BORA KIPI? KUJIUNGA KATIKA MITANDAO MINGI YA KIJAMII AU MTANDAO MMOJA TU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BORA KIPI? KUJIUNGA KATIKA MITANDAO MINGI YA KIJAMII AU MTANDAO MMOJA TU


Ukisoma kitabu, MIFEREJI 7 YA PESA, unaweza kunielewa kwa urahisi zaidi kile ninachotaka kuandika hapa. Umuhimu wa MALENGO katika maisha ya binadamu ya kila siku kuanzia maisha yake, kazi, ajira, biashara , masomo, na hata mahusiano yake na Mwenyezi Mungu aliyemuumba.


Katika kutimiza majukumu yake ya kila siku binadamu hujikuta amezungukwa na vitu vingi, vitu hivyo vyote kila kimoja humvutia kukifanya lakini muda na rasilimali haviwezi kumruhusu kuvifanya vyyote kwa wakati mmoja. Mtu anapojaribu kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja basi mara nyingi hujikuta ufanisi unakuwa mdogo na mambo hayaendi vizuri jinsi alivyotarajia.

SOMA: Tayari malengo yako ya mwaka 2017 ulishayaandika mahali?

Mfano mzuri na ambao nimelenga kuuzungumzia leo ni hii mitandao ya kijamii kama vile, facebook, blogs twitter, instagram na mingineyo mingi. Kuihudumia mitandao hii nikiwa na maana ya kuweka vitu au kupost picha, makala, habari nk. kunahitaji muda na hata wakati mwingine gharama za pesa kama vile kuweka bando katika simu au line ya moderm. Gharama hizi hasahasa muda ndiyo kikwazo kikubwa mno kwa mtu kuweza kushiriki kikamilifu katika zaidi ya mtandao mmoja au miwili.

Hata unaweza kufanya uchunguzi kidogo tu kwa watu mbalimba wamiliki na wanaoendesha mitandao hii. Ukiona mtu anafanya vizuri sana kwenye mtandao mmoja, tuseme labda facebook basi na ujue katika mitandao mingine siyo rahisi nako aweze kushiriki tena kikamilifu. Au unaweza ukakuta mtu anaendesha blogu na wakati huo huo yupo katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Akitaka kwenye blogu afanye vizuri sana basi ni lazima tu katika mitandao mingine apunguze nguvu aidha kwa kuweka vitu vichache au kwa kuposti huko mara chache zaidi ya kwenye blogu, isipokuwa tu labda iwe anazo raslimali au watu anaowalipa wa kumuendeshea blogu au mitandao hiyo.

SASA BORA KIPI?
Itategemea zaidi na malengo yako ya kujiunga na hiyo mitandao ya kijamii, wengine hujiunga nayo kwa malengo ya kutangaza biashara au shughuli zao wanazozifanya, wengine kwa malengo tu ya kijamii kama vile kuwasiliana na kuwa karibu na marafiki, ndugu na jamaa, na hata wengine huingia mitandao hiyo kwa lengo la kupata umaarufu. Haijalishi mtu ameingia katika mtandao kwa lengo lipi, lengo la kila mtu ni kupata wafuasi au wanaotembelea kurasa zake wengi kadiri inavyowezekana.

SOMA: Hatua 5 za kufuta ili umiliki website yako mwenyewe.

Kwa mfano labda wewe lengo lako ni kutangaza zaidi biashara yako, kuwa katika mitandao mingi ya kijamii na tofauti tofauti ni jambo zuri sana na linaloweza kukuletea wateja wengi lakini tatizo lipo ni kwa vipi utakavyoweza kupata wafuasi wengi katika page zako hizo nyingi, facebook, insta, twitter, blogu nk. Kumbuka ili kuwa na wafuasi wengi kazi yake siyo ndogo na huchukua muda pia. Kujiunga tu hamna shida, unaweza ukawa na akaunti hata ishirini, hamna atakayekuzuia. Ugumu upo kwenye, wafuasi au wasomaji na watazamaji utawapata vipi?

Kwa maoni yangu binafsi, mimi nafikiri dawa ni kustiki kwenye mtandao mmoja au miwili ambayo utaihudumia kwa nguvu zako zote kuhakikisha ndiyo zitakazokuletea wafuasi wengi na mwishowe wateja wengi kwenye biashara yako. Nikisema mitandao ya kijamii namaanisha, yote, blogu, website, pamoja na mitandao yenyewe ya kijamii kama facebook nk. kwani vyote kila kimoja ni website au tovuti(mtandao)

Kuna watu kwamfano hutumia facebook tu peke yake kutangaza biashara zao na wala hawana hata haja na blogu sijui tovuti wala twitter lakini huhakikisha haipiti siku hawajaposti kitu facebook. Matokeo yake huwa na wafuasi wengi sana jambo linalowaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuuza bidhaa au huduma zao.

Mwingine yeye anaweza kuwa na blogu tu peke yake ambayo nguvu zake nyingi na muda humalizia humo. Ingawa blogs na tovuti mara nyingi utakuta zinaunganishwa na mitandao mingine ya kijamii kwa lengo la kvuta zaidi wafuasi, lakini utakuta kile kinachowekwa kwenye blogu ndicho hicho hicho huwekwa katika mitandao hiyo ya kijamii mingine. Mtu ni vigumu sana kuweka material original katika kila mtandao au page anayomiliki.

Ukiachilia mbali wale mablogger wanaondesha blogs zao kwa kukopi au kulink articles za mablogger wengine, si wenye blogu wengi waliokuwa na uwezo wa kuandika makala(articles) mpya na original kila siku, kwa wastani makala moja inaweza ikachukua hata masaa mawili mpaka sita kutegemeana na ukubwa wake tangu utafiti, kuanza kuiandika mpaka kuipost.

SOMA:Gundua siri ya kufanikisha biashara yako.

Na hii hasa ni kwenye blogu lakini katika mitandao mingine kwa mfano facebook, post zake zinaweza zisiwe ndefu sana kwani namna zinavyofanya kazi kuvutia wateja wengi ni tofauti na blogu, blogu zinategemea zaidi maneno muafaka(keywords)  wakati facebook yenyewe hutegemea zaidi ni wafuasi wangapi uliokuwa nao na mvuto wakile unachoandika au kupost kwa wafuasi hao.

Unapochagua jukwaa moja au majukwaa machache kwa ajili ya kampeni yako ya kwenye mtandao haimaanishi kwamba majukwaa au mitandao mingine ya kijamii hauwezi kushiriki kabisa hapana. Inawezekana kama nilivyotangulia kusema hata ukawa na account hata ishirini za mitandao ya kijamii mbalimbali lakini mkazo na nguvu zako ukazielekezea kwenye mitandao au majukwaa mawili tu au hata moja. Watu wengi wakakufahamu kupitia majukwaa hayo.

Lakini pia inawezekana ikiwa wewe unazo rasilimali au uwezo kifedha wa kuweza kuwalipa watu au hata kuwa na washirika ambao mnafanya kazi kwa ushirikiano fulani basi unaweza ukawa na majukwa mengi na ukamudu kuweka humo vitu kila siku kwa usaidizi wa hao watu.

Dunia ya leo inavyobadilika kwa kasi kubwa siyo rahisi tena umkute mtu hana ukurasa hata mmoja kwenye hii mitandao ya kijamii, hivi karibuni siyo ajabu ukaja kukuta mitandao hii ndiyo inageuka njia kuu ya kufanya mambo mengi yakiwemo manunuzi, biashara mpaka hata matibabu kama ripipoti kamili ya makala hiyo ya mabadiliko ya kasi ya dunia inavyoeleza.

SOMA: 2017 ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena.

Umejiandaa andaaje na mabadiliko hayo? Chukua hatua kuanzia sasa usijekujuta hapo baadae. Miliki hata ka ukurasa ka facebook kanatosha kukuingiza katika behewa la treni hiyo ya mabadiliko ya kasi ya dunia ya leo.


……………………………………………………………………… ..

MAFUNZO KWA VITENDO
JE,
Ungependa kuwa na blogu yako lakini huna maarifa au utaalamu wa kuianzisha?

Una wazo la kuanzisha biashara ya kwenye mtandao lakini hujui uanzie wapi?

Tayari unayo blogu lakini ungependa kuiboresha kusudi upate wateja na followers zaidi?

Una kipaji cha kuandika na ungependa kufahamu njia rahisi kabisa ya kuwafikia wasomaji wako?

TUNALO JIBU LA MASWALI YAKO
Tunatoa huduma ya kufundisha kwa vitendo jinsi ya kuanzisha blogu, vitu vyote muhimu vya kuweka ili ifanye kazi vizuri pamoja na jinsi ya kuifanya ipate watembeleaji wengi.

Utauliza au kutaka uelekezwe kitu chochote kile kinachohusiana na blogging na mitandao mingine ya kijamii pamoja na jinsi unavyoweza kutengeneza pesa kupitia blogu yako hiyo siku chache baada ya kuanzisha.

Unafundishwa peke yako kwa vitendo hatua kwa hatua na kuendelea kupewa support hata baada ya mafunzo mpaka blogu yako iwe na watembeleaji wa kutosha.


Ni muhimu uwe na vitu vifuatavyo kama utapenda mafunzo haya;

1. Chagua kabisa eneo unalopendelea kuandika(Your niche) kwa mfano kama wewe unapendelea maswala ya biashara na ujasiriamali basi blogu yako ni vizuri ihusu mambo hayo zaidi, kama ni habari basi iwe ni habari zaidi nk.

2. VIFAA
Ijapokuwa mafunzo utapewa kupitia vifaa vyetu wenyewe katika eneo letu, lakini ni vizuri pia ukawa na vifaa vyako mwenyewe nyumbani au unakoishi kwa ajili ya kwenda kufanyia mazoezi pamoja na kufanyia kazi baada ya mafunzo kwani haiwezekani kufanya biashara ya kwenye mitandao ikiwa hauna vifaa unavyomiliki mwenyewe.

Vifaa muhimu unavyohitaji kuwa navyo ni;
1. Kompyuta ya mezani au Laptop, hii ni lazima kwani simu ya mkononi ni vigumu kuandika makala ndefu.

2. Moderm au kifaa cha kukuunganisha na Intaneti, nacho ni lazima kwa ajili ya mtandao wa intaneti.

Gharama ya mafunzo ni Tsh. 30,000/=, elfu thelathini tu.


TUPO MBEZI KWA MSUGURI JIRANI NA STENDI

SIMU: 0712 202244   AU   0765 553030

0 Response to "BORA KIPI? KUJIUNGA KATIKA MITANDAO MINGI YA KIJAMII AU MTANDAO MMOJA TU"

Post a Comment