SALAMU ZANGU 2018 KUKUTAKIA HERI NA MAFANIKIO YA KWELI, KWAHERI 2017 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SALAMU ZANGU 2018 KUKUTAKIA HERI NA MAFANIKIO YA KWELI, KWAHERI 2017


Sasa hivi ni Jumatatu saa sita na dakika moja mwezi wa kwanza mwaka 2018(1/1/2018) na pia ni mwanzo wa maisha yetu mimi na wewe yaliyobakia hapa duniani. Je, ni kitu gani unachotaka katika muda huo wa maisha yako uliobakia? Usije ukachagua kitu kulingana na hali yako uliyokuwa nayo sasa wala hali yako uliyokuwa nayo zamani.

SOMA: Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena.

Tengeneza ndoto zako na malengo yako ukizingatia kile kitu hasa unachokitaka. Tafuta maarifa, weka mpango, tekeleza mpango na mwishowe pata mafanikio makubwa kuliko yale uliyowahi kuwa nayo katika muda wako wote uliokwisha ishi hapa duniani. Kwa kuhakikisha imani yako, fikra na maneno vinakuwa chanya, mwili wako utafanya kile akili inayouambia ufanye kwa kujua ama kwa kutokujua.

Ungependa mafanikio chanya na utajiri katika maisha yako? Basi zuia kabisa na wala usikaribiane na ‘takataka’ zozote hasi kutoka mahali popote, kutoka kwa mtu yeyote wala kutoka kwa kitu chochote. Chochote kile unachokilenga kiwe kizuri au kibaya, akili yako itakigeuza kuwa kweli iwe unataka au hutaki. Lenga kwenye ndoto zako na malengo yako, jiepushe na vitu vyovyote hasi, iwe ni watu au matukio yote yanayokusababisha utende au kuzungumza mambo yaliyokuwa hasi.

SOMA: Uwe ni mwaka wa kufanya mapinduzi makubwa katika maisha yako kiuchumi.

Hili linaweza kuwa jambo gumu kutekeleza katika dunia hii iliyojaa nguvu hasi, lakini UNAWEZA! Cha msingi tu ni kuamua kufanya utekelezaji. Ikiwa ni lazima uachane na marafiki kwa kuwa fikra zao ni hasi mno na wanakwaza ndoto zako ni bora na iwe hivyo. Jiambatanishe mwenyewe na watu walio na ndoto za mafanikio kama za kwako na jiepushe kabisa na wale wenye fikra hasi wakiwemo hata marafiki zako vipenzi wa muda mrefu. Ikiwa unataka mafanikio zaidi maishani ni lazima sasa uamue kufanya hayo mabadiliko kwa dhati ya moyo wako.

Semi kama vile, “siwezi”, “sitaweza” “ni ngumu mno”, zote hizi ni kauli, na unapozitoa kauli kama hizi ‘unaiprogramu’ akili yako mithili ya kompyuta kutokufanya chochote kile cha maana isipokuwa kubakia vilevile kama ulivyokuwa mwaka jana 2017 na miaka mingine iliyopita. Mwanasayani mashuhuri na wa wakati wote, Albert Einstain aliwahi kutamka maneno haya hapa chini; 

“Uwendawazimu maana yake ni kufanya jambo lilelile, tena na tena ukitegemea matokeo tofauti”-Albert Einstain.

Unaweza ukajiuliza; “Ni kwa vipi nitaweza kutekeleza haya?” Kama umeweza kusoma makala hii hapa, bila shaka tayari wewe ni mtu ambaye umekwishaifungua akili yako kwa ajili ya fursa lukuki za mafanikio. Namaanisha kwamba tayari wewe ni mtu unayejitambua kwani vinginevyo pengine muda huu ungelikuwa unatizama muvi au series. Umeanza sasa kutafuta njia ya mafanikio na maisha yale unayoyataka, na hivyo unaweza kupata kile ukitakacho maishani.

SOMA: Njia mpya za kufanya mambo, Dunia, biashara na ajira vinabadilika kwa kasi ya kutisha.

Siku hizi maarifa na hasa ya pesa na mafanikio yamekuwa rahisi sana kupatikana shauri ya maendeleo katika teknolojia ya intaneti, lakini pia kutokana na wingi na ukubwa wake kama msitu mnne unaweza usiwee kunufaika na chochote iwapo hutajifunza kwa shabaha. Hili nimeliweka wazi sana katika kitabu changu ninachowapa wateja kama zawadi bila kulipa chochote kiitwacho KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO, unaweza kukipata free of charge kwa kujaza taarifa zako kwenye fomu baada ya kubofya hapo kwenye title ya kitabu. Nimefafanua vizuri kwamba, ‘stick’  na program moja ya maana kwanza uokoe muda wako kwani karibu mambo yote ni yaleyale na hakuna jipya chini ya jua.Mzunguko wako wa pesa ukishakaa vizuri ndipo sasa unaweza ukafuatilia program nyinginezo mbalimbali. Ni msisitizo katika kubajeti muda adimu tuliokuwa nao.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiandika juu ya biashara na ujasiriamali, nimeandika pia vitabu na mwaka huu wa 2018 nimeanzisha kampeni kubwa ya SEMINA ZA MICHANGANUO YA BIASHARA BUNIFU ZITAKAZO ‘BOOST’ MZUNGUKO WA FEDHA KATIKA BIASHARA ZA WALE WATAKAOJIUNGA NA MPANGO HUO. Ilikuwa semina hizo zianze rasmi tarehe 3 mwezi huu lakini inaweza ikacheleweshwa kidogo kutokana na kutokukamilika kwa kundi jipya la Whatsapp tuliloanzisha. Hata hivyo washiriki wa semina za zamani na wale wanaoendelea kujisajili kwa kiingilio cha sh. Elfu 10, wanaendelea kusoma masomo ya michanganuo ya biashara katika blogu yetu ya darasa la semina.


Tafsiri ya kitabu cha Think and Grow Rich katika lugha ya Kiswahili imekamilika na sasa kila siku ya Jumatatu na Alhamisi sehemu za tafsiri hiyo zinawekwa katika blogu ya jifunzeujasiriamali, ikiwa wadau mtaamua tunaweza kuongeza siku ikawa mara tatu kwa wiki. Makala za kawaida na programu nyingine zote ndani ya blogu ya jifunzeujasiriamali, zimefanyiwa maboresho ya hali ya juu katika mwaka huu na zitaendelea kuboreshwa kadiri tutakavyoendelea kupokea maoni kutoka kwa nyie wadau wenyewe.

Kwa upande wa vitabu vyetu 3, Michanganuo, Duka la rejareja na Mifereji 7 ya pesa, tumetoa punguzo la bei ya softcopy za vitabu vyote 3, ukinunua vyote 3 badala ya sh elfu 18, unalipa sh. elfu 15 tu na ofa hiyo ni hadi tarehe 10 mwezi huu. Pia Hardcopy za vitabu vyote 3 zinapatikana kama kawaida.

Kama mwandishi nguli wa vitabu vya pesa na mafanikio Robert Kiyosaki anavyosema mara kwa mara katika vitabu vyake vingi; 

"Jifunze kuifanya pesa ikufanyie kazi kuliko wewe kuifanyia kazi pesa. Kuwa na biashara ndiyo njia bora zaidi ya mtu kutajirika, baada ya kuanzisha biashara yako na KUTENGENEZA MZUNGUKO IMARA WA FEDHA, sasa unaweza ukaanza kuwekeza katika vyanzo vingine vya fedha"- Robert Kiyosaki 

Nakutakia mwaka 2018, uwe ni mwaka wako wa MZUNGUKO ULIOKUWA CHANYA WA PESA.

Mwandishi na Mhamasishaji wako,

Peter Augustino Tarimo
self help books Tanzania 

Simu:           0712202244
Whatsapp:   0765553030  








0 Response to "SALAMU ZANGU 2018 KUKUTAKIA HERI NA MAFANIKIO YA KWELI, KWAHERI 2017"

Post a Comment