BADILISHA KITU KIMOJA TU KATI YA HIVI 11 KUREKEBISHA UPYA UHUSIANO WAKO NA FEDHA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BADILISHA KITU KIMOJA TU KATI YA HIVI 11 KUREKEBISHA UPYA UHUSIANO WAKO NA FEDHA.


uhusiano na fedha
Kama mtu atakuuliza ni kitu gani ambacho ungependa ukibadilishe katika maisha yako halafu pesa zisiwe tena tatizo kwako ungetaja kitu gani? Bila shaka ungeweza kumtajia kitu chochote kile hata kama ingelikuwa ni kula mmlo mmoja tu kila siku kwa miezi kadhaa.

Binadamu sisi sote ndoto zetu, tungependa kuishi maisha mazuri, kumiliki vitu vizuri, kama nyunba, magari ya kisasa, simu ya bei kubwa nk. lakini bado wengi wetu tunaishi maisha yenye mzunguko hafifu wa fedha na vikwazo lukuki katika masuala yote yahusuyo fedha, na tunaathiriwa kwa kiasi kikubwa hata na zile gharama za msingi kabisa za maisha kama vile, kodi za nyumba, chakula na ada za watoto za shule.

Ingekuwaje kama kuna tabia moja katika maisha yetu ambayo tukiibadilisha mambo yanaweza kunyooka?  Na je, ungekubali kubadilisha tabia hiyo? Wala jambo hilo halipaswi kuwa kubwa au gumu sana kulitekeleza. Mara nyingi huwa tunajiwekea malengo ambayo hatimaye tunashindwa kuyatekeleza kama tulivyodhamiria. Lakini vipi kama tunaweza kubadilika sasa na kuamua kuwa tofauti?


Katika mambo 11 yaliyotajwa, hebu amua leo kubadilisha moja tu, siyo yote ingawa huzuiwi kuyazingatia yote ikiwa utaweza. Huo unaweza ukawa ndio mwanzo wa kubadilisha kabisa uhusiano wako na fedha, kuwa mzuri zaidi kama ulikuwa mbaya.

........................................................................

Ndugu msomaji somo hili tunakwenda kujifunza leo jumapili usiku katika Group la Whatsap na email la MICHANGANUO ONLINE, Tutakuwa pia na sehemu ya pili ya sura ya 9 ya tafsiri ya kile kitabu cha THINK & GROW RICH(FIKIRI UTAJIRIKE)

Kujiunga na Group hili kiingilio ni shilingi elfu 10 na unakuwa mwanachama wa kudumu siku zote. Tunatoa pia masomo mbalimbali yote yaliyokwishapita kwenye group pamoja na vitabu na makala mbalimbali zenye mafunzo. Namba za kulipia ni 0712202244  au 0765553030 ukishalipa tuma ujumbe wa simu au whatsapp 0765553030

2 Responses to "BADILISHA KITU KIMOJA TU KATI YA HIVI 11 KUREKEBISHA UPYA UHUSIANO WAKO NA FEDHA."

  1. Mbona hua humalizii Hizi makala au

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hellow Unknown, Kuna baadhi ya makala huwa simalizii kwa sababu zinakuwa ni maalumu kwa ajili ya group la wale wanaohitaji kujifunza zaidi. Sababu ya kuziweka hapa nusu ni kwamba msomaji yule anayependa kujifunza zaidi aweze tu kupata utangulizi wa makala na kisha makala kamili anajiunga na kundi hilo kwa kiingilio kidogo sana cha shilini elfu 10 tu kwa mwaka mzima anapata na vitabu na michanganuo ya zawadi(offa)

      Aidha kuna makala nyingine nyingi ndani ya blogu ambazo huwa zinabakia kuwa kamili bila ya kuzipunguza kitu chochote, na mtu yeyote anaweza akazisoma free of charge kabisa pasipo kulipia chochote zaidi ya muda wake mwenyewe.

      Asante sana
      peter Tarimo

      Delete