MELI UKUBWA WA VIWANJA 2 VYA MPIRA YAUNDWA INDIA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MELI UKUBWA WA VIWANJA 2 VYA MPIRA YAUNDWA INDIA.

INDIA
India imeunda meli yake ya kwanza yenyewe iliyokuwa na uwezo wa kubeba ndege na vyombo vya angani katika mji wa Kusini wa jimbo la Kerala.

INS Vikrant.

Ripoti inasema kuwa meli hiyo yenye uzito wa tani 37,500  inayoitwa INS Vikrant inatarajiwa kufanyiwa majaribio makubwa  mwaka 2016 kabla haijaungana na meli nyingine za kijeshi mwaka 2018.


Nchi nyingine zenye uwezo wa kuunda meli kama hiyo ni Marekani, Uingereza, Urusi na Ufaransa. Meli hii ina urefu wa mita 260 sawa na futi 850 na upana wake ni mita 60. Imeundwa bila kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi kwa kutumia  chuma aina ya steel chenye ubora wa hali ya juu kutoka kampuni inayomilikiwa na serikali.


CHANZO : BBC NEWS

0 Response to "MELI UKUBWA WA VIWANJA 2 VYA MPIRA YAUNDWA INDIA."

Post a Comment