya masomo 70 jiunge kwa kutoa kiingilio chako sh. Elfu 10 tu na ada hii ni ya miezi 12/mwaka mzima.

Kulipia tumia namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo na ujumbe watsap au sms usemao “NATAKA SEMINA KUBWA YA KUANDIKA MICHANGANUO”

 

 

0 Response to "MPANGO WA FEDHA"

Post a Comment