NUSURA MAGULUKO THE BUS DRIVER, 'HAWA THE BUS DRIVER' WA KARNE YA 21 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NUSURA MAGULUKO THE BUS DRIVER, 'HAWA THE BUS DRIVER' WA KARNE YA 21


Niliposoma habari ya mwanadada huyu katika blogu ya Irenemwamfupe kwa kweli nilikumbuka mbali sana, enzi zileee………., tukiwa ‘O level’ tukisoma vitabu vya Literature form one na two. Kulikuwa na kitabu kimoja kilichotungwa na mwandishi mashuhuri Richard S. Mabala, ‘HAWA THE BUS DRIVER’, Hawa alielezewa na Mabala kama mwanamke aliyekuwa jasiri, shupavu kiasi ambacho hata wanaume akiwemo na mumewe mwenyewe walimuogopa na kumheshimu. Hawa mbali na kuwa jasiri pia alikuwa dereva wa basi, nadhani wakati huo labda ilikuwa ni UDA, akifanya safari zake kwenda mjini.
Nilikisoma kitabu hicho karne iliyopita ya 20 lakini leo hii ninapokikumbuka maudhui yake na mafundisho utafikiri ndiyo kwanza kimeandikwa leo, vitabu vya Mabala vilinivutia sana nadhani hata na watu wengi viliwavutia pia.
 
Nusura akiomba kabla ya safari.

Dereva Nusura Maguluko akiwa 'mzigoni'
Dereva Nusura Maguluko kwa mujibu wa Irene blogu ni dereva wa kike katika basi la Ndenjela Coach linalofanya safari zake, Mbeya na Dar es sala.

Picha ya kitabu ni kutoka blogu ya Susan Abraham.

0 Response to "NUSURA MAGULUKO THE BUS DRIVER, 'HAWA THE BUS DRIVER' WA KARNE YA 21"

Post a Comment