MWENDESHA MAGARI YA MASHINDANO MAARUFU FORMULA ONE MICHAEL SCHUMACHER HALI BADO TETE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MWENDESHA MAGARI YA MASHINDANO MAARUFU FORMULA ONE MICHAEL SCHUMACHER HALI BADO TETE

Michael Shumacher 
Kufuatia ajali aliyopata bingwa wa mashindano ya magari ya Formula One Michael Shumacher kwenye mchezo wa kuteleza kwenye barafu, madaktari wamesema kwamba hali yake bado ni tete na anapigania uhai wake kwani alipata mshituko mkubwa baada ya kubamiza kwa nguvu kichwa.

Michael Schumacher mshindi mara saba wa mashindano ya Formula One yupo kwenye hali tete baada ya kufanyikwa matibabu kutokana na ajali aliyopata akiwa anacheza mchezo wa kuteleza kwenye barafu.


Schumacher mwenye miaka 44 alidondoka mapema Jumapili na kugonga kichwa chake kwenye mwamba na hizi ni taarifa kutoka kwenye kituo ambacho alikuwa anacheza huo mchezo.
Japokuwa managers wa kituo hicho wamesema Schumacher alikuwa amevaa helmet wakati  anacheza.
Baada ya ajali hiyo Michael alofikishwa kwenye hospital ya the Grenoble University Hospital Center kwa ajali ya matibabu.


0 Response to "MWENDESHA MAGARI YA MASHINDANO MAARUFU FORMULA ONE MICHAEL SCHUMACHER HALI BADO TETE"

Post a Comment