MSANII MWINGINE WA KIKE “MISS” JACK PATRIC ADAIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MSANII MWINGINE WA KIKE “MISS” JACK PATRIC ADAIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA


Ile dhana iliyokuwa imejengeka miongoni mwa watu wengi nchini kwamba huenda Utajiri wa wasanii wengi wa muziki na filamu hapa nchini, kwamba siyo wa kawaida bali unatokana kwa kiasi kikubwa na biashara ya dawa za kulevya, inazidi kushikakasi vichwani mwa watu baada ya msanii mwingine tena ambaye pia aliwahi kuwa Miss wilaya ya Ilala kudaiwa kukamatwa na dawa za kulevya huko nchini China.

Habari kuhusiana na tukio hili zimeripotiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ukiwemo Jamii forum walioandika hivi kuhusu msanii huyo,

Anayedaiwa kuwa Jack Patrick akisindikizwa na mwanausalama katika chumba cha mkutano na mapaparazi.
 Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.


Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

Pichani(juu kabisa mwanzoni) ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013.”

Waandishi Habari huko china wakichukua picha katika tukio hilo

















Jack Patrick enzi zake akila bata.
Mrembo huyo ‘Jack Cliff’ pia aliwahi kushiriki katika video ya wimbo maarufu wa Diamond Platnumz ‘Nataka Kulewa” Hebu mcheki hapo chini videoni jinsi alivyokamua vizuri katika wimbo huo wa ‘Nataka kulewa’ halafu ujaribu kupiga picha ni jinsi gani mwanadada huyo mrembo atakavyo kwenda kukabiliana na kitanzi.(Ikiwa atapatikana na hatia lakini japo tunamuombea apone) Ni afadhali hata ya mumewe Abdullatif  Fundikira aliyekamatwa na dawa kama hizo lakini akafungwa Tanzania ambako hamna hukumu ya kitanzi kama ilivyo Uchina.



CHANZO: JAMII FORUM

0 Response to "MSANII MWINGINE WA KIKE “MISS” JACK PATRIC ADAIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA"

Post a Comment