“VIJANA JIEPUSHENI NA MASUGARMUMMY NA MASUGARDADDY”: PASTOR MITIMINGI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

“VIJANA JIEPUSHENI NA MASUGARMUMMY NA MASUGARDADDY”: PASTOR MITIMINGI

Mkuu wa huduma ya VHM, Mchungaji Mitimingi akitoa semina
Katika semina za vijana  zinazotolewa kila mwezi na Wapo Mission katika ukumbi wa BCIC Mbezi Beach maarufu kama semina za  kuwaridhisha vijana vipawa na maadili chini ya Askofu Sylvester Gamanywa, semina ya mwezi huu, walialikwa wazungumzaji mbalimbali na miongoni mwao alikuwa ni Mchungaji Peter Mitimingi wa huduma ya VHM  aliyetoa mada juu ya Mahusiano.

Katika hotuba yake, aliwaasa vijana kujiepusha na ‘Mashugamami’ na ‘Mashugadady’  ili kujitegemea kimaisha. “Piga kazi kwa mikono yako , Biblia inasema, Mungu atabariki kazi ya mikono yenu, siyo kazi za mikono ya ile mijimama kule”. Alisema.

Askofu Sylvester Gamanywa akiongea na vijana.


Naye  Mzungumzaji  mwingine, Dr. Binagwa  akitoa mada alisema, “Ni vigumu sana kijana tunayemtaka mwenye muelekeo mpya, mabadiliko mapya, mtazamo mpya, kama hana malengo maishani, anajiendea, kama hafuati muda, kama hana imani, kama hajali, kama hana nidhamu, kama hajengi uchumi binafsi, ni vigumu sana kijana huyo kuendelea”

Picha kutoka mitandao ya martamalecela.blogspot na wapofm.org

0 Response to " “VIJANA JIEPUSHENI NA MASUGARMUMMY NA MASUGARDADDY”: PASTOR MITIMINGI"

Post a Comment