UNGEPENDA NAFASI YA AJIRA/KAZI SERIKALINI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UNGEPENDA NAFASI YA AJIRA/KAZI SERIKALINI?

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania  wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.
Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii  na Afisa vipimo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo za kazi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.

Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misenyi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukoba, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.

Nafasi hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Nzega, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ushetu.

Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya Songea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyang`wale, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ukerewe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Geita na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu. Kwa maelekezo zaidi tembelea hapa katika tovuti ya serikali ya ajira

0 Response to "UNGEPENDA NAFASI YA AJIRA/KAZI SERIKALINI?"

Post a Comment