KWANINI MIKOPO YA RIBA MITAANI, MICHEZO YA UPATU NA BAADHI YA VICOBA SI SALAMA KUJIUNGA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KWANINI MIKOPO YA RIBA MITAANI, MICHEZO YA UPATU NA BAADHI YA VICOBA SI SALAMA KUJIUNGA?


MASOMO YA MICHANGANUO YA BIASHARA KWA NJIA YA WASAP
Biashara ya kukopesha pesa ni moja kati ya biashara kongwe kabisa duniani, miaka kwa miaka binadamu wamekuwa wakiazimana pesa kwa malengo mbalimbali tofauti. Hata kabla ya fedha kuvumbuliwa watu walikuwa wakikopeshana vitu au bidhaa mbalimbali wengine wakichaji riba(chajuu) na wengine walikopeshana tu hivyohivyo pasipo kudai chochote toka kwa mkopaji, mkopaji alitakiwa kurejesha kiasi kilekile alichokopa.


Ni miaka ya hivi karibuni tu au tuseme karne chache zilizopita biashara hii ilikuja kuchukuliwa rasmi na mabenki lakini hata pamoja na hivyo bado watu mmojammoja na vikundi kama vile vya upatu, saccos na viccoba wanaendelea na biashara hii. Uzuri wa biashara hii ni kwamba mtu unaweza ukaingiza kipato pasipo kufanya kazi kubwa sana endapo utaisimamia vizuri. Biashara za kukopeshana pesa zipo za aina mbili;

·       Mikopo isiyokuwa na riba
·       Mikopo yenye riba

1.Mikopo isiyokuwa na riba
Katika aina ya kwanza ya mikopo ndiyo iliyokuwa kongwe zaidi na ipo ya aina nyingi mojawapo ni ile ambayoi hufanyika zaidi baina ya watu mitaani katika vikundi visivyokuwa rasmi maarufu kama MCHEZO, michezo ya upatu sifa yake kubwa ni kutokuwa na riba isipokuwa mingine huwa na faini pale mkopaji anapochelewesha kulipa kwa wakati.


Lengo kubwa la mtu kucheza mchezo ni ili kuweza kupata mtaji au fedha kwa ajili ya kutimiza lengo fulani na kisha fedha hizo kuja kuzirejesha taratibu, lakini pia mchezo unamsaidia mtu kujijengea nidhamu ya utunzaji wa pesa kwani anapokuwa akiwachangia wenzake ni sawa na kuweka akiba kwa ajili ya matumizi yake ya baadae.

Kwahiyo kimsingi kabisa upatu lengo lake ni zuri sana na wala halina shaka yeyote isipokuwa madhara yake ambayo ndiyo tutakayokwenda kuyajadili na kuyafahamu kinagaubaga.

2.Mikopo yenye riba
Hii ni biashara kama zilivyokuwa biashara nyingine zozote zile, ila tu bidhaa inayouzwa ni pesa ili ikatumike kutengeneza fedha zaidi. Biashara ya kukopesha fedha kwa riba hufanywa na makundi yafuatayo;

1)  Watu binafsi maarufu kama, MIKOPO YA RIBA MITAANI
2)  Vikundi vilivyosajiliwa kama vile SACCOS, VICCOBA nk.
3)  Mabenki na taasisi nyinginezo kubwakubwa za fedha.

Kabla hatujakwenda rasmi kuona NI  KWANINI MIKOPO YA RIBA MITAANI, MICHEZO YA UPATU NA BAADHI YA SACCOS NI HATARI MTU KUJIUNGA, hebu kwanza tuone mikopo inavyofanya kazi….
……………………………………...........

Mpenzi msomaji wa makala hizi, makala hii tutajifunza leo Mei 8 2020 katika Group la MICHANGANUO ONLINE na CHANNEL YA TELEGRAM saa 3 usiku mpaka saa 4 na kiingilio chake ni shilingi elfu 10 tu.

Ukishalipia tunakutumia masomo na semina zote tulizojifunza tangu mwezi January, vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara pamoja na kukuunganisha na group hilo.

Utapata pia fursa ya kujifunza semina na masomo mengine yote yajayo kila siku kwa miezi yote iliyobakia mpaka mwaka huu wa 2020 umalizike tutakapohitimisha programu ya mwaka mzima. Aidha Semina za michanganuo ya biashara zinazolipa haraka zinaanza tena wiki hii hatua kwa hatua.

Namba za malipo ni 0712202244  au 0765553030 na jina hutokea Peter Augustino Tarimo, baada ya kulipia tutumie namba unayotumia wasap au anuani yako ya email pamoja na kutuma ujumbe wa “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE NA OFFA ZOTE” kwa namba 0765553030

0 Response to "KWANINI MIKOPO YA RIBA MITAANI, MICHEZO YA UPATU NA BAADHI YA VICOBA SI SALAMA KUJIUNGA?"

Post a Comment