SEMINA: NJIA ZA UHAKIKA ZA KUBORESHA MZUNGUKO WAKO WA FEDHA 2018 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA: NJIA ZA UHAKIKA ZA KUBORESHA MZUNGUKO WAKO WA FEDHA 2018

Ndugu msomaji wa blog hii, Karibu tena na leo napenda kukushirikisha jambo moja ambalo ndilo litakalokwenda kuwa ufunguo katika kampeni zetu mwaka wote huu wa 2018 tunaokwenda kuuanza masaa machache yajayo. 

Mzunguko chanya wa fedha katika shughuli zetu za kiuchumi ndio kila kitu, ukiweza kuudumisha hautahangaika tena, utapata utulivu wa nafsi na kila kitu kitakwenda barabara.


Ili kudumisha mzunguko chanya wa pesa katika biashara yeyote unayofanya kuna hatua zinazopaswa kuchukuliwa. Nyingi ya hatua hizo tutazijadili katika kampeni zetu lakini lakini, hatua kubwa zaidi ya zote ni lazima kwanza mtu umiliki biashara iliyokuwa na uwezo wa kuzunguka haraka, biashara yenye uhitaji mkubwa kwa jamii, kwa maneno mengine uwe na biashara ambayo soko lake halina mashakamashaka.

Mwaka huu mpya wa 2018 tumeandaa michanganuo maalumu ya miradi bunifu yenye fursa za kipekee. Miradi hiyo imefanyiwa utafiti mkubwa na kuthibitika kuwa na kiwango cha chini kabisa cha hatari(lower risk) pamoja na uwezekano mkubwa sana wa kuzalisha faida na hivyo kuufanya mzunguko wako wa fedha kuwa chanya muda wote.

Katika mwaka huu wa 2018 mwezi wa kwanza tutaanza na mradi mmoja ambao ni mradi wa ufugaji wa kuku. Ijapokuwa ni ufugaji wa kuku wa kienyeji, siyo ufugaji wa kawaida na uliozoeleka hapana, staili yake ni mpya na wala haijapata kusimuliwa mahali pengine popote pale, ni kazi ya ubunifu mkubwa wa kijasiriamali kama ujasiriamali wenyewe unavyotaka kwa mujibu wa kitabu cha “MICHANGANUO YA BIASHARANA UJASIRIAMALI.”.

Habari nyingi kuuhusu mradi huu zitafichuliwa kwa wale watakaoshiriki mafunzo haya ambayo yatafanyika rasmi siku ya Jumatano ya tarehe 3 mwezi Januari 2018 kupitia Blog maalumu ya SEMINA ZA MICHANGANUO pamoja na kundi ‘group’ la Whatsapp kwa namba 0765553030.

Mjadala utaendelea kwa mwezi mzima kabla hatujahamia kwenye mradi mwingine. Kumbuka tumeandaa miradi/biashara 12 zisizokuwa na mashaka yeyote kuhusiana na ulipaji wake.


Ikiwa utapenda kujiunga na mpango huu, kiingilio ni shilingi elfu 10 na utapata fursa ya kushiriki semina zote zitakazofuata pamoja na kusoma masomo ya semina nyingine zilizokwisha pita siku za nyuma. Ikiwa ulishalipia semina zilizopita hautalipa tena, utakachofanya ni kunitumia tu namba yako kwa ajili ya kukuunganisha Whatsapp ikiwa utataka kwani asilimia kubwa ya  masomo ya kwenye blogu ndiyo hayohayo yatakayotumwa whatsapp.

Ili kujiunga, lipa shilingi elfu 10 kupitia namba 0712202244  au  0765553030, jina, Peter Augustino Tarimo, tuma na anuani yako ya GMAIL, isiwe yahoo wala aina nyinginezo. Na kama unatumia Whatsapp, nitumie ujumbe huu kupitia whatsapp “NIUNGANISHE KUNDI LA SEMIA ZA MICHANGANUO” kwa namba 0765553030.

Mwaka mpya huu wa 2018 pia tumetoa OFFA, punguzo la bei kwa wateja wanaonunua vitabu vyetu 3 katika mfumo wa softcopy kwa njia ya email. Badala ya kulipa sh. Elfu 18 kwa softcopy za vitabu vyote 3, utalipa sh. Elfu 15 tu! na kutumiwa vitabu 3 utakavyodownload kwenye simu au kompyuta yako. Offa itamalizika rasmi tarehe 10 January 2018.

Karibu sana kwenye semina, na nakuhakikishia hautojutia kamwe kiingilio chako.

Peter Augustino Tarimo
Self help books Tanzania
Simu:          0712202244

Whatsapp:  0765553030

0 Response to "SEMINA: NJIA ZA UHAKIKA ZA KUBORESHA MZUNGUKO WAKO WA FEDHA 2018"

Post a Comment