SIRI KUBWA 5, KWANINI HUWA TUNACHELEWA KUFANIKIWA KIFEDHA MAISHANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SIRI KUBWA 5, KWANINI HUWA TUNACHELEWA KUFANIKIWA KIFEDHA MAISHANI

Kila mtu angependa kuzifahamu siri kubwa za mafanikio kiuchumi ili hatimaye aweze kumiliki mali na fedha za kutosha katika maisha yake yote na pengine hata kizazi chake chote kisijekuhangaika tena kwenye umasikini. Lakini jambo hili limekuwa gumu kwa watu wengi na sababu kubwa ni hizi hapa chini;

Woga na kutojiamini, Kwanini niwe mimi?)
Kizingiti cha kwanza kabisa kinachowazuia watu wengi kupata fedha na hatimaye kuwa huru kifedha ni ile hali ya kujiuliza, kwani mimi ni nani mpaka nitajirike? Kwanza kwenye ukoo wetu hakuna mtu hata mmoja aliyewahi hata kumiliki pikipiki, mimi nitawezaje?.

Watu wengi tumezaliwa na kukulia katika familia masikini, tukasoma na watoto wa familia masikini kama sisi na hata baada ya masomo tuliendelea kuzungukwa na watu walewale masikini pasipo hata kuwa na watu wa mfano(role models) hivyo kutokuzijua vyema njia kuu za mafanikio na kuziweka katika vitendo ili kufanikiwa katika biashara na miradi mbalimbali ya uwekezaji kiuchumi

Hii ndiyo sababu wakati mwingine unakuta wale watu wanaokulia katika familia zenye uwezo kiuchumi inakuwa rahisi sana kwao pia kupata mafanikio ya kiuchumi haraka kwasababu tokea mwanzo wanaamini kwamba mafanikio ni kitu cha kawaida kwao na kinachowezekana na wala siyo kwamba mafanikio yao yanatokana na utajiri wa familia zao.

2. Kutokufanya maamuzi.
Sababu ya pili watu hatufanikiwi kirahisi ni kutokuchukua hatua. Mtu anaweza akahudhuria semina za mafanikio, akasoma vitabu vingi tu vya pesa na mafanikio, akawa karibu kabisa na watu waliofanikia kiuchumi lakini hakuna kitakachoweza kubadilika kwake endapo hatafanya maamuzi na kuchukua hatua ya kufanya jambo. 

Ataishia tu kubakia katika hali ileile aliyokuwa nayo zamani. Kanuni za mafanikio zinamtaka kila anayetaka kufanikiwa maishani basi ahakikishe anatekeleza mambo kwa vitendo na wala siyo kubakia na ndoto tu kichwani siku zote.

Ikiwa utaendelea kufanya vilevile ulivyozoea kufanya siku zote, utaendelea kupata matokeo yaleyale uliyozoea kupata kila siku”- Albert Einstain.

3. Kuahirisha(Labda nitafanya kesho)
Hii ni sababu ya tatu kwanini hatupati pesa na mafanikio kwa urahisi. Watu siku zote hatukosi visingizio vya kutokufanya kile tunachotakiwa kufanya ili kujipatia mafanikio kifedha.

Utasikia “Oo..nasubiri kwanza mwezi huu wa Ramadhani uishe ndio nianze” hata kama biashara yenyewe haihusiani kabisa na vyakula, “Mara..oo.. nasubiri msimu wa Krismasi na mwaka mpya ufike ndiyo nianzishe biashara yangu ya nguo” Unashangaa miezi yote iliyobakia mpaka msimu wa Krismasi ufike atakuwa akifanya kitu gani.

Wengine, “kipindi hiki siyo kizuri, nasubiri masika iishe kwanza” nk. Ilimradi tu watu tunakwepa kuchukua hatari na kuishia kuahirisha mambo, siku zinapita, miezi, miaka bila kufanya kitu cha maana. Na linapokuja suala kama hili la janga la corona ndio kabisaa! kuna wengine watalala tu ndani badala ya kujishughulisha wangali wakichukua tahadhari ya kutosha. Maana ya mafanikio siyo kukaa na kujibweteka ni lazima tufanye kazi.

..........................

Mpenzi msomaji somo hili litafundishwa mpaka mwisho leo tarehe 24/4/2020 katika Magroup ya Whatsap ya Michanganuo-online pamoja na Channel yetu ya Telegramu.

Huwa kila siku tunajifunza masomo ya fedha na Michanganuo ya biashara bunifu zinazolipa.

Kiingilio ni sh. elfu 10 tu kwa mwaka huu wote wa 2020, unapewa pia offa ya vitu mbalimbali kama ifuatavyo mara tu baada ya malipo;


1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI -kwa kiswahili

2.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-kwa kiingereza

3.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)-kwa kiswahili

4.  Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikiti maji(KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kwa kiswahili

5.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) -kwa Kiswahili & kiingereza


Kulipia tumia namba zifuatazo; 0765553030  au 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma na ujumbe usemao, "NIUNGANISHE NA MAGROUP YA MICHANGANUO-ONLINE NA OFFA YA VITU 6"

Ikiwa hukusoma semina yetu ya mchanganuo wa kiwanda cha usagishaji nafaka(DONA) bonyeza hapo ni bure/free hulipi chochote

0 Response to "SIRI KUBWA 5, KWANINI HUWA TUNACHELEWA KUFANIKIWA KIFEDHA MAISHANI"

Post a Comment