KAMATA, PELEKA JELA WEZI HAWA 3 WANAOKUIBIA MUDA WAKO USIPATE PESA NYINGI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KAMATA, PELEKA JELA WEZI HAWA 3 WANAOKUIBIA MUDA WAKO USIPATE PESA NYINGI


Watu tuna masaa mengi mchana ambayo huwa hatuyatumii kikamilifu inavyotakiwa. Kuna vitu vingi huwezi kuamini vinakula muda wetu wakiwemo wezi maarufu 3 wa muda na kusababisha tusiweze kupata pesa kama vile ambavyo tungependa tupate. Hebu fikiria kila siku unatamani kufungua biashara au mradi wako wa pembeni ili uboreshe zaidi kipato chako badala ya kutegemea tu mshahara au faida ya biashara yako kuu. 

Unajitahidi uwe na kipato nje ya hicho lakini kila unapojaribu kuanza unaishia njiani. Hupati matokeo mazuri na majukumu unayaona yanaingiliana. Muda unaoutumia katika biashara yako hiyo ya pembeni unakuta hautoshi na unalazimika kuingiliana na ule wa kazi yako ya msingi au biashara mama.


Ili mtu kuwa na akili iliyohamasika muda wote na uweze kutimiza majukumu yako kwa ufanisi wa kiwango cha hali ya juu, inategemea sana ni jinsi gani unavyokamilisha ratiba zako . Usitegemee baada ya kutoka kazini kwako utakuwa na hamasa ya kutosha ya kufanya kazi za kukuingizia kipato cha ziada kama huko kazini umeacha viporo vya kazi zinazokusubiri uje uzikamilishe siku ya pili au kuna kazi hukuzifanya kwa ufanisi na bosi wako amekasirika na kukufokea.


Hata kwa yule anayefanya biashara yake binafsi kuna kiasi kikubwa cha pesa anachokikosa kutokana na kutojipanga sawasawa kwenye eneo la muda, vitu mbalimbali anavyofanya na vipaumbele vyake  kwa ujumla. Ikiwa mtu wa namna hii atajipanga vizuri na kuwaepuka matapeli wa muda anaweza kupata muda zaidi wa kutosha akajenga jina la biashara yake na bila shaka yeyote kutengeneza pesa nyingi zaidi ya vile alivyokuwa akipata zamani.

Lakini wezi hawa wa muda wako ni kina nani?

........................................................

Mpenzi msomaji wa makala hii, fuatana nami kwenye group la masomo ya kila siku la MICHANGANUO-ONLINE, hili ni somo la 5 leo katika mfululizo wa masomo 30 kwa mwezi huu wa 12

Karibu ulipie kiingilio chako sh. elfu 10 upate na offa ya masomo mengine yote toka mwezi Januari, semina, vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara bunifu zinazolipa. offa hii mwisho wake ni tarehe 30 Desemba 2018.

Namba za malipo ni, 0765553030  au  0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo. Ukishalipia tuma ujumbe wa wasap au wa kawaida usemao, 'NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO'

Siyo lazima uwe unatumia wasap ndipo uweze kupokea masomo haya, tunatuma pia kwenye email kila kitu sawa na tunavyofanya katika wasap.

0 Response to "KAMATA, PELEKA JELA WEZI HAWA 3 WANAOKUIBIA MUDA WAKO USIPATE PESA NYINGI"

Post a Comment