WAFUASI WA MALEMA WAMZOMEA RAIS JACOB ZUMA WAKATI AKIHUTUBIA KUMBUKUMBU YA MAOMBOLEZO YA MZEE MANDELA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WAFUASI WA MALEMA WAMZOMEA RAIS JACOB ZUMA WAKATI AKIHUTUBIA KUMBUKUMBU YA MAOMBOLEZO YA MZEE MANDELA

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Katika Hali iliyowasononesha viongozi wengi walio hudhuria katika kumbukumbu ya maombolezo ya kumuaga Rais Mtaafu na Baba wa Taifa la Afrika ya Kusini Marehemu Nelson Mandela, akiwemo Askofu mtaafu Desmond Tutu, kundi la watu waliojichanganya kwenye umati wa wananchi waliohudhuria shughuli hiyo walikuwa wakimzomea Rais wan chi hiyo Jacob Zuma wakati akitoa hotuba yake.
Kiongozi wa vijana aliyetimuliwa kutoka chama cha ANC Julius Malema
Wachambuzi wa mambo wamedai ya kwamba inawezekana kabisa kutokana na Afrika ya Kusini hususan katika chama cha ANC kuwepo mivutano iliyosababisha kuanzishwa kwa vyama vingine pinzani kama kile kilichoanzishwa na Julius Malema aliyekuwa kiongozi wa vijana ANC akatimuliwa kwa utovu wa nidhamu basi inawezekana waliofanya kitendo hicho wakawa miongoni mwa hao wasioridhishwa na uamuzi wa chama kumtema Julius Malema.

Ilibidi Askofu mstaafu wa Anglican na mshindi mwenza na Mandela wa tuzo ya Nobel ya Amani Askofu Desmond tutu wakati akitoa hotuba yake atumie busara ya hali ya juu, kwa kutanguliza kwanza rai kuwa yeye anasimama kama mzee na angeomba watu wote wliofika pale kuwa na heshima na staha kwa wageni waliokuwa wamefika pale. Kweli bwana kumbe utu uzima ni dawa watu mara moja walitii kauli ya Mzee Tutu wakanyamaza na alipowaamuru kusimama walifanya hivyo kwa adabu.

Ingawa kuna raia wengi wa Afrika ya Kusini wasioridhishwa na mienendo ya Taifa hilo hasa baada ya Mandela kuachana na ulingo wa siasa lakini hapana shaka kwamba asilimia kubwa ya Waafrika Kusini bado wana imani kubwa na chama chao cha ANC, pamoja na Jacob Zuma mwenyewe.


Wazomeaji wanaweza kuonekana washindi  katika hafla hiyo tu lakini katika mustakabali wa siasa za Afrika ya Kusini chini ya misingi imara aliyoiasisi, mwenyewe  Marehemu Nelson Mandela hawana chao. Iweje kweli kama una akili timamu na unataka kumuenzi mtu unayemheshimu kwa kujali uvumilivu, haki,amani na upendo, ukaanze kuzomea kwenye umati wa watu mashuhuri tena katika shughuli ya maombolezo ya mtu aliyechukia uhuni wa dizaini hiyo. 

Hivi kweli ule ni ustaarabu? Hata hapa kwetu Tanzania tabia kama hiyo ipo kwa baadhi ya watu kwa visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu.

0 Response to "WAFUASI WA MALEMA WAMZOMEA RAIS JACOB ZUMA WAKATI AKIHUTUBIA KUMBUKUMBU YA MAOMBOLEZO YA MZEE MANDELA"

Post a Comment