KUPANGA KABLA YA TUKIO KAMA KUNUNUA NGUO MTOTO HAJAZALIWA NI UCHURO/BALAA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUPANGA KABLA YA TUKIO KAMA KUNUNUA NGUO MTOTO HAJAZALIWA NI UCHURO/BALAA?


kununua nguo mtoto hajazaliwa ni uchuro?
Sote tumejikuta tumezaliwa katika tamaduni za ajabu, jamii nyingi za Kiafrika, suala la kupanga jambo lolote lile kabla ya siku ya tukio lenyewe maana yake ni uchuro au kujitabiria balaa kubwa. Mfano ni pale mtu anapoamua kufanya shoping ya nguo za mtoto wake kabla hajazaliwa, utasikia “huyu ana wazimu nini, atanunuaje nguo mtoto angali bado tumboni, atajuaje kama ni wa kike au ni wa kiume?”.

Matukio makubwa kama vile harusi, kuanza nasomo, kupata mtoto, kuanzisha biashara, kupunguza uzito, kujenga nyumba nk. watu wengi huogopa kufanya mipango ya maandalizi(kupanga) wakihofia eti kwa kufanya maandalizi hakusaidii kitu, kwanza ni uchuro, utajuaje kama siku yenyewe itafika ukiwa ungali hai.nk.

SOMA: Sababu kuu 5 kwanini uandae kwanza mpango wa biashara yako kabla hujaianzisha.

Kwa ujumla watu husingizia sababu nyingi zisizokuwa na msingi ili kuepuka kufanya mipango au maandalizi ya tukio na kusubiri mipango ya zima moto dakika za lala salama. Na watu wengine kwa kuogopa wataonekana wanga, wachawi ama watu wa ajabu na wenzao, hujifanya hawapangi chochote huku nyuma ya pazia wakiwa wanapanga kimyakimya mambo yao.

Ukweli ni kwamba vile vitu ambavyo watu wanadhani kuwa ni uchuro, kiuhalisia wala siyo kweli ni kinyume chake. Watakuona mtu wa ajabu ukifanya maandalizi ya kupata mchumba lakini ni maajabu zaidi kukurupuka na kwenda kuvamia mchumba usiyemfahamu vizuri kwa kutokufanya maandalizi akaja kukuletea magojwa ya ajabu au hata mtafaruku mkubwa kwenye ndoa yenu. Jamii itakuona wa ajabu sana utakapoamua kumfungulia mwanao aliyezaliwa jana tu akaunti ya akiba ya benki kwa ajili ya masomo yake ya baadae, lakini uchuro halisi wa kweli utaujua pale mwanao huyo atakapoanza shule kipindi umefilisika au kufukuzwa kazi na mfukoni hauna hata senti tano.

SOMA: Jinsi ya kuanzisha biahsra itakayodumu miaka 100 na zaidi ijayo.

Utaitwa mwendawazimu utakapoonekana ukisoma vitabu vya malezi ya watoto na afya ya uzazi kabla hata haujachumbiwa au kuchumbia, lakini uwendawazimu wa kweli ni pale utakapokuja kuzaaa watoto wako na kushindwa kuwapatia malezi bora, wengine wakageuka chokoraa, vibaka, wanaojiuza miili yao na wakabaji vichochoroni.

Utaonekana unapoteza muda wako mwingi kufikiria mpango wa biashara yako utakuwaje, lakini kupoteza muda halisi utakuja kukujua wakati biashara yako itakapokwama, kufa au kusuasua kutokana na kushindwa kuisimamia na kuiendesha vizuri kunakotokana na kukosekana kwa mpango mzuri tangu ulipokuwa ukiianzisha.

Usikubali hata kidogo kuingia katika mkumbo wa kutokupanga mambo yako mapema kabla ya tukio halisi eti kwa kuhofia kuonekana mtu wa ajabu na wale wanaokuzunguka. Watu wote wenye mafanikio ya kushangaza leo hii, walipanga kwanza mambo yao kabla hawajayafanya. Kwa mfano waliweka pesa zao akiba kabla ya kuzitumia, kuweka akiba ni aina mojawapo ya mipango kwani unajitayarisha na mambo yajayo hata kama huna uhakika nayo asilimia mia moja. Hupanga karibu kila kitu kabla ya kukifanya, vitu kama milo yao, safari zao, wanapoanzisha biashara au uwekezaji fulani, masomo, ajira, harusi, kuzaa mtoto na hata wanapofanya ujenzi wa nyumba zao.

SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongezamafanikio ya biashara yako.

Ikiwa katika jamii utaonekana upo makini sana na mipango yako tuseme labda mipango ya kibiashara, kupunguza uzito uwe na mwili wenye afya, kuongeza kipato cha ziada, au mpango wowote ule wa manufaa katika maisha yako, ukumbuke kwamba watu katika jamii hiyo wanaokuzunguka hawatajisikia vizuri na ndiyo kiini cha wao kukuona mtu wa ajabu, tayari unakuwa umeshaanza kujitofautisha na wao, unageuka kuwa kama mzimu, na wanaogopa utafanikiwa uwaache pale walipo na hivyo wanaona ni bora wakukatishe tamaa kusudi muendelee kuwa wote pamoja katika jahazi la ukosefu wa mafanikio.

Kupanga mambo yako kabla hujayatenda hukupa uhuru mkubwa. Uliwahi siku moja kuwa na safari muhimu sana kwa mfano siku uliyokuwa unakwenda mjini kwa mara ya kwanza kabisa ukitokea kijijini kwenu? au siku ya kwanza kwenda kuanza chuo, shule nk.? Unakumbuka jinsi ulivyofanya maandalizi hata usiku ule ukakesha mpaka saa 8 ya usiku ukinyoosha nguo zako kwa pasi ya mkaa? Tena basi wala hukusukumwa na mtu ulifanya mwenyewe tu automatic. Vipi ikiwa kama ungesubiria mpaka asubuhi muda unafika wa kuondoka ndipo uanze kujiuliza nguo zangu, kiatu changu, begi langu, mkoba wangu uko wapi?

Kama wewe ni wa ajabu, mtu wa uchuro wakati unapopanga masuala yako ya msingi katika kuhakikisha mustakabali mzuri wa maisha yako, basi moja kwa moja ujue kwamba wewe upo katika kundi jema, kundi la wanamafanikio.

……………………………………………………..

Ndugu msomaji wa blogu hii;
Kati ya vitu vingi nilivyokutayarishia, kitabu cha “MICHANGANUO YABIASHARA NA UJASIRIAMALI, siwezi nikakifananisha na vitu vingine vyote. Ni ndani ya kitabu hiki nilipokusanya kila kitu kuhusiana na jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara kwa mafanikio. Kummbuka Mpango wa biashara ni jinsi unavyoianza biashara mpaka mwisho wake. Mchakato wa kuandaa mpango wa biashara iwe ni kwa kichwa tu au hata kwa kutumia peni na karatasi, una thamani kubwa kushinda hata mpango wenyewe ulioandikwa.

Kitendo cha kufikiria kimkakati ndicho kinachokufanya wewe ufahamu mbinu mbalimbali utakazotumia kufanikisha biashara yako na hata ikiwa mipango itakwenda tofauti au kinyume na ulivyopanga na mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwaga, unakuwa mwepesi zaidi kutumia mbinu mbadala, ‘plan B’ kwani unakuwa tayari ulishazifikiria kichwani kitambo kabla hujaanza kutekeleza wazo la biahsra yako.

Kitabu hiki kinapatikana katika mifumo 2

1. HARDCOPY, au kitabu cha karatasi cha kawaida;
Ukiwa Dar es salaa tunakuletea mpaka pale ulipo kwa bei ya shilingi elfu 22 (22,000/=). Ukiwa mikoani, agiza mtu anayefika Dar akuchukulie au pia unaweza ukatuma shilingi elfu 30 kwa njia ya simu na sisi tukakutumia kitabu kwa njia ya basi linalofika ulipo.

2. SOFTCOPY: Kitabu kwa njia ya E-mail, ukiwa sehemu yeyote ile nje au ndani ya Tanzania, tuma shilingi elfu 10 (10,000) kwa njia ya simu ya mkononi, na sisi tutakutumia kitabu hiki mara moja bila kuchelewa.

Unaponunua kitabu hiki unaunganishwa bure na masomo ya SEMINA za michanganuo na mzunguko wa fedha kila siku kwenye Group la WHATSAPP, EMAIL NA BLOGU YA PRIVATE

Namba zetu za simu ni 0712202244  au  0765553030  jina ni Peter Augustino Tarimo. Nammba ya WHATSAPP ni 0765553030

Tupo:  MBEZI YA KIMARA KWA MSUGURI

*Uaminifu na uhakika ndiyo kipaumbele chetu kikubwa kwa mteja, kwani tunafahamu kwenye hii mitandao pia wapo watu wengi wasiokuwa waaminifu, tunatimiza kwa wakati kile tunachokiahidi bila ubabaishaji wala utapeli wa aina yeyote.



0 Response to "KUPANGA KABLA YA TUKIO KAMA KUNUNUA NGUO MTOTO HAJAZALIWA NI UCHURO/BALAA?"

Post a Comment