KAMPUNI KUBWA LA MICROSOFT 'LAIMEZA' NOKIA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KAMPUNI KUBWA LA MICROSOFT 'LAIMEZA' NOKIA

Afisa mtendaji mkuu wa microsoft Steve Ballmer, kusoto na Mwenyekiti wa bodi,  Nokia, Risto Siilasmaa kulia
Kampuni ya simu za mkononi ya Nokia imesaini mkataba wa kununuliwa na Kampuni kubwa la Microsoft  kwa kiasi cha shilingi trilioni 11.5  sawa na Euro bilioni 5.4 au dola bilioni 7.2.

Nokia pia itatoa leseni zake za hati miliki pamoja na ramani za huduma zake kwa kampuni hiyo inayomilikiwa na tajiri namba moja Marekani  Bill Gates. 

Kwa mujibu wa mitandao mbali mbali ikiwemo Sky News, BBC,  CNN na USA Today, Makampuni hayo kwa pamoja yalinukuliwa mbele ya waandishi wa habari kuwa makubaliano hayo yatakamilika mwanzoni mwa mwaka ujao, wakati ambao kiasi cha wafanyakazi 32,000 wa Nokia watahamishiwa kwenye kampuni ya Microsoft.

Simu ya Nokia maarufu kama "kitochi"
Wakati Nokia ikikumbwa na ushindani mkali kutoka kwa washindani wake Samsung& Apple na simu zao za kisasa za smsrtphones yenyewe imeendelea kubakia nyuma na simu zake za bei ya chini kama nokia za tochi. Vilevile imekuwa ikikosolewa kwa kutokuwa na kasi ya kutosha kwenye soko la simu za mikononi.

Kwa upande mwingine Samsung na Apple nao wamekuwa wakikosolewa vikali kutokana na simu zao pamoja na vifaa vingine kama Ipad na kompyuta mpakatoto kutokukaa na chaji muda mrefu. Ikiwa Microsoft watakuja na ubunifu betri ikakaa angalao siku mbili au tatu washindani wake hao watakuwa wamepigwa bao la kisigino. Si ajabu nao wakaja na aina nyingine mpya ya smartphones.

“Ni hatua kubwa kwa siku zijazo  ambapo ni mafanikio makubwa kwa wafanyakazi, wanahisa na wateja wa makampuni yote mawili” alisema Steve Ballmer, Mtendaji Mkuu wa Microsoft.

0 Response to "KAMPUNI KUBWA LA MICROSOFT 'LAIMEZA' NOKIA"

Post a Comment