VITABU MUBASHARA KWENYE SIMU YAKO YA MKONONI, KOMPYUTA AU TABLET | JIFUNZE UJASIRIAMALI

VITABU MUBASHARA KWENYE SIMU YAKO YA MKONONI, KOMPYUTA AU TABLET

Teknolojia sasa mahali ilipofikia, huna haja tena ya kuhangaika huku na kule kutafuta kitabu, gazeti ama jarida zuri ulipendalo kwa ajili ya kusoma, kuna njia nyingi sasa hivi ambazo unaweza ukavipata vitu hivyo moja kwa moja katika chombo chako cha mawasiliano unachotumia, kwa lugha ya siku hizi huitwa MUBASHARA. 


Maana yake unapata kitu iwe ni kitabu, taarifa, picha au video moja kwa moja. Ingawa neno hilo ‘mubashara’ linaweza likamaanisha ‘live’ , kitu kikifanyika muda huo huo kama tukio, lakini pia kiswahili kinaruhusu kubadilisha maana ya maneno yake pale neno linapoleta mantiki nzuri, mubashara imetumika hata kumaanisha mapenzi ya kweli(mapenzi yasiyokuwa na chenga).


Moja tu ya njia hizo ni hii tunayoitumia sisi Self help books Tanzania kuwafikia wateja wa vitabu tunavyochapisha. Tunaposema “vitabu mubashara” tunamaanisha, Kitabu kinamfikia mteja moja kwa moja pale alipo, bila kikwazo cha aina eyote ile, kwa gharama nafuu kuliko kama vile angelinunua kitabu cha karatasi cha kawaida, mteja pia anakuwa na uwezo wa kukisoma kitabu hicho muda huohuo au muda wowote awapo na nafasi na inaweza ikawa hata ni ndani ya usafiri kwani kifaa kama simu ya mkononi mahali popote pale inawezekana mtu kufungua.

Mteja anahitaji kufanya vitu vifuatavyo ili kupata kitabu/vitabu mubashara katika kifaa chake cha mawasiliano, kumbuka kifaa hicho chaweza kuwa ni simu ya kisasa ya mkononi(SMARTPHONE), kompyuta ya mezani(desktop), kompyuta mpakato(laptop) au tablet.

1)  Kutuma anuani yake ya email kwa njia ya meseji katika namba, 0712202244  au  0765553030

2)  Kulipia kitabu/vitabu kupitia namba za simu, 0712202244  au  0765553030(Peter Augustino Tarimo)

3)  Tuma meseji ni kitabu kipi unachohitaji.

Baada ya kukamilsha hatua hizo 3, mteja atatumiwa kitabu kikiwa katika mfumo wa softcopy(PDF) ndani ya dakika 5-10 kupitia email yake na ataweza kukidownload(kukipakua) muda huohuo na kuanza kusoma au kukisave katika kifaa chake cha mawasiliano.

Vitabu vilivyoko sokoni kwa sasa hivi ni hivi vifuatavyo;


Tsh.  10,000/=
 



 Tsh.  5,000/=



Tsh.  3,000/=

Kwa vitabu zaidi, tembelea, SMART BOOKS TANZANIA

0 Response to "VITABU MUBASHARA KWENYE SIMU YAKO YA MKONONI, KOMPYUTA AU TABLET"

Post a Comment