BINADAMU BANDIA WA KWANZA KUUNDWA NA WANASAYANSI AZUNGUMZA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BINADAMU BANDIA WA KWANZA KUUNDWA NA WANASAYANSI AZUNGUMZA.

Binadamu wa kwanza kutengenezwa na wanasayansi , kwa mara ya kwanza ameonyeshwa katika jumba la makumbusho mjini Washington nchini Marekani. Binadamu huyo kwa jina ‘Frank’ alitengenezwa katika chuo kikuu cha Zurich kuonyesha namna uhandisi wa kibaiolojia ulivyopiga hatua kubwa katika siku za hivi karibuni.
 
Binadamu wa bandia aliyetengenezwa na wanasayansi
Anakaribia kuwa kama sisi kila kitu kuanzia moyo, maini , figo, mikono, miguu, mishipa ya damu na kila kiungo ila kasoro  moja tu ni kwamba hawajaweza kuunda ubongo.

BBC ilipomuuliza ‘mtu huyo wa bandia’ endapo watakuja kuwa mbadala wa binadamu wa kawaida, alijibu  “hapana” bali wao ni kwa ajili tu ya kuwapa manufaa binadamu wa kawaida hasa katika maswala ya kitabibu kama vile kubadilishana viungo vilivyofeli, mfao figo, moyo, ini, na vinginevyo.



0 Response to "BINADAMU BANDIA WA KWANZA KUUNDWA NA WANASAYANSI AZUNGUMZA."

Post a Comment