SIKU YA MEI MOSI: JE AJIRA NI JAMBO BAYA, UTUMWA NA KUKOSA MALENGO? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SIKU YA MEI MOSI: JE AJIRA NI JAMBO BAYA, UTUMWA NA KUKOSA MALENGO?


SIKUKUU YA MEI MOSI
Leo ni siku ya kwaza ya mwezi wa tano May mosi, ni siku ya kwanza ya muda wamaisha yetu yaliyobakia hapa duniani. Kwa wafanyakazi katika sekta mbalimbali ni siku ya kutafakari na kujiuliza ikiwa ni kitu gani hasa wanachohitaji bila kujihukumu na mazingira ama hali yako ya huko nyuma ulikotoka.

Inawezekana huko nyuma mambo yako hayakuwa mazuri hata kidogo au yalikuwa mazuri lakini huu si wakati wa kutathmini malengo yako au ndoto zako kwa kutazama huko nyuma ilikuwaje ni wakati wa kuyatazama upya malengo yako ukizingatia tu kile unachokitaka maishani, ukitafutie maarifa, urekebishe upya mpango wako na mwisho upate mafanikio makubwa, makubwa ambayo hujawahi hata siku moja kuwa nayo katika maisha yako yote huko ulikotoka.


Kwa imani, kauli na fikra chanya muda wote mwili wako utafanya kile kile ambacho akili yako imekuwa ikiuambia mara kwa mara kwa kujua au hata kwa kutokujua. Ikiwa tunataka mafanikio chanya kifedha na kimaisha kwa ujumla katika maisha yetu, hatuna budi kuzuia na kuondoa kabisa mambo yote hasi yanayotuzunguka iwe ni katika vitu vinavyotuzunguka, watu na hata mawazo yetu wenyewe kwani chochote kile tunachoelekezea nguvu na akili zetu kiwe kibaya au kizuri, akili zetu hukibadilisha kuwa katika kitu halisi tuwe tunapenda au hatupendi.

Lenga tu katika ndoto na malengo yako na jiweke mbali kabisa na vitu, watu na matukio yenye mlengo hasi yanayoweza kukufanya kutoa pia kauli hasi, hii inaweza ikawa vigumu sana kutekeleza hasa katika nyakati hizi zilizojaa kila aina ya taarifa lakini inawezekana ikiwa utaamua kufanya maamuzi. Wewe mwenyewe ndiye uliye na uamuzi wa mwisho wa kuruhusu taarifa au mawazo yeyote yale kutoka nje kuingia akilini mwako, hata ikiwa kuna watu wako wa karibu vipi ambao unahisi wanakutoa katika mstari wa malengo yako una uwezo na haki ya kuwaambia “jamani naombeni mkae mbali na mimi nitimize kwanza malengo yangu.” Jihusishe tu na vitu au watu walio na mawazo ya kujenga ikiwa kama kweli umeamua kubadilika.


Achana kabisa na kauli kama vile, “siwezi”, “ni ngumu mno” “haiwezekani” na “sitaweza” kauli kama hizi zitajijenga katika akili yako na kushika mizizi kama vile magugu yafanyavyo katika shamba la ngano safi zikijifanya kuwa nazo ni safi kumbe ni vitu viharibifu. Kauli hizi zikizoeshwa akilini mtu hujikuta akirudiarudia makosa yaleyale aliyokuwa akiyafanya zamani.

Iwe wewe ni mfanyakazi au hata unafanya shughuli zako za kujiajiri, kila mtu ana ndoto zake, hizo ni njia tu za kuzifikia ndoto hizo. Jambo jingine la kuzingatia ni kwamba binadamu hatujaumbwa kudumu na kitu kimoja maisha yetu yote, aliye kwenye ajira leo itafika muda unaweza ukaja kumkuta amebadilika na kuwa mfanyabiashara mkubwa au mwekezaji. Hali ni hivyo hivyo ilivyo kwa waliojiajiri au wenye biashara zao binafsi, kesho na keshokutwa unaweza kuja kumkuta mtu aliyekuwa na biashara zake akifanya kazi kwa mtu katika kampuni. Hivyo binafsi siamini kama kuajiriwa ni laana hata kidogo bali ni njia bora ya kuelekea kujiajiri

Ajira na kujiajiri ni vitu 2 vinavyotegemeana na hakuna kilichokuwa bora kushinda mwenzake, ikiwa kila mtu angeamua kuwa na biashara yake au kampuni, wafanyakazi wangetoka wapi? Lakini kitu cha kuzingatia hapa ni malengo yako katika kile unachokifanya sasa iwe umeajiriwa au umeajiri. Ikiwa ndoto zako ni siku moja kuja kuajiri kumiliki biashara unaweza ukaanza na kuajiriwa kwanza wala siyo kosa hata kidogo, halafu mwishowe ukaja kugeuka kuajiri watu wengine na wewe.


Hivyo ndivyo mzunguko ulivyo duniani kote. Mtu yeyote asije akakudanganya kwamba eti ajira au kufanya kazi ya mtu mwingine au serikali ni jambo baya, ni utumwa nk. hapana, hiyo ni njia tu ya wewe kufikia ndoto zako, na kukamilisha mzunguko ambao ikiwa kama usingekuwepo basi mambo yasingelikwenda kabisa duniani, ni sawa kama ilivyokuwa katika mbuga ya wanyama, Simba na chui wapo lakini ni lazima pia kuwe na nyasi, miti, swala, nyati na pundamilia ili simba chui na wanyama wengine wote hao waweze kuishi, ukiondoa kimoja hakuna mbuga ya wanyama tena.

……………………………………………………

Ndugu msomaji, vitabu 3 vya self help books Tanzania vipo na unaweza ukajipatia nakala yako katika mifumo yote miwili iwe unataka softcopy kwa njia ya email au hardcopy kitabu halisi cha karatasi. Softcopy tunatuma kwa njia ya email na hardcopy tunakuletea mpaka ulipo ikiwa upo Dar es salaam. Mikoani tunatuma kwa mabasi au unaweza kumuagiza mtu anayekuja Dar. Tazama majalada yake hapo chini pamoja bei zake.

Kwa anayenunua softcopy ya kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI anapata pia na offa ya kujiunga na group la masomo ya kila siku WHATSAP pamoja na masomo mbalimbali na semina zilizopita. 

Usisahau pia katika Group la WHATSAPP masomo ni kila siku kwa mfano leo Jumatatu tutakuwa na somo lisemalo, "HATUA 3 MUHIMU UNAZOWEZA KUZIDHARAU LAKINI UKIZICHUKUA NI LAZIMA MIPANGO YAKO IZAE MATUNDA"  Pia Tafsiri ya kitabu cha Think & Grow rich nayo itakuwepo na leo ni sehemu ya 3 ya sura ya 10 

SIMU:   0712202244, 
WHATSAPP: 0765553030



SOFTCOPY KWA EMAIL SH. 10,000

HARDCOPY  DAR    NI    SH. 22,000




 SOFTCOPY KWA EMAIL SH. 5,000

HARDCOPY  DAR    NI    SH. 10,000



SOFTCOPY KWA EMAIL SH. 3,000

HARDCOPY  DAR    NI    SH. 5,000

0 Response to "SIKU YA MEI MOSI: JE AJIRA NI JAMBO BAYA, UTUMWA NA KUKOSA MALENGO? "

Post a Comment