GUNDUA SIRI YA KUFANIKISHA BIASHARA YAKO SASA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

GUNDUA SIRI YA KUFANIKISHA BIASHARA YAKO SASA

Kama mwanzo wa makala ya hivi punde ya African Dream,mwanabiashara Mercy Kitomari-ambaye alianzisha kampuni ya kutengeza aiskrimu hai ya Nelwa's Gelato-anaeleza mbinu kumi bora anazotumia katika kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa wanabiashara chipukizi:

Anza na Lengo.
Kwanini uko kwenye mitandao ya kijamii? ana nadi
Kuna majibu matatu pekee yanayokubalika: a)kuongeza kujulikana kwa bidhaa zako kwa kufikia watu zaidi b)kujenga imani ya wateja kwa kuwapa usaidizi zaidi ama c)kuongeza mauzo kwa kutafuta wanunuzi zaidi,watakaonunua mara kwa kwa mara.Usianze kama huwezi jibu swali hili.

Wapuuze wapinzani wako-
Kujaribu kuiba wateja wa watu wengine ni mbinu mbovu.Utaanza kuunda maamuzi mabaya kwa sababu unajaribu kuwafikia.
Fikra na kampeni bora zaidi bado hazijatendeka katika sekta yako.Angalia nafasi ambazo hazijaguzwa unazoweza kupata na kutumia.Tazama kile watu wanafanya kwenye sekta tofauti na ujaribu mbinu hizo.

Usiwe kwenye mitandao yote ya kijamii.
Usimamizi wa kijamii utamaliza rasilmali zako zote.Kila mtandao wa kijamii unaosimamia utakugharimu muda,pesa na nguvu zaidi,kwa hivyo amua zile utazipa kipao mbele.

Una pesa na wakati wa kutosha.
Watu huwa wanasema kuwa hawana muda na pesa za kuwekeza katika mitandao ya kijamii.Lakini ukweli wa mambo ni kuwa hauwezi kutowekeza.Kama hauna fedha za kutosha,inafaa uwe na wakati zaidi wa kuunda maudhui ama kuunda mtandao.
Mercy Kitomari ana mkahawa wa Nelwa's Gelato mjini Dar es Salaam inayosambaza kwenye hoteli na biashara zingine.

Weka lengo rahisi-
Kwa mfano,kuchapisha mara mbili zaidi kila wiki-ama kufikia bloga mmoja kwa siku.Pia fanya ukaguzi wa ndani kujua jinsi unavyotumia muda wako kwa sasa.
Mitandao ya kijamii ni bora,lakini watu wengi huchanganya kushikika na kazi na kuwa na ufanisi.Tambua shughuli zinazoleta ''mapato kutoka kwa uwekezaji'' ya juu zaidi,zipe kipao mbele na uweke mipaka.
Kuwa na nidhamu na kuwajibika kwa wengine.
Mwishowe,utahitajika kuchukua msimamo mgumu.Utahitaji kugawanya rasilmali zako chache na kuchagua kile utakachofanya (na kile utakachopuuza).Lakini utaona kuwa uamuzi huu ni rahisi kama una lengo.Matumizi yako ya mitandao ya kijamii yatakuwa na kusudi.Utapata kuwa una wakati wa kutosha wa kuitumia kimkakati.

Tambua kile kinachohamasisha wasikilizaji wako.
''Sekta'' ama ''biashara'' hazichoshi-watu wanaosema hayo ndio wanaochosha.Jinsi unavyojenga mawazo ya maudhui ya blogi ni kuelewa wasikilizaji wako na faida ambazo bidhaa na huduma zako zinawapa.
Mercy Kitomari anasema kuwa huduma ya wateja ni muhimu sana kwenye mitandao sawia na ya uso kwa uso.

Kuwa na sauti.
Watu hawapendi kuungana na mashirika yasiyokuwa na uso.Wanataka kuungana na wanadamu wa kweli.Hakuna atakayiependa,amini ama kuheshimu kampuni yako ikiwa hawezi kupata majibu yaliyo sawa na yenye uaminifu kwa wakati ufaao.Mitandao ya kijamii ni zaidi ya ''kujiingiza katika mazungumzo''.Ni njia mpya ya kufanya mambo,na vifaa kadhaa vipya kukusaidia kufanya hivo.
Lakini misingi ya njia za mauzo inabakia.Unahitaji kuvutia watu,kujenga imani yao na kuwawezesha kushiriki zaidi.

Tamba sana kupia Facebook na Twitter.
Mitandao ya kijamii na mauzo kwenye mtandao inaanza na DNA yako,bidhaa ama huduma zako,na watu wako.Kwa hivyo kama unataka kuimarisha majibu yako kwenye mitandao ya kijamii,anda na kushughulikia utenda kazi wa ndani wa kampuni yako.


CHANZO: BBC


1 Response to "GUNDUA SIRI YA KUFANIKISHA BIASHARA YAKO SASA"

  1. Niko mbioni kufungua biashara ya duka la bidhaa za nyumbani maarufu kama duka la mangi, najitahidi sana kusoma makala zako na hata za waandishi wengine kujifunza ni namna gani nitaifanya biashara yangu inipe mafanikio makubwa

    ReplyDelete