'MAJANGA' YA MARAISI AFRIKA MASHARIKI CHANZO CHA WIVU KWA JK. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

'MAJANGA' YA MARAISI AFRIKA MASHARIKI CHANZO CHA WIVU KWA JK.


HUU NI MTAZAMO WANGU:

Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete
Ni dhahiri kabisa sasa kwamba Uganda , Rwanda na Kenya , siyo kitu kimoja tena na Tanzania kama ilivyokuwa wakati walipoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki. Badala yake kinachoonekana kinafanana na kile kilichoiua Jumuiya ya Africa Mashariki ya akina Mwalimu JK.Nyerere, Idd Amin Dada na Jommo Kenyata hapo mwaka 1977; ‘tofauti za viongozi kuliko wananchi wa kawaida’.

Rais wa Uganda Kaguta Museven
Mimi binafsi naona kinachowasumbua Maraisi hawa wa nchi hizi tatu ni wivu, ukiwachunguza wote, Kagame, Museven na Kenyatta , wote wana “Majanga”  aidha yanayowasubiri  au yanayowasumbua tayari kwa muda mrefu.

Tukianza na Museven, yeye kwanza amengangania madaraka kwa muda mrefu kitu ambacho hata waliokuwa washirika wake wa karibu sana nchi za Magharibi zimeanza kumchoka. Licha ya kuitisha chaguzi za mara kwa mara lakini kidemokrasia ilifaa angatuke. Kutokana na sababu hii wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanamweka katika kundi la akina Muamar Ghadafi na Mubarak. Kutokana na sababu hizo bila shaka atamuona Rais Kikwete kama yuko juu zaidi yake.
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Kwa upande wa Rais Paul Kagame, yeye kama rafiki yake Museven, amengangania madarakani kwa muda mrefu na inadaiwa pia kwamba anawakandamiza wapinzani wake kisiasa na hata wakati mwingine kutuma majasusi kwenda kuwaulia uhamishoni wanakokimbilia kwa kisingizio cha kutokomeza ubaguzi wa kikabila. Janga jingine linalomuandama ni hili la “kutia mafuta ya taa” mgogoro Mashariki mwa DRC, Wachambuzi wamefika mbali na kutabiri hata Kagame kuja kuburuzwa The Hauge siku za usoni kama kina Loraa Gbagbo na Charles Tylor.

Rais Kenyata, kwanza anashangaza kwani, Kikwete ndiye aliyekwenda kusaidia kupoza machafuko ya ghasia za baada ya uchaguzi  2007 pasipo kuonyesha kuegemea upande wowote. Kenyata pamoja na kushinda uchaguzi uliopita , lakini bado suala la kesi yake na Ruto ICC nalo linamfanya ajione mdogo mbele ya Jk.
 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
“Majanga” hayo ya Maraisi hawa watatu yanawakosesha usingizi na kumuona mwenzao Rais Kikwete kama ana bahati na yupo juu zaidi kuliko wao. Ujio wa Viongozi wakubwa wakubwa wakiwemo Maraisi wa Marekani hasa Rais Barak Obama kulizidi kuwachefua , kwa kuona hata endapo hapo baadae labda Marekani itaamua kumng’oa mmoja wao kama ilivyofanya kwa kina Ghadafi basi ni lazima iitumie Tanzania kama ‘Base’  


Sasa ndio wameamua kumzunguka kwa visingizio kibao visivyokuwa na kichwa wala miguu ili  Jk na Tanzania kwa ujumla tuonekane hatufai mbele ya jumuia za Kimataifa.

0 Response to "'MAJANGA' YA MARAISI AFRIKA MASHARIKI CHANZO CHA WIVU KWA JK."

Post a Comment