SAFARI YA KWENDA KUTUA MWEZINI: CHINA YAWA NCHI YA TATU BAADA YA MAREKANI NA URUSI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SAFARI YA KWENDA KUTUA MWEZINI: CHINA YAWA NCHI YA TATU BAADA YA MAREKANI NA URUSI

Rocket iliyobeba Chang'e-3 kikiwa ndani na "Rabbit" sungura kikirushwa kutoka eneo la Xichang kituo cha kurushia  Satellite  Kusini Magharibi mwa jimbo la  Sichuan, China, hapo tarehe 2  Desember  nmwaka huu.

Ikiwa Nchi ya Uchina leo hii itafanikiwa chombo chake cha anga za juu Chang’e -3 kutua salama katika umbo la angani lililokuwa karibu zaidi na Dunia yetu tunayoishi yaani Mwezi, nchi hiyo ya Mashariki mwa Dunia itakuwa Taifa la Tatu kurusha chombo na kikatua salama katika uso wa mwezi baada ya nchi za Marekani na Urusi kufanya hivyo miaka takribani 37 iliyopita.

Marekani ilikwenda mbali zaidi kwani ilifanikiwa kurusha chombo cha Appolo 11 pamoja na binadamu waliokuwa hai ndani yake wakafika huko na kurudi tena Duniani  wakiwa salama wasalimini.

Change’s-3, chombo kisichokuwa na binadamu ndani kikiwa kimebeba kigari(Rover) kinatarajiwa kutua juu ya mwezi katika eneo liitwalo “Sinus Iridium” au “Bay of Rainbow” saa kumi  jioni kwa saa za huko China Desemba, 2014 kwa mujibu wa Shirika la Habari la China Xinhwa News.


Mara tu kitakapotua, Change’s-3 kitafyatua kigari chenye miguu minne kilichopewa jina la “YUTU” likiwa na maana ya ‘Sungura’ kwa lugha ya Kichina, Kina kamera nne na miguu mingine miwili iliyokuwa na uwezo wa kuchimbua chini ardhini umbali wa mita 30. Kitatalii juu ya uso wa mwezi huku kikichunguza tabaka lake, udongo na miamba kwa angalao muda wa miezi 3.

Jina ‘Yutu’ lilichaguliwa kwa kura na wananchi mtandaoni na linamaana itokanayo na hadithi ya kufikirika ihusuyo mnyama Sungura mweupe wa “Mungu” aliyeitwa Change’s, na anayesadikiwa na Wachina kwamba aliishi mwezini.


Uchina katika Misheni yake hii iliyopewa jina la “China Lunar Exploration Program” imegawanyika katika awamu tatu na ya kwanza ilikuwa ni Kuuzunguka Mwezi, ya pili, Chombo kutua katika Mwezi na ambayo ndiyo hii ya leo, halafu ya tatu itakuwa ni  kuchukua na kurudisha Duniani sampuli za udongo na mawe yanayopatikana mwezini ifikapo hapo mwaka 2020.


Hii ni awamu ya pili na awamu ya kwanza ilikuwa Change-1 na Change-2. China ina dhamira ya kuudhibitishia ulimwengu uwezo wake kama Taifa kubwa sawa na Mataifa mengine ya Magharibi kama Marekani.

Mataifa mengine ya  mashariki yanayofanya jitihada katika safari na kutuma vyombo katika anga za juu ni India, Iran na Pakistan.  

0 Response to "SAFARI YA KWENDA KUTUA MWEZINI: CHINA YAWA NCHI YA TATU BAADA YA MAREKANI NA URUSI"

Post a Comment