ALIYEVUNJA NDOA YA NELSON MANDELA NA MKEWE WINNIE KUMBE ALIKUWA KINDA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

ALIYEVUNJA NDOA YA NELSON MANDELA NA MKEWE WINNIE KUMBE ALIKUWA KINDA.

Nelson Mandela akiwa na mkewe Bibi Winnie Madikizela Mandela walipooana.
Nelson Mandela baada ya kutoka gerezani, kila mtu alipenda aone shujaa huyo pamoja na familia yake, akiwemo mkewe kipenzi Bibi Winnie Madikizela Mandela aliyetaabika kwa muda wote wa miaka 27 akipambana na makaburu wakati mumewe akiwa kifungoni  wakiishi maisha ya furaha, amani na upendo.

Mandela na Winnie alipotolewa gerezani mwaka 1990
Lakini ni bahati mbaya sana na jambo la kusikitisha kuja kuona miaka miwili tu baada ya kuachiwa kwa Mandela ndoa yao inavunjika, Baada ya kuoana waliishi miaka miwili na pia baada ya kuachiwa kutoka kifungoni waliishi tena miaka miwili tu.

Mandela na Winnie walioana hapo June 14, 1958, lakini walikaa pamoja kwa muda usiozidi miaka miwili Mandela ndipo akafungwa kifungo cha Maisha jela. Kwa kipindi chote hicho cha miaka 27, Bibi Winnie Mandela aliishi maisha ya misukosuko akipigana na utawala wa Makaburu hali iliyomfanya kuwa ‘Sugu’ na mwishowe akatumbukia katika wimbi la ulevi, kukata tama pamoja na uhalifu wa kuteka nyara hali iliyomtumbukiza katika kesi mbaya ya mauaji. Alibadilika kabisa kutoka kuwa msichana mpole wa kijijini, aliyekuwa mwenye haya, mpaka kuwa ‘mwanasiasa moto wa kuotea mbali’ na mwenye jina kubwa.

Skendo iliyokuja kutibua ndoa yao ni tuhuma za uhusiano haramu, baina ya Bi Winnie Mandela na kijana wakili, mfanyakazi katika kitengo cha mahusiano ya jamii cha chama cha ANC aliyejulikana kama Dali Mpofu miaka 30 wakati huo huku Winnie akiwa na miaka mara 2 yake, kitengo ambacho pia ndicho Winnie alikuwa akifanya kazi.


Dali Mpofu  pamoja na Julius Malema walikuwa mmoja kati ya mawakili waliokuwa wakimtetea Bibi Winnie Mandela katika kesi yake iliyokuwa ikimkabili, na uhusiano huo inadaiwa ulianza kipindi hata kabla Mzee Madiba hajatolewa gerezani.
 
Dali Mpofu jamaa anayedaiwa kuivuruga ndoa ya Mandela na Mkewe Winnie.
Lakini katika kujitetea upande wa Winnie ulidai kuwa tuhuma hizo zilikuwa ni njama za Makaburu kutaka kumdidimiza Winnie, kwani hata ndiyo maana walimwachia Mandela huru baada ya kumnunua afanye yale waliyoyataka wao. Julius Malema mwenyewe akimtetea swahiba yake Dali alitamka “Dali Mpofu asingeweza kulala na mama yake”
 
Bibi Winnie Mandela miaka ya 90

Lakini pia Mzee Mandela mwenyewe alikuwa na ushahidi mzito wa barua iliyonaswa ikitoka kwa Bi Winnie kwenda kwa huyo mpenzi wake Dali Mpofu, barua ambayo ndani yake Bibi Winnie Madikizela Mandela alikuwa akilia wivu kwa Mpofu kulitelekeza penzi lake kwake ambalo lilikuwa limemnogea kiasi cha kukaa zaidi ya miezi 6 ndani ya nyumba pasipokusemezana na mumewe Mzee Madiba. Ilikuwa aibu kubwa! 
Mzee Nelson Mandela, kulia ni Bi Winnie Mandela na kushoto ni Bi Graca Machel wakati wa kuadhimisha siku yake ya 84 ya kuzaliwa hapo tarehe 18 July 2004, sherehe zilifanyikia mji alikozaliwa wa QUNU jimbo la Cape

Ikabidi ndoa ivunjike, kila mtu akaishi kivyake na hapo ndipo Mzee Madiba alipoamua ‘kuvuta kifaa kingine’ Graca aliyekuwa mjane wa rais Rrais wa Msumbiji Samora Machel.

0 Response to "ALIYEVUNJA NDOA YA NELSON MANDELA NA MKEWE WINNIE KUMBE ALIKUWA KINDA."

Post a Comment