JE, WAJUA BINADAMU NI LAZIMA AFANYE BIASHARA ANGALAO MARA MOJA MAISHANI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE, WAJUA BINADAMU NI LAZIMA AFANYE BIASHARA ANGALAO MARA MOJA MAISHANI?

Hebu jaribu hata kuchunguza wale watu walioko kwenye ajira, viongozi mbalimbali wa kisiasa na kiserikali unapofika muda wakastaafu ama kuachana na nyadhifa zao huwa wanakwenda kufanya kitu gani?. Unaweza ukaniambia wengi wao huenda kupumzika wakila pensheni zao au mafao yao ya uzeeni. 

Hilo halina ubishi lakini ukweli unabakia palepale kwamba mafao hayo au pensheni hayawezi kumhakikisha mtu uhuru na usalama kifedha kwa kipindi kirefu. Fedha hizo za mafao zinahitajika zizae ndipo ziweze kumhakikishia mstaafu uhuru kifedha kwa maisha yake yote yaliyobakia.

Hali hii ndiyo husababisha watu wengi wanapokuwa bado makazini au wawapo bado viongozi hata katika ngazi za juu kabisa wakati mwingine hata maraisi wa baadhi ya nchi hapa duniani, hutamani au hata kuwa na mawazo ya kuanzisha miradi ya kiuchumi kusudi watakapostaafu wawe na vitegauchumi vya kuwafanya waendelee kuishi maisha mazuri na hapa ndipo ilipo hoja yangu hii ninayotaka kuijenga ya kila binadamu katika nyakati fulani za maisha yake ni lazima atafanya biashara hata mara moja taka asitake.


Yupo mzee mmoja rafiki yangu sana, siku moja nilipokuwa napiga naye stori kuhusu masuala ya maisha, pesa, kazi na biashara kwa ujumla akawa ananiasa sana juu ya kuzingatia kufanya biashara. Yeye anasema anapenda sana kufanya biashara lakini anakiri katika maisha yake karibu yote hajawahi kufanya biashara hata moja. Anasema alikuwa akifanya kazi ya kuajiriwa kama afisa masoko kwenye taasisi moja ya serikali. 

Lakini cha kushangaza akaniambia baada ya kustaafu sasa analima mihogo huko Kiluvya kwa ajili ya kisamvu katika shamba lake ambacho huwa anawauzia kina mama wajasiriamali ambao nao huenda kukiuza kisamvu hicho maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Siyo hivyo tu mzee yule wa kichagga alinieleza kwamba anao mradi wa kutotolesha vifaranga wa kuku na kuku wachache kwa ajili ya mayai ya kuuza.

SOMA: Mchanganuo wa biashara ya kuku wa mayai 1000

Ilibidi nimuulize, “Sasa mbona umesema hujui kufanya biashara na miradi yote hiyo ni nini?” Mzee akachek sana na kusema, “afadhali wewe unaelewa, sikupenda kukuambia nafanya biashara kwa sababu watu wengi hawachukulii miradi kama hii kuwa ni biashara, kwenye akili za watu wengi wamejenga taswira kuwa biashara ni zile kubwakubwa tu au zinazohusisha kuuza na kununua peke yake wanasahau hata miradi kama hii ya ufugaji na kilimo pia ni biashara ikifanywa kitaalamu.” 

Mzee yule aliendelea kuniambia hata kuwa na nyumba za kupangisha nayo ni biashara pia. Hivyo na mimi nikaja kutambua kwamba hata mtu aliyestaafu kazi ya kuajiriwa lakini akawa alijenga nyumba zake za kupangisha hilo lilikuwa ni wazo lake la biashara itakayomsaidia baada ya kustaafu.

Hivyo ni sahihi kabisa kusema kwamba “Mwanadamu penda asipende ni lazima katika muda fulani wa maisha yake atafanya biashara tu” Kama ndiyo hivyo basi, ni nini cha kufanya?

Inafaa kila mtu kujifunza ABC kuhusiana na biashara na ujasiriamali mapema iwezekanavyo bila kujali yupo katika ajira au karibu anaachana na ajira au hata ameshastaau ajira. Uzuri ni kwamba siku hizi siyo kama zamani mpaka uingie darasa la semina ndipo uweze kujifunza. Kuna mtandao wa Intaneti ambao una njia nyingi za kujifunza kupitia simu yako au kompyuta. Kuna programu mbalimbali unazoweza kufuatilia mwenyewe ukiwa popote pale. Vipo pia vitabu kama vya SELF HELP BOOKS TANZANIA vilivyoandikwa kwa kiswahili vyenye kila kitu ambacho mjasiriamali yeyote anahitaji ili kufanikisha biashara yake kwa ufanisi wa hali ya juu.

Self Help books tuna kitabu kimoja, MICHANGANUO YABIASHARA NA UJASIRIAMALI, hiki ni kama alfa na Omega kwani kina kila kitu ndani, kina kurasa 410 ambazo kila moja huwezi kuiruka kama wewe ni mroho wa material za ujasiriamali na biashara. Tunacho pia MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRIWASIYOPENDA KUITOA, hiki nasema ndiyo baba wa vitabu vya hamasa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, sitii chumvi wala kuvuta kamba kwangu kama huamini jaribu kudownload kurasa chache za KITABU HICHO HAPA usome. 

Kitabu kingine cha malipo tuna MAFANIKIO YA BIASHARA. DUKA LA REJAREJA, nisingependa kukiongelea sana kitabu hiki kwani ni mimi nimekitunga mwenyewe kutokana na uzoefu wangu binafsi wa miaka 12 nikifanya biashara hiyo. Nathubutu kusema hakuna nisichojua kuhusiana na duka la rejareja, jipatie kitabu hicho uthibitishe mwenyewe.

Sipendi kukulazimisha kununua vitabu hivyo, kwanza sijui mfuko wako ukoje na hali yenyewe sasa hivi inajulikana na kila mtu pesa ni ngumu, basi walao nitakupa bure kitabu kingine hiki hapa, SIRI NA MBINU ZAKUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO, sitaki thumni yako, wewe bonyeza hayo maandishi kisha ujaze email yako, jina na nambari ya simu kisha chukua kitabu ujisomee free of charge..!

1 Response to "JE, WAJUA BINADAMU NI LAZIMA AFANYE BIASHARA ANGALAO MARA MOJA MAISHANI?"