HALI NGUMU NA MZUNGUKO MDOGO WA PESA, PROFESA LIPUMBA ATOBOA SIRI


Profesa akisoma ripoti ya Baraza kuu la chama cha Wananchi CUF kwa waandishi wa habari jana, aliweka wazi sababu kubwa inayochangia mzunguko wa fedha kwa wananchi kuwa mdogo na hatimaye kupelekea maisha kuwa magumu kwamba ni pamoja na malimbikizo ya madeni ya serikali. Alisema mzunguko wa pesa unapokuwa mdogo husababisha;

·       Wananchi kukosa uwezo wa kununua bidhaa na huduma mbalimbali hivyo biashara nyingi kudoda.
·       Wamiliki wa biashara kukosa uwezo wa kuwalipa wateja wanaowasambazia bidhaa na huduma.
·       Hali ya maisha kwa ujumla kuwa ngumu.

Profesa Lipumba aliongeza kwamba mikopo ya mabenki kwenye sekta binafsi katika mwaka 2017 kwa mujibu wa takwimu za Benki kuu, imepungua kwa asilimia 3.4

SOMA: Mzunguko mzuri wa fedha ndiyo njia nzuri ya kufikia malengo 2018

0 Response to "HALI NGUMU NA MZUNGUKO MDOGO WA PESA, PROFESA LIPUMBA ATOBOA SIRI"

Post a Comment