UTAJIRI WA DHULUMA NA KAFARA HAUNA BARAKA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UTAJIRI WA DHULUMA NA KAFARA HAUNA BARAKA.

Arusha,
Hayo yalisemwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Meru, Paul Akyoo alipokuwa akiongoza misa ya mazishi ya aliyekuwamfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, Erasto Msuya (43) jana huko mkoani Arusha.



Katika mahubiri yake yaliyochukua dakika 30, alisema utajiri wa aina hiyo hauna baraka wala amani kwa wahusika kutokana na dhamira zao kuwasuta kila wanapokumbuka uhalifu walioutenda.



Katika mazishi hayo yaliyokuwa na watu wengi kiasi cha Kamati ya Mazishi kulazimika kusitisha utoaji wa heshima za mwisho,Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema wauaji wa Msuya watasakwa na kufikishwa mahakamani wiki ijayo.

“Waliomuua Msuya wataumbuka mchana kweupe wiki ijayo watakapofikishwa mahakamani. Nawahakikishia kuwa vyombo vya dola viko kazini na ukweli kuhusu waliohusika na tukio hili la kinyama utajulikana hadharani wiki ijayo wahusika watakapofikishwa mahakamani,” alisema Mulongo.
Naye Lazaro Mambosasa, ambaye alimwakilisha Mkuu wa jeshi la polisi, IGP Said Mwema, alisema  IGP Mwema amewaagiza polisi katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro kuwasaka na kuwafikisha mahakamani wahusika wote bila kujali majina, ukwasi wala vyeo vyao.




























Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Maselle ambaye aliwasilisha salamu za rambirambi za Rais Jakaya Kikwete naye alisema Rais Kikwete ameshtushwa na kusikitishwa na mauaji ya Msuya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu katika mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.
Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Agosti 7, mwaka huu, alizikwa saa 10:20 jioni.
Chanzo blogu ya Larrybwy91 

0 Response to "UTAJIRI WA DHULUMA NA KAFARA HAUNA BARAKA."

Post a Comment