KUPINDULIWA SERIKALI YA JOSEPH KABILA WA CONGO UVUMI WAZAGAA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUPINDULIWA SERIKALI YA JOSEPH KABILA WA CONGO UVUMI WAZAGAA


Wasiwasi umetanda kote nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Barani Afrika na Duniani kwa ujumla baada  ya vijana waliokuwa na silaha za kienyeji kama mapanga, marungu na mashoka pamoja na bunduki kuvamia  maeneo ya kituo cha Televishen ya taifa, makao makuu ya Radio  uwanja wa ndege.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa milio ya risasi ilianzia uwanja wa kimataifa ambapo pia kuna taarifa kupitia mitandao kwamba milipuko ya risasi ilisika katika maeneo ya kambi ya jeshi.


Wanasema risasi zilizkuwa zikifyatuliwa kuelekea kila pande hivyo kuwalazimu watu waliokuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Kinshasa kujificha kujikinga na mashambulio hayo.
Msemaji wa polisi Kanal Mwana Mputu anasema Polisi wanaendelea kudhibiti eneo hilo huku wakiendelea kuwasaka wanaohusika katika shambulio hilo japo hawajaeleza sababu za shambulio hilo.

CHANZO: BBC

0 Response to "KUPINDULIWA SERIKALI YA JOSEPH KABILA WA CONGO UVUMI WAZAGAA"

Post a Comment