DIAMOND PLATNUMZ:KABLA SIJAFANYA COLLABO NA DAVIDO NYIMBO ZANGU ZILIKUWA MWISHO CHALINZE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

DIAMOND PLATNUMZ:KABLA SIJAFANYA COLLABO NA DAVIDO NYIMBO ZANGU ZILIKUWA MWISHO CHALINZE


Diamond Platmumz akifanya mahojiano leo hii usiku na kituo cha redio cha Times Fm amesema kwamba yeye wakati alipokuwa akienda kufanya collabo (ushirikiano) ile nyimbo ya “My number one” hakuwa anafahamika Kimataifa. “Watu waliongea mengi sana lakini lakini hawakujua fikra zangu zilikuwa nini, lakini ile nyimbo ndiyo iliyopita na kuniingiza MTV….ile nyimbo……”

DIAMOND PLATNUMZ
Alisema muziki sasa hivi ni biashara, ni lazima watu waangalie na kuhakikisha wanashirikiana kusudi waweze kupata mafanikio badala ya kuanza kushindana “Tuache mawazo ya kukomoana wenyewe kwa wenyewe” alisema Diamond. Ili kutengeneza pesa nyingi alishauri wasanii wawe na tabia ya kufocus/kulenga mbele na kukufikiria nje ya Tanzania na Afrika Mashariki mpaka Afrika nzima na Dunia kwa ujumla.

Kuhuiana na madai kuwa anaringa kadiri anavyopata mafanikio alikanusha na kusema kuwa yeye amekuwa akiwasaisia watu wengi tu na wale wanaompaka matope ni wachache ambao wanajidai wanamjua sana na kutaka ‘kumcontrol’. Amesema hadi leo hii anatenga muda na hata kukiwa na shughuli mbalimbali kama msiba au sherehe mitaa yake ya zamani uswahilini Tandale bado huwa anakwenda kujichanganya na watu na wala hawafanyii unyanyapaa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Zaidi ya yote MKALI Diamond ametanabahisha kwamba “mission” yake kubwa ni kuimba katika lugha ya kiingereza kwa baadhi ya nyimbo zake kwani moja ya sababu zilizomkosesha tuzo ni pamoja na kutokuimba katika lugha inayojulikana kimataifa, alisema wasanii wa kinaigeria wana advantage kubwa kwa kuimba kwa kiingereza lakini pia akasema siyo lazima sana kuimba katika lugha ya kiingereza ili kufanikiwa kwani midundo nayo ni kigezo, mfano kuna wasanii Nigeria japo hawaimbi kwa kiingereza  lkakini kwa kuwa nyimb zao zinachezeka basi wameweza kupata tuzo. Lakini anadai Watanzania wanapenda zaidi miziki yenye hadithi za kimapenzi, “fulani kamuacha fulani, ukienda kuimba ukilalamika mapenzi huko nje watu hawatakuelewa kabsa, wanataka muziki unaochezeka”

Msikilize mwenyewe Diamond hapa chini akifanya mahojiano na Kituocha redio cha TIMES FM.


0 Response to "DIAMOND PLATNUMZ:KABLA SIJAFANYA COLLABO NA DAVIDO NYIMBO ZANGU ZILIKUWA MWISHO CHALINZE "

Post a Comment