MANDELA AZIPATANISHA TENA MAREKANI NA HASIMU WAKE MKUBWA CUBA NI TUKIO LA KIHISTORIA HAIJAWAHI KUTOKEA KILA MTU ASHANGAA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MANDELA AZIPATANISHA TENA MAREKANI NA HASIMU WAKE MKUBWA CUBA NI TUKIO LA KIHISTORIA HAIJAWAHI KUTOKEA KILA MTU ASHANGAA.

Rais Raul Castro kaka wa Rais mtaafu wa Cuba, Fidel Castro akisalimiana kwa kupeana mkono na Rais wa Taifa la Marekani Barak Obama, tukio linalosemekana ni la kihistoria.



Kweli ni maajabu, aliyohutubia Barak Obama ndiyo hayo hayo aliyokuwa akiyatenda pale uwanjani na kwa kweli ikiwa kama asingefanya vile kila mtu angemshangaa, asingeliweza katika hotuba yake kuwalaumu baadhi ya viongozi duniani wanaojidai kumuenzi Mandela kwamba alikuwa msamehevu,  na mwenye kuvumilia mawazo tofauti ya watu wengine ilihali wanashindwa hata kuwa wavumilivu kwa wananchi wao wenyewe wanaoonyesha kutofautiana nao kimtazamo.

Wachambuzi wa mambo wamefikia hata hatua ya kuchambua wahafidhina wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kukataa Rais wao Ruhani asihudhurie shughuli hiyo kwa madai ya kwamba atakwenda kushikana mkono na kiongozi wa “taifa la kishetani” wakimaanisha Marekani. 

Nadhani kama wahafidhina hao ni kweli walikuwa na maana hiyo basi walikuwa sahihi kwani mbele ya Mzee Madiba Ruhani asingelikuwa na ubavu wa kukataa kushikana mkono na Rais Obama. Mandela amekuwa mno alama ya maridhiano na kusameheana na hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Raisi wa Cuba Raul Castro na Barak Obama, bila hata ya ridhaa yao wenyewe walijikuta wakipeana mikono na nadhani huo ndio utakaokuwa mwisho wa uadui wao.



0 Response to "MANDELA AZIPATANISHA TENA MAREKANI NA HASIMU WAKE MKUBWA CUBA NI TUKIO LA KIHISTORIA HAIJAWAHI KUTOKEA KILA MTU ASHANGAA."

Post a Comment