NA HII VIDEO YA TUBONGE YA JOSE CHAMELIONE KANISANI UMESHAIANGALIA? NI BONGE LA VIDEO ICHEKI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NA HII VIDEO YA TUBONGE YA JOSE CHAMELIONE KANISANI UMESHAIANGALIA? NI BONGE LA VIDEO ICHEKI



Download video ya wimbo wa Jose Chamelione alio 'act' akiwa ndani ya kanisa katoliki, uione na uisikilize kwa makini utagundua kweli Mganda huyu anaimba. Si kama namsifia au kumpigia debe la hasha, ila mimi binafsi tu naipenda sana staili ya nyimbo zake na ubunifu anaotumia katika video hizo. Ujasiriamali ndivyo unavyotaka katika nyanja zote iwe ni katika muziki, sanaa, na hata michezo ya aina mbalimbali kama mpira wa miguu(soka) au kuigiza filamu.

Hata hapa kwetu Tanzania siku hizi vijana wetu wanakuja juu sana, waangalie wasanii na wanamuziki wa kizazi kipya kama vile kina, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, mrembo Wema Sepetu, Nay wa Mitego, Jokate Mwegelo a.k.a Kidot, Jackueline Wolper, Jennifer Kyaka maarufu kama Odama, Profesa J, Shilole, Snura Mushi, Mzee Majuto, Mzee Small, Ray Kigosi, Dr.Cheni, Elizabeth Michael a.k.a Lulu, Ommy Dimpoz, Agnes Masogange, Hemed Suleiman au 'phd', Jacob Steven maarufu kama'JB', Masanja Mkandamizaji na wengine wengi tukiwataja wote hapa hapatatosha. Kila mmoja anajitahidi kwa nafasi yake katika ubunifu wa kile wanachokifanya.


0 Response to "NA HII VIDEO YA TUBONGE YA JOSE CHAMELIONE KANISANI UMESHAIANGALIA? NI BONGE LA VIDEO ICHEKI"

Post a Comment