JINSI YA KUANZISHA BIASHARA: HATUA 12 MUHIMU ZAIDI ZA KUFUATA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUANZISHA BIASHARA: HATUA 12 MUHIMU ZAIDI ZA KUFUATA

Mama anayeanza kufanya biashara
Unapoandika kuhusiana na biashara na ujasiriamali huwezi ukakwepa kuulizwa maswali mbalimbali yanayohusiana na jinsi ya kuanzisha biashara hata kama maswali hayo yanaonekana kuwa ni ya kawaida sana na tayari yameshajibiwa mahali pengine kwingi mitandaoni na hata nje ya mitandao ya kijamii.

Maswali kama vile, Naomba kujua hatua za kuanzisha biashara, namna ya kuanza biashara na mtaji mdogo, namna ya kuanzisha biashara bila mtaji na mengine mengi.

Kuna msomaji wangu mmoja kwa kutumia email alinitumia swali hili hapa chini namimi nikaona nilijibu kama ifuatavyo;

Je, ni hatua gani zinazofaa zaidi kuanzisha biashara?

JINSI YA KUANZISHA BIASHARA: HATUA 12 ZA KUFUATA

MAJIBU YA SWALI HILO KWA KIFUPI NI HAYA HAPA CHINI;

1.       Tambua kwanza una kipaji gani, taaluma, uzoefu au unapendelea zaidi kitu gani katika maisha yako

2.       Jiulize jamii inayokuzunguka ina mahitaji gani au wana tatizo lipi linalohitaji suluhisho

3.       Fikiria au tafuta wazo la biashara utakayoweza kuifanya kwa kutumia vigezo namba 1 & 2

4.       Fanya utafiti wa wazo lako hilo la biashara kuulizia ujue kila kitu kinachohusiana nayo kipoje

5.       Andaa mpango wa biashara ya wazo lako, siyo lazima uuandike mahali mpango huo, just tu unaweza ukaufikiria kichwani utautekeleza-tekelezaje

6.       Tafuta/andaa rasilimali zinazohitajika ukiwemo mtaji pesa, rasilimaliwatu na ujuzi.

7.       Anza kidogokidogo kwa kutumia rasilimali ulizopata usisubiri mpaka upate kila kitu, vingine utapata mbele kwa mbele

8.       Sajili biashara yako mamlaka zinazohusika kisheria

9.       Endesha biashara yako 

10.  Tafuta nyenzo mbalimbali kama vile wafanyakazi, mikopo au wabia pamoja na teknolojia mbalimbali ili ukue na kutajirika

11.  Fungua matawi na wekeza katika biashara nyingine tofautitofauti zinazolipa

12.  Andaa mapema mtu wa kukurithi kwani binadamu hatuishi duniani milele.

Hatua mbalimbali nilizozitaja hapo juu unaweza ukapata ufafanuzi wake kwa kirefu ndani ya kitabu changu kiitwacho, MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, kitabu ambacho kina kila kitu mjasiriamali yeyote yule mdogo anayeanza na wale waliokwisha anza lakini bado hawajafikia hatua za juu kuweza kufikia hatua hizo kwa urahisi kabisa. 
Kitabu hiki kinapatikana kwa njia ya email kama kitabupepe(Softcopy) kwa sh. Elfu 10 na pia kama kitabu cha kawaida cha karatasi(Hardcopy) kwa sh. Elfu 22 Kukipata wasiliana na mimi kwa Whatsap; 0765553030 au Simu/sms: 0712202244

Unaweza pia kukipata katika offa inayokaribia kuisha muda wake ambapo unapata vitu mbalimbali kikiwemo kitabu hiki(softcopy) pamoja na kuunganishwa na group la masomo ya kila siku la whatsaa la MICHANGANUO-ONLINE, lipia elfu 10 kwa namba 0765553030 kisha tuma ujumbe usemao; NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO PAMOJA NA OFFA INAYOKARIBIA KUISHA MUDA WAKE"


SOMA PIA MAKALA NYINGINE NZURI HAPA CHINI;

1. Jinsi kiwanda kidogo kinavyoweza kukutoa kimaisha na kuwa tajiri wa kutupa.

2. Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado

3. Ni biashara ndogo yenye mtaji mdogo, faida ndogo lakini inayokua upesi.

4. Mwaka huu wa 2020, ishi kama Tai usikubali tena kuishi kama kunguru.

0 Response to "JINSI YA KUANZISHA BIASHARA: HATUA 12 MUHIMU ZAIDI ZA KUFUATA"

Post a Comment