UMUHIMU WA KULIGAWA SOKO LA BIASHARA YAKO KATIKA MAKUNDI/VIPANDE TOFAUTI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UMUHIMU WA KULIGAWA SOKO LA BIASHARA YAKO KATIKA MAKUNDI/VIPANDE TOFAUTI

soko lengwa
Unapoandika mpango wa biashara au hata ikiwa wewe ni mfanyabiashara tu unayetaka kufanikiwa katika biashara unayofanya, huna budi kugawa soko lako  katika vipande vipande. Kuligawa soko katika vipande tofauti maana yake ni kuwapanga wateja wako watarajiwa katika makundi tofauti tofauiti kulingana  na vigezo kama vile, umri, kipato, aina ya bidhaa wanazopendelea, maeneo (kijiografia), mahitaji ya wateja, ama mgawanyo mwingine wowote ule utakaochagua.

Kuligawa soko kutakuwezesha kulifahamu  vizuri zaidi soko lako na kukuwezesha kuelekeza  nguvu zako za matangazo na promosheni  katika lengo moja au mawili  badala  ya malengo mengi tofauti tofauti yatakayo sababisha mafanikio yawe kidogo. ‘Kumbuka mkimbia na kuku wengi hatimaye huwakosa wote’.

Pia kutakuwezesha kuwafahamu washindani pamoja na bidhaa wanazozalisha zinazofanana na za kwako hivyo utaweza kujua ni hatua zipi uchukue kuimarisha zaidi shughuli zako za kutafuta masoko na mauzo.

Kwa  mfano mtu  mwenye mgahawa eneo fulani anaweza akawagawa  wateja wake  muhimu  kama ifuatavyo;
                                                                
1)  Wenye  kipato cha chini.
2)  Wenye kipato cha kati na
3)  Wenye  kipato cha juu.
                                    
Mwenye  biashara ya kusambaza vifaa vya ujenzi anaweza akaligawa soko/ wateja wale katika makundi kama ifuatavyo;

1)  Taasisi za serikali.
2)  Makampuni  binafsi.
3)  Watu binafsi.

Mgawanyo wa soko unasaidia biashara /kampuni  kupanga malengo yake katika makundi  tofauiti  ya wateja ukizingatia  unakuwa  umefahamu  vizuri ni kundi lipi lenye wateja wengi au ni lipi  linalolipa zaidi. Katika kuchagua ni kipande/kundi gani utazingatia zaidi faida za kundi husika.Unaweza ukachagua kundi moja, mawili au zaidi. Lakini inashauriwa “kudili” na makundi machache kadiri inavyowezekana hata ikibidi kundi moja tu kwani unapoamua kulenga makundi mengi zaidi unapunguza ufanisi.


Hakikisha kama unatengeneza mpango wa biashara, unaelezea kwa chati na jedwali kila  kipande katika  mgawanyo wako kwani ndio msingi wa mikakati yako. Eleza kwa mfano ni kitu gani kinachotofautisha Taasisi za serikali na makampuni binafsi, je ni mauzo?, ni idadi ya wafanyikazi?, ni wingi  wa  bidhaa wanazonunua ama kuna kigezo kingine chochete  kile?.

Pia mgawanyo wa soko unakuwezesha kufahamu kwa uhakika zaidi washindani wako wanaolenga soko lile lile unalolenga wewe. Utapangilia vizuri  kampeni zako za  matangazo, promosheni na programu za mauzo.

Katika  kugawa soko zingatia  vigezo vinavyoleta  tofauti katika watu kununua, kuchagua vyombo vya habari utakavyotumia kutangaza na hadhi ya wateja walengwa, jiulize ikiwa vitu kama umri , elimu aina ya chakula kipato na mitindo kama  vina athari yeyote kwa wateja unaotaka kuwalenga.

Jibu litategemea aina ya biashara  unayofanya, kwa mfano nguo za mtindo fulani zitapendwa na  vijana zaidi kuliko  makundi ya watu wengine,na kuna baadhi ya migahawa huwavutia zaidi watu wenye elimu ya juu, Ni mara chache utakuta watu wenye elimu ama vipato vya chini wakiingia  sehemu kama Mlimani City, Movenpick au migahawa mingine mikubwa mjini.

Kipande cha soko lengwa.
Kipande cha soko lengwa maana yake ni kwamba katika makundi ya watu au soko uliyogawa, chagua ni kipande au kundi gani unaloona linafaa zaidi au linaendana na mikakati yako uliyojiwekea.Kundi/kipande hiki ndicho utakachozingatia zaidi kukihudumia ili kikuingizie faida zaidi.


Elezea ni  kwa nini biashara yako inalenga kundi/makundi hayo ya wateja (soko),  ni kitu gani kinachoyafanya yakuvutie kushinda makundi mengineyo?. Unapogawanya soko  lako katika  vipande vipande unatakiwa  ufanye hivyo ki-mkakati, kwa mfano, muuza  nguo za fasheni anaweza kulenga  kundi la wenye kipato  cha juu kwani anajua  wanapenda vitu vyenye majina makubwa na vya bei ya juu.

………………………………………………………….........

Mpenzi msomaji wa makala hii, ikiwa unataka kujua kwa kina jinsi ya kuandaa mpango wa biashara yeyote ile jiunge na semina inayoendelea sasa katika BLOGU YA MICHANGANUO, ni blogu (private) unayoingia tu kama umeshalipa kiingilio chako sh. elfu 10. Ndani ya semina hiyo utapata mambo mengi yakiwamo,

·       Masomo 11 ya jinsi ya kuandaa mpango wa biashara katika fomati za PDF na MP3

·       Templates au vielezo kwa ajili ya kurahisisha kazi ya kuandika mpango wa biashara kwa lugha za kiswahili na kiingereza.

·       Mpango wa biashara ukurasa mmoja, hii ni staili au mtindo wa kuandika mpango wa biashara mfupi na uliokuwa rahisi sana ikiwa huna muda wa kutosha kuandika mpango mrefu.

·       Mifano halisi ya michanganuo ya biashara kwa kiswahili na kwa kiingereza.

·       Michanganuo halisi mbalimbali ukiwemo wa kuku wa mayai, saluni ya kiume na mingineyo.

·       Vitabu 2 vya jinsi ya kuandika mpango wa biashara, vya kiswahili na kiingereza(The very best books on business planning ever)

Jiunge sasa kwa kulipa kiingilio chako sh. elfu 10 tu kupitia namba za simu 0712202244  au  0765553030, jina ni Peter Augustino, tuma na anuani yako ya e-mail(GMAIL lakini) kwa meseji, kisha utapata email yenye masomo pamoja na link ya BLOGU YAMASOMO YA SEMINA hiyo.



0 Response to "UMUHIMU WA KULIGAWA SOKO LA BIASHARA YAKO KATIKA MAKUNDI/VIPANDE TOFAUTI"

Post a Comment