TAJIRI ANAYEONGOZA AFRIKA ALIKO DANGOTE AMEKOPA, WEWE UNANGOJA NINI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

TAJIRI ANAYEONGOZA AFRIKA ALIKO DANGOTE AMEKOPA, WEWE UNANGOJA NINI?

Bilionea namba moja Afrika Aliko Dangote
Tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote wa Nigeria , leo amesaini mkataba wa mkopo na umoja wa mabenki ya ndani na nje ya Nigeria unaofikia Dolla za kimarekani bilioni 3.3 kwa lengo la kujenga kiwanda kikubwa kabisa cha kusafisha mafuta na bidhaa za petrol ikiwa ni pamoja na mbolea za chumvi chumvi.

Kiwanda hicho kitagharimu jumla ya dola za Kimarekani billion 9 na kitatengeneza nafasi za moja kwa moja za ajira zipatazo 9,500 huku ajira zisizokuwa za moja kwa moja zikiwa ni 25,000.

Aliko Dangote ndiye Mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa Jarida maarufu la Forbes.

0 Response to "TAJIRI ANAYEONGOZA AFRIKA ALIKO DANGOTE AMEKOPA, WEWE UNANGOJA NINI?"

Post a Comment