SEMINA SIKU YA 7: MPANGO WA BIASHARA, KIWANDA CHA USAGISHAJI NAFAKA HATUA KWA HATUA (USADO MILLING) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA SIKU YA 7: MPANGO WA BIASHARA, KIWANDA CHA USAGISHAJI NAFAKA HATUA KWA HATUA (USADO MILLING)

familia bora hula dona
Ikiwa ni siku ya mwisho ya semina yetu hii, leo tunaangalia sura ya mwisho ya mchanganuo wa biashara ya kiwanda cha Usagishaji unga wa dona cha USADO Milling, Vielelezo au Viambatanisho.

Sura hii huwa haina vitu vingi sana labda tu mchanganuo wako nao uwe mrefu sana. Kimsingi huwekwa au kuambatanishwa vile vitu ambavyo hukuweza kuviweka ndani ya mchanganuo wako kutokana na urefu au umuhimu wake kutokuwa mkubwa sana kwa ajili ya msomaji wako kufanya marejeo atakapohitaji kufanya hivyo.


9.0 VIELELEZO
Katika kipengele hiki cha vielelezo kuna vitu vingi ningeweza kuambatanisha lakini hapa nimeweka Majedwali mbalimbali ya hesabu ambayo sikuweza kuyaweka ndani ya sura za ndani za mchanganuo wenyewe.

Ningeliweza pia kuweka, mikataba ya biashara USADO iliyofanya na wadau wake mbalimbali, picha na ramani, kopi za matangazo, CV za viongozi, nyaraka za dhamana za mikopo, nyaraka za utafiti uliofanyika nk.


SEMINA SIKU-6  
…………………………………....


Mpaka kufikia hapa ndugu msomaji wangu nimefikia tamati ya mafunzo haya yaliyochukua siku 7. Mafunzo haya utanufaika nayo zaidi endapo tu utayafuatilia huku ukiwa na Mpango kamili wa biashara ya kiwanda cha USADO Milling pamoja na Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.

Kitabu ambacho kina mafunzo ya kina kabisa juu ya uandaaji wa michanganuo ya biashara. Kitabu hiki kinafundisha namna mtu anavyoweza kuandika Mpango wa biashara yeyote ile kwa njia rahisi pamoja na mifano ya Michanganuo ya biashara mbalimbali zilizofanyiwa utafiti wa kina. Kitabu pia kina course nyingine zote za Biashara na ujasiriamali mjasiriamali yeyote anazohitaji.

Karibu pia katika magroup yetu ya Whatsap na Channel ya Telegram kwa ajili ya mafunzo zaidi ikiwa utahitaji. Magroup yetu ya MICHANGANUO-ONLINE ukijiunga mafunzo ni mwaka mzima kwa malipo ya mara moja tu sh. 10,000/=, huwa hatuna malipo yaliyojificha nyuma ya pazia.

Masomo yetu makuwa kila siku yanahusu vitu viwili vifuatavyo

(1) Michanganuo ya Biashara bunifu zinazolipa
(2) Fedha/Financia Literacy.

Aidha mada nyinginezo kuhusiana na biashara, ujasiriamali na maendeleo binafsi kwa ujumla vinapewa nafasi.


Asante sana.

PETER AUGUSTINO TARIMO

WHATSAPP/CALL: 0765553030

SMS/CALL:             0712202244  SEMINA SIKU-6                

0 Response to "SEMINA SIKU YA 7: MPANGO WA BIASHARA, KIWANDA CHA USAGISHAJI NAFAKA HATUA KWA HATUA (USADO MILLING)"

Post a Comment