MCHANGANUO WA BIASHARA: KUANZISHA SHULE YA CHEKECHEA(DAY CARE CENTRE) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MCHANGANUO WA BIASHARA: KUANZISHA SHULE YA CHEKECHEA(DAY CARE CENTRE)

Sera ya utoaji wa Elimu Tanzania inayoendeshwa chini ya Wizara ya Elimu inazitaka shule zote kutoka mikoa yote ya Tanzania kutoa elimu bora kwa watoto wote kuanzia shule za chekechea au kwa jina lingine shule za awali, shule za msingi, shule za sekondari mpaka vyuo vikuu.

Kwa kuzingatia kwamba miaka ya awali ya mtoto yeyote yule ni muhimu mno katika ukuaji wake kiakili na hata katika nyanja zingine zote, Serikali ya Tanzania iliamua kuweka mfumo wa elimu ujulikanao kama, 2-7-4-2-3+ ambao unajumuisha, miaka 2 ya awali(Kindergarten) au maarufu kama chekechea. Mtoto huanza chekechea akiwa na umri kati ya miaka 4-6.
Elimu ni ufunguo wa maisha,
Miaka saba 7 ni kwa ajili ya shule ya msingi “Primary School Education”. Miaka 4 ni Elimu ya Sekondari, kidato cha kwanza hadi cha nne 4 “Ordinary Level”, ngazi hii mtoto hujiunga baada ya matokeo ya la saba kutoka. Miaka 2 mtoto husoma elimu ya sekondari ya juu(Advanced Level ‘A Level”) ambapo hujiunga na ngazi hiyo baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka, ambapo huangaliwa ufaulu katika matokeo ya Baraza la Mitihani Tanzania “NECTA”

Miaka 3 na kuendelea ya mwisho huwa ni kwa ajili ya kusoma vyuo vikuu au vyuo vingine na taasisi za ufundi. Hapa ndipo utakutana na vitu kama, Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu, Mikopo ya elimu ya juu na hata Bima ya afya.

Lakini yote kwa yote kila kitu kinaanzia pale chekechea ingawaje shule za chekechea, walimu wa chekeche na hata vyuo vya kufundisha ualimu wa chekechea bado havijapewa uzito na umuhimu unaostahili. Mfumo wa Elimu ya Tanzania una uhusiano mkubwa sana na mfumo wa ajira Tanzania. Ajira Tanzania huwezi ukailinganisha na ile ya wenzetu kama Kenya, Uganda na hata Zambia.

Sababu kubwa ni kwamba wenzetu hao majirani wameweka msisitizo na umakini mkubwa zaidi katika elimu ya watoto wao ya nursery(chekechea) hasahasa katika upande wa lugha, simaanishi kwamba kiingereza ni bora kushinda kiswahili, la hasha, ila pointi yangu hapa ni “consistence” au kwa maneno mengine msisitizo katika lugha moja kwanza kuepusha kuwachanganya watoto katika hatua hizi muhimu za awali.
Elimu nzuri huchangia Mafanikio ya maisha. 
Mwanafunzi hujenga tabia ya kujiamini na kuwa na fursa nzuri zaidi ya kuajiriwa endapo atakuwa mahiri katika ile lugha atakayokuwa anakwenda kuitumia kwenye ajira. Sisi Watanzania tuliokuwa wengi ni “uvuguvugu”. Kwenye kiingereza hatupo na wala kwenye kiswahili pia hatumo vizuri. Na hii ndiyo sababu kubwa inayotufanya tukose kujiamini(lose confidence) mbele ya majirani zetu Wakenya na wengineo, tunabakia kuwa “less competent” linapokuja suala la ajira kimataifa. Yoote haya huanzia vidudu(chekechea).

Ndiyo maana siku hizi kuanzisha shule bora ya chekechea Tanzania kunatafsiriwa na wengi kuwa ni lazima shule hiyo iwe ni “English Medium”, yenye kufundisha `kwa lugha ya Kiingereza. Watu tunasahau kwamba ili mtoto aweze kuwa na uelewa mzuri wa masomo yake kuna vitu vingi vya kuzingatia mfano, nguo za watoto, chakula cha watoto, ratiba nzuri ya chakula, michezo ya watoto nk.

Hata matokeo mazuri kidato cha nne 4, yale ya darasa la saba 7, kidato cha sita 6(form six), vyuo na hata vyuo vikuu yanategemea sana ni jinsi gani mtoto alivyowekewa msingi imara tangu alipokuwa darasa lake la awali(nursery school).

SOMA: Maktaba ya vitabu inayotembea mashuleni.

Hapa chini kuna muhtasari wa Mchanganuo/mpango wa biashara ya uanzishaji wa shule ya chekechea(Day Care Centre) au wengine hupenda kuiita “Nursery”

Huo ni ufupisho wa mpango mzima, unaweza ukausoma wote kwenye kitabu cha “MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI”. Ndani ya kitabu hicho cha kurasa 410 kuna michanganuo mingine halisi ya biashara mbalimbali zinazolipa unazoweza ukaanzisha hapa Tanzania. Michanganuo meandikwa kiubunifu kuchochea mtu kuwa mbunifu na hata unaweza ukaitumia michanganuo hiyo kama ramani wakati ukiandika mchanganuo wa biashara yako yeyote ile.

Hata kama hauna “interest” ya kuandika mpango wa biashara , lakini kwa kuisoma michanganuo hiyo peke yake unapanuka kimawazo juu ya biashara mbalimbali na kupata ‘triki’ nyingi ambazo pengine ulikuwa bado haujazigundua.

SOMA: Kwanini uandike mchanganuo wa biashara yako kabla ya kuanza biashara yenyewe.

Vitabu vya Michanganuo na Ujasiriamali vipo, na unaweza ukapata nakala yako kwa kuwasiliana na mimi kupitia namba, 0712 202244 au 0765 553030  kisha utaletewa kitabu chako mpaka pale ulipo kama wewe unaishi Dar es salaam . Malipo yanafanyika ukishapokea kitabu na Bei ya kitabu kimoja ni TSH. 20,000/-, elfu ishirini tu.

Kama upo Mikoani pia wasiliana na sisi kwa namba hapo juu, kisha baada ya kulipa fedha sh. 20,000/= pamoja na gharama ya usafirishaji, tunakutumia kitabu kupitia mabasi yanayokwenda mikoani kutokea Dar. Vitabu ni vya kawaida vya karatasi.

Ikiwa utataka kitabu kwa e-mail(Softcopy)PDF bei huwa inapungua na ni shilingi 10,000/= elfu kumi tu kwa kitabu kimoja.

…………………………………………………………………….........

Mpango wa Biashara ya Shule ya Chekechea, shule ya awali.
(Jinsi ya Kuanzisha Shule ya Vidudu, Nasari)


SHULE YA CHEKECHEA.
Cheichei Day Care centre.


MUHTASARI.
Cheichei  Day Care ni Kituo  kitakachokuwa  kikijihusisha  na uangalizi  na ufundishaji wa watoto wenye umri kuanzia   mika 3 hadi mitano. Kutokana na mfumo wa maisha siku hizi kubadilika tofauti na miaka  iliyopita, familia nyingi hasa hasa maeneo ya mijini baba na mama wote utakuta wanafanya kazi hivyo kuwa vigumu kukaa na watoto wao wadogo wakiwaangalia kuanzia asubuhi mpaka jioni. Cheichei  watalenga familia za namna hii.

Katika miaka mitatu ya mwanzo  Cheichei wamejiwekea malengo yafuatayo-
(i)   Kuhakikisha wazazi wote wa watoto watakaowaangalia kituoni  wanafanya kazi zao mchana kutwa huku wakiwa hawana wasiwasi juu ya usalama wa watoto wao.
(ii)         Kupokea watoto wapatao 20 katika  mwaka wa kwanza  na kuongezeka kila mwaka kwa asilimia 50%.

Kituo kitamilikiwa kwa ubia kati ya Bibi Joys Komba na Mama Teresia Nduguru ambao wote ni waalimu wastaafu wa shule za msingi wenye uzoefu  wa kutosha katika shughuli  za ufundishaji  na uangalizizi wa  watoto.
Jumla ya mahitaji yote  ya kuanzia  biashara ni shilingi milioni 20, vifaa, gharama mbalimbali  pamoja na fedha za akiba.

1.1      Dhamira kuu.
Dhamira kuu ya Cheichei Day Care ni kutoa uangalizi  wa hali ya juu pamoja na  mafuzo bora kwa watoto ambao wazazi au mzazi huwa kazini  nyakati za mchana. Wazazi hao hufanya kazi zao kwa kujiamini  huku wakijua  watoto wao wapo salama  kwa asilimia mia moja.

1.2      Malengo.
Katika miaka mitatu ya  mwanzo Cheichei  kitakuwa na malengo  yafutayo;
·     Kutoa uangalizi  na mafunzo kwa watoto yenye  ubora wa hali ya juu, huku wazazi wao wakifanya kazi zao pasipo kuwa na wasiwasi juu ya usalama wa watoto wao.
·  Kuhakikisha  ndani ya mwaka wa kwanza wanapata watoto wapatao 20.
·        Kuongeza idadi ya watoto kila mwaka kwa asilimia 50%
·  Kutoa malipo mazuri kwa wafanyakazi wao wote pamoja na gawio zuri kwa wamiliki kila mwaka.



16 Responses to "MCHANGANUO WA BIASHARA: KUANZISHA SHULE YA CHEKECHEA(DAY CARE CENTRE)"

  1. Nawezaje kupata soft copy ya mchanganuo huu wa kuanzisha shule ya awali? WhatsApp 0754947671

    ReplyDelete
  2. Naomba soft copy ya mchanganuo was daycare

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaweza kupata upo, tuwasiliane namba zangu ni 0712202244 au 0765553030

      Delete
  3. Naomba soft copy ya mchanganuo wa day care

    ReplyDelete
  4. Duuu muda Muafaka Sana je naweza kupata soft copy ya mchanganuo wa kuanzisha day care na namna ya kusajili,? E-mail yangu ni moshiro getrude @gmail. Com

    ReplyDelete
  5. Nashukuru Sana! Nahitaji mchanganuo pia napenda kufahamu jinsi ya kusajiri kituo. 0686 061 829

    ReplyDelete
  6. Tafadhari naomba nakala ya mchanganuo huu wa Day Care Center email.fredkatulanda@gmail.com

    ReplyDelete
  7. Mkuu naomba mchanganuo wa biashara ya shule 0865399321

    ReplyDelete
  8. Naomba kupata Mchanganuo 0756323474

    ReplyDelete