Idadi hiyo ya wanafunzi
watakaojiunga katika shule za Serikali mwaka huu, imeongezeka kutoka 33,683
mwaka jana hadi kufikia 54, 085 sawa na asilimia 75.6 ya wanafunzi 71,527 wenye
sifa ya kujiunga na kidato cha tano Tanzania Bara.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa
alisema kati ya waliochaguliwa wavulana ni 31,352 na wasichana ni 22, 733.
“Wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha tano 2014 ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Kati yao wavulana 14, 826 sawa na asilimia 27.41 wamechaguliwa kusoma masomo ya
sayansi na wengine 16, 526 sawa na asilimia 30.5 wamechaguliwa kusoma masomo ya
sayansi ya jamii,” alisema.
Alisema wasichana 7,859 sawa
na asilimia 14.5 wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi na wengine 14, 874 sawa
na asilimia 27.5 watajiunga na masomo ya sayansi ya jamii.
“Wanafunzi hao wamechaguliwa
kujiunga kidato cha tano katika shule 241 zikiwamo 33 zilizopangiwa wanafunzi
kwa mara ya kwanza mwaka huu,” alisema.
Mbali ya wanafunzi hao
wanaojiunga kidato cha tano, Majaliwa alisema wengine 472 watajiunga na vyuo
mbalimbali vya ufundi.
Alisema waliochaguliwa
wanatakiwa kuripoti katika shule husika kuanzia Julai 10 na kwamba watatakiwa
kufanya hivyo ndani ya siku 20 vinginevyo nafasi zao zitachukuliwa.
Kuhusu robo ya wanafunzi ambao
walifaulu lakini hawakuchaguliwa, Majaliwa alisema hiyo ilitokana na ufinyu wa
nafasi za shule na kukosa tahasusi (combination).
“Wanafunzi 16,800 wakiwamo
watahiniwa wa kujitegemea 10 waliokuwa na sifa za msingi hawakuchaguliwa.
Waliokosa kuchaguliwa kwa sababu ya ufinyu wa nafasi ni wanafunzi 16, 400 na
wale kutokana na combination ni 400,” alisema.
Kuhusu wanaojiunga na vyuo vya
ufundi, Majaliwa alisema idadi yao imepungua kutoka 530 mwaka jana hadi 472
mwaka huu kutokana na vyuo hivyo kuanza kudahili wanafunzi wa shahada ya
kwanza.
Alisema kati ya hao
waliochaguliwa, wavulana ni 355 na wasichana ni 117 na kwamba idadi ya
wasichana imeongezeka kwa wanafunzi watatu kutoka 114 mwaka jana sawa na
asilimia 2.63.
“Serikali inatarajia kufanya uchaguzi wa awamu ya pili baada ya kubaini
nafasi zitakazokuwa wazi zinazotokana na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya
kwanza na imeweka utaratibu wa kuwapatia nafasi ya kusoma kidato cha tano na
cha sita pamoja na stashahada ya elimu wanafunzi wenye sifa,” alisema.
CHANZO MWANANCHI
0 Response to "FORM FOUR WALIOSHINDA MTIHANI MWAKA HUU: WENGI WACHAGULIWA KIDATO CHA TANO "
Post a Comment